TBC inafanya hujuma kwa upinzani bungeni!

Kuna mchezo unaendelea kwa kukata matangazo wabunge wa upinzani wanauliza maswali. Ameanza Joshua Nassari hakusikika akafuatiwa na Deo Sanga wa CCM akasikika, akaja Zitto hakusikika akafuata Diana Chiroro wa CCM akasikika, akafuata Conchesta Rwamulaza kuuliza swali la msingi hakusikika lakini majibu ya waziri yakasikika. Akaja Amina Mwidau wa CUF hakusikika lakini majibu ya Mh Kawambwa na swali la nyongeza la Prof Msolwa yakasikika! Akafanyiwa Agripina Buyogera NCCR, akafuatiwa na Bwanausi CCM akasikika.

Nadhani kwa ushaidi huo hapo juu ni dhahiri kuna hujuma!

Mbona TBC inaeleweka tangu kitambo?
 
Tatizo wabunge wa upinzani wamekunywa viroba asubuhi na mapema. Ndo maana sauti za akina nasari hazisikiki sababu ya viroba

Maelezo yako ya mwanzo kwenye topic hii yalionyesha kama una akili timamu. Huko unakoelekea ni uchizi...matokeo ya kubugia viroba?
 
Ujanja wa kitoto sana, Prof. Possi unaruhusu huu upuuzi?

Japo tunakujua hupendi CHADEMA lakini hicho ni chombo cha umma.

Nawe ni msimamizi tu. Hebu tendeni Haki

Huyu mama anakasumba mbaya na chuki dhidi ya cdm ni hatari
 
Jamiiforums sasa ina wajinga wengi mno, sababu wakati matangazo yanaendelea TBC wameweka tangazo lilikuwa linaslide chenye pale kwamba kuna hitilafu kwenye sauti na sio kweli kwamba ni kwa upinzani ni kwa wote , mtu atafute marudi yake hata asione. Sasa kwan Hansad hakuna, punguzen utoto nyinyi mapunga!
 
Hii ni hujma dhahiri, Wenye kauliza maswali hakusikika pia, ila speaker katika kufujga bunge kasikia, TBC acheni utoto watanzania tunafatilia kila jambo kwa umakini kwa sasa
 
Jamiiforums sasa ina wajinga wengi mno, sababu wakati matangazo yanaendelea TBC wameweka tangazo lilikuwa linaslide chenye pale kwamba kuna hitilafu kwenye sauti na sio kweli kwamba ni kwa upinzani ni kwa wote , mtu atafute marudi yake hata asione. Sasa kwan Hansad hakuna, punguzen utoto nyinyi mapunga!

Ujinga gani wakati nimeleta fact? hivi mitambo iankuwa na hitirafu wanapoongea wapinzani?
 
wewe umejua leo huwa ndo kawaida yao, au ulishaona mjadala wa upinzani unapewa nafasi na TBC, kazi yake nikuongelea vizuri chama tawala hiyo ni kawaida kwa vyombo vya habari africa,
Ila wajue siku zinahesabika:drama::drama::A S thumbs_down:
 
Ttz nn jamani?wote tunajenga nyumba moja knn tugombanie fito?hivi vyama vitapita bt tz itabaki milele acheni mijadala matuc kejeli isiyo na maslahi kwa taifa
 
....vituo kama hiki cha TBC vinavyofanya kazi kwa kubeba udhalimu wa watawala na kuwanyima haki yao wale wa upinzani huwa vinachomwa moto punde wananchi wanapoamua kufanya mageuzi kwa nguvu ya umma....Hawa TBC wamesahau kwamba mishahara yao inalipwa na kodi za watanzania wote..shame on them dogs....
 
Jamiiforums sasa ina wajinga wengi mno, sababu wakati matangazo yanaendelea TBC wameweka tangazo lilikuwa linaslide chenye pale kwamba kuna hitilafu kwenye sauti na sio kweli kwamba ni kwa upinzani ni kwa wote , mtu atafute marudi yake hata asione. Sasa kwan Hansad hakuna, punguzen utoto nyinyi mapunga!
Kwa sababu umetukana unaonaje ukawa wewe punga mfalme.
 
Ile hali iliyojitokeza asubuhi inakera sana. Kwa muda kama nusu saa tunaona picha bila sauti halafu hamna cha apology wala nini. Hivi kweli TV ya Taifa inashindwa na tv za mitaani. Hii ni aibu iliyoje? Unaweza kujiuliza hivi tatizo nini tangu atoke Tido Mhando kama mkurugenzi? Ni kukosa ubunifu au nini? Kwa kweli inakera sana.
 
Back
Top Bottom