KING KOBRA;Pole sana. Mtume Yohana anaandika kwenye kile kitabu cha Injili ya Yohana kuwa kuna mambo mengi tu aliyoyafanya Yesu na kama yote yangeandikwa vitabu vyote visngeliwezekana kuhifadhiwa.
Kama ni mahali palipo andikwa ambapo Mungu alikusanya watu (aliruhusu) watu wakusanyika halafu akaruhusu wauawe wote ni sehemu nyingi tu katika bublia ila nakikumbuka kisa kimoja cha Samson Mnadhiri wa Mungu. Baada ya toba yake na kilio chake, Mungu alimrudishia nguvu zake ili awaue Wafilisti (Wapalestina wa leo). Walikuja kumdhalilisha Samson. Neno la Mungu linasema, watu alio waua Samson siku hiyo moja tu walizidi wale alio waua wakati wa nguvu zake. Hio si moja tu katika habari za neno la Mungu kuonesha kuwa Mungu hazuiwi na lolote.
Nikuulize swali lingine la kizushi tu; Tuseme weye Mungu wako asingeweza kuzuia hayo yasitokee? Kama angeweza, mbona aliruhusu? Usicheze na uwezo wa Mungu.