Taulo za Kike (Pedi) Ni chanzo kizuri Cha Mapato kwa Serikali?

SCOOBY DOO

Member
Dec 16, 2013
76
69
Leo niliamua kuliangalia swala la PEDI kwa undani Sana. Wakati nikijadiliana na watu kadhaa hasa Vijana wa CCM walionekana kutokujali Sana kwa Kodi hiyo, wao waliona ni sawa, lakini walinikera sana baada ya kuona Vijana hawa hawakujua akina Mama wanaotakiwa kuibeba Kodi hiyo na Mama zao wamo, Dada zao wamo, Shangazi zao wamo, Wake zao wamo, eti mawazo yao yalikuwa yakienda kwa wanawake wanaojiuza tu pale mitaa ya Dar

Huwa nakumbuka kauli ya Katibu Mkuu wao wa CCM kwamba Vijana wa Chama hicho hawana maadili, Wana tatizo kubwa la kimaadili, Sasa kama Katibu Mkuu wao amekiri hivyo mi Nani nipinge? Utasema alimwambia Makonda, mi nasema Makonda Ni sample sahihi, na kama Makonda anayeaminika Sana Hana maadili nani ana maadili humu.

Baada ya kutaja orodha wa Ndugu zao ambao ni wanawake ndipo wale Vijana walianza kupoa na mmoja mmoja kuaga. Niliwakumbusha kuwa watoto wengi wa kike huanza uhuni mapema kwa sababu ya mahitaji Kama Pedi na nguo za ndani. Niliwauliza ni nani Kati yao aliwahi kumpa mke wake pesa kwa ajili ya pedi, maskini Kati ya Vijana sita ni mmoja Ndio alionesha amewahi kuombwa Mara moja pesa hiyo na mke wake na hakumpa!!! Swali ni kuwa wanazipataje??

Kwa sensa iliyopita NBS inaonesha jumla ya wanawake waliopo Tanzania ni 23,053,933 na Kati ha hao wenye umri wa kuanzia miaka 14 na kuendelea ni kama nusu ya wanawake wote Yaani 11,526,966 Yaani Hawa wanaweza kuingia hedhi. Sasa twende vizuri tujue ni Nini Serikali ya CCM na Mataga wanakata kwa biashara hii.

Free style ambayo nafikili inatengenezwa nchini inauzwa shilingi 2,000 na zinakuwemo peace 8. Kwa wastani mwanamke anaweza kuingia hedhi kwa muda wa siku 3 Mpaka 5 na wengine Mpaka 7. Kwa hivyo kwa siku moja mwanamke ambaye hatokwi na damu nyingi anaweza kutumia taulo 3 na kwa wale wanaotokwa na damu nyingi hufikisha taulo tano Mpaka saba!!!

1: Sasa tuweke wastani wa taulo 4 kwa siku Mara siku nne, maana yake mwanamke mmoja atatumia wastani wa taulo 16
2: Kodi ya taulo za ndani itakuwa 10% na taulo za nje 25% na Bei free style Ni 2000, tufanye bila kujali bidhaa ni ya ndani au imetoka nje, kodi inaweza kuweka ongezeko la Mpaka sh 500 (peace 8) kwa round figure.
3: Kwa hiyo tukichukua Kodi ya Tsh 500 mara 2, mwanamke mmoja atalipa Tsh 1,000 (Kodi) kwa mwezi mmoja, kwa mwaka mzima atakuwa amelipia Kodi ya kuingia Hedhi kiasi Cha Tsh 12,000 hivi.
4: Kwa hiyo kwa wanawake 11,526,966 x Tsh 1,000 watalipa 11,526,966,000 kwa mwezi mmoja. Na kwa mwaka mzima itakuwa 138,323,592,000 Tsh.

Kwa hiyo sio chanzo kibaya Sana hiki, Mataga wanapaswa kuhamasisha chanzo hiki ha ha ha
 
Back
Top Bottom