Taxi mtandaoni tunaonewa

Taxi mtandaoni tunaonewa

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Posts
16,095
Reaction score
24,323
Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na tabia inayolalamikiwa sana na madereva wa usafiri wa mtandao (Bolt, Farasi, Paisha n.k.) katika eneo la Kivukoni Ferry, Dar es Salaam.
Baadhi ya madereva wa bodaboda wanaopaki karibu na Pantoni wamekuwa wakifanya kitendo cha kuchomoa funguo za bodaboda, au gari la dereva wa Bolt anapofika kuchukua abiria aliyeshuka kwenye pantoni, kisha wanampa askari ambaye askari huchua fedha ambazo hazijulikani ni kiasi gani kwakuwa hakuna control number wanayopewa ili kulipa fedha hiyo.

Ni muhimu kukumbusha jambo moja la msingi: hakuna sheria inayomkataza dereva wa Bolt au usafiri wa mtandao kumchukua abiria wake katika eneo la ferry, iwapo dereva huyo hafanyi kosa la barabarani. Vilevile, hakuna kibao cha barabarani kinachokataza magari ya aina hiyo kufika katika eneo hilo kwa ajili ya kupakia au kushusha abiria.

Kitendo cha mtu kuchomoa funguo za gari la mtu mwingine bila mamlaka ya kisheria kinaweza kuchukuliwa kama uvunjifu wa utulivu na kuingilia mali ya mtu, jambo ambalo si sahihi katika jamii inayoheshimu sheria.

Ni lazima tukubali kwamba dunia imebadilika. Leo hii teknolojia imeleta mifumo mipya ya usafiri kama Bolt, Uber na mingineyo ambayo inawawezesha abiria kuagiza usafiri kwa simu zao. Hii ni sehemu ya maendeleo ya uchumi wa kidijitali na haiwezi kuzuiwa kwa nguvu au vitisho.

Badala ya kulinda “vijiwe” vya zamani kwa migogoro, ni busara zaidi kwa vijana na madereva wa bodaboda kukumbatia teknolojia. Leo hii hata bodaboda zinaweza kujiunga kwenye majukwaa ya kidijitali na kupata wateja wengi zaidi bila ugomvi.

Ujumbe ni rahisi:

  • Tuheshimu sheria.
  • Tuheshimu kazi za wengine.
  • Tukubali mabadiliko ya teknolojia.
Maendeleo hayazuiliki kwa nguvu. Teknolojia imekuja kubaki.
 
Mambo mengine kujitakia kesi za bure tuu laiti ingekua mimi hapo kungewaka aisee
 
Leo nimeona Muhimbili, bodaboda (bolti) tena kavaa kofia ya bolti kabisa, ile anapakia abiria wake. police vidampa wakamrukia wakamnyang'anya funguo.
Raia waliwazonga wale police hadi mateja wakaingilia ndo police wakamuachia yule jamaa
Au Bolt hawalipi kodi , ADMINI JAMII FORUM FICHUA naomba hili jambo muliangazie.
 
Tz hatuendi na kasi ya Tech, unaongelea ferry wakati tax mtandao wanatapata tabu sana kariakoo.

Kupigwa fain ni kawaida kisa wrong parking, tatizo kubwa ni kutokua na uongozi/jumuiya thabiti.

Boda wana umoja wa shari tu, ila mambo muhimu wala hawajuagi waombe vipi zaidi ya kumchangia mama pesa za fomu.
 
Leo nimeona Muhimbili, bodaboda (bolti) tena kavaa kofia ya bolti kabisa, ile anapakia abiria wake. police vidampa wakamrukia wakamnyang'anya funguo.
Raia waliwazonga wale police hadi mateja wakaingilia ndo police wakamuachia yule jamaa
Eti Vidampa, nimechekaa 😂😂😂
 
Kwani dereva wa Bolt anakuwa wapi hadi anapokonywa funguo?
Hawajakutana na mtu aliyepinda zaidi yao, mbona watasimulia hadi mizimu ya kwao.
Lol
 
Back
Top Bottom