Ntemi Kazwile
JF-Expert Member
- May 14, 2010
- 2,182
- 309
Katika tukio la mauaji yaliyotokea Tarime (North Mara Mine) shirika la utangazaji la taifa limeonyesha mapungufu makubwa na kupoteza kabisa umuhimu wa kuwepo kwake, kwa siku mbili mfululizo wametoa kwenye taarifa zao za habari (prime time) za saa mbili kuhusu tukio hili lakini cha ajabu hakuna hata sehemu moja ambapo wamewapa fursa waathirika kueleza upande wao wa habari, kwa siku zote wamemnukuu Kagasheki na Kamanda wa polisi lakini hakuna sehemu yoyote ambapo wamewanukuu wanaotuhumiwa kuvamia mgodi ili nao watupe upande wao lakini hilo halijatokea.
Kwa mtazamo wangu TBC imegeuka kuwa chombo cha wanasiasa walioko madarakani (CCM) na si cha watanzania kama ambavyo sababu za kuundwa kwake zinaeleza, kwa hiyo uendeshaji wa chombo hiki kuendelea kugharimiwa na watanzania wote ni UFISADI, ni bora basi CCM wakakichukua na kulipia uendeshaji wake kwa sababu kinaendeshwa kwa matakwa ya CCM siyo watanzania wote!
Katika tukio la mauaji
yaliyotokea Tarime (North Mara Mine) shirika la utangazaji la taifa limeonyesha mapungufu makubwa na kupoteza kabisa umuhimu wa kuwepo kwake, kwa siku mbili mfululizo wametoa kwenye taarifa zao za habari (prime time) za saa mbili kuhusu tukio hili lakini cha ajabu hakuna hata sehemu moja ambapo wamewapa fursa waathirika kueleza upande wao wa habari, kwa siku zote wamemnukuu Kagasheki na Kamanda wa polisi lakini hakuna sehemu yoyote ambapo wamewanukuu wanaotuhumiwa kuvamia mgodi ili nao watupe upande wao lakini hilo halijatokea.
Kwa mtazamo wangu TBC imegeuka kuwa chombo cha wanasiasa walioko madarakani (CCM) na si cha watanzania kama ambavyo sababu za kuundwa kwake zinaeleza, kwa hiyo uendeshaji wa chombo hiki kuendelea kugharimiwa na watanzania wote ni UFISADI, ni bora basi CCM wakakichukua na kulipia uendeshaji wake kwa sababu kinaendeshwa kwa matakwa ya CCM siyo watanzania wote!
Wakubwa hii tbc si ya kuangalia kabisa,wanakwenda kwenye mikutano ya wakubwa na kuwanukuu bila kuhoji chochote hawana tofauti na uhuru fm siwapendi au nao tuwaite uhuru tv.jamani tuwapongeze itv kwani wameonesha live wakati mbunge anafika,anafukuzwa,unapigwa mawe msafara na pia wakawahoji wananchi.je hii ni tv ya kichaga?naomba waheshimiwa viongozi wa chadema mnijibu ni lini mtakuwa na vyombo vyenu vya habari,kama magazeti,redio na tv?tunapata shida kujua habari.big up.
TUANDAE MAANDAMANO YA KUPINGA UCHAKACHUAJI UNAOENDELEA TBC(vilevile tutake huyu mkurugenzi mpya ajiuzuru). IKISHINDIKANA KWA MAANDAMANO, TUTAANZA KUPIGA MAWE WAANDISHI WA TBC KILA WATAKAPOONEKANA.
Mkuu mapendekezo yako yamejaa hekima: HAKI HUTAFUTWA, haiji kama mvua au hewa tunayopumua. Lazima tuwalazimishe kuwa chombo chetu, mimi binafsi nalipa zaidi ya milioni 15 (hapa sijajumlisha kodi zilizofichwa kama vile VAT na kodi zingine zilizofichwa) kwa mwaka kuchangia shughuli za serikali na ningependa kupata zaidi ... barabara mbovu, umeme haupatikani, hospitali hakuna dawa, hata habari sahihi nisipewe? I SAY NO!