Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,346
- 26,138
Salamu zenu wadau!
Leo nawadokeza mambo mawili makubwa ambayo yanawahusisha Tume ya Taifa ya Uchaguzi-NEC na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar- ZEC. Mambo haya mawili ndiyo hasa yanayoonyesha uhusiano uliopo kati ya NEC na ZEC.
Mosi, ZEC ni mawakala wa NEC kusimamia uchaguzi wa ngazi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa upande wa Zanzibar. ZEC hukaimishwa na kukasimishwa mamlaka yote ya NEC kule Zanzibar wakati wa uchaguzi wa Rais na Wabunge wa JMT. ZEC hufanya kazi za NEC Zanzibar.
Pili, kulingana na Ibara ya 66 ya Katiba ya Tanzania ya sasa,wabunge watano wa Bunge la JMT huchaguliwa na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar kutoka miongoni mwa Wawakilishi wote. Ndiyo kusema,BWZ lina haki ya kuwa na Wabunge/Wawakilishi watano kwenye Bunge la JMT.
Uchaguzi wa Wawakilishi kule Zanzibar husimamiwa na ZEC. Na hata Wabunge wa Bunge la JMT kutoka majimbo ya Zanzibar husimamiwa na ZEC kama mawakala wa NEC. Kufutwa kwa uchaguzi wa Zanzibar-wa Wawakilishi ni kutokuwepo kwa Baraza la Wawakilishi na kutokuwepo kwa Wabunge watano wanaotokana na Baraza hilo.
Bunge halitakamilika bila Wabunge toka Baraza la Wawakilishi la Zanzibar. Wabunge wa Tanzania Bara wametokana na uratibu wa NEC. ZEC nao husababisha kupatikana kwa Wabunge kama nilivyoeleza hapo juu.
Hivyobasi, NEC na ZEC zinahusiana vya kutosha. Nasema tena na tena,kufutwa kwa uchaguzi wa Zanzibar kuna athari kwa Tanzania nzima.