Tatizo Sio Magufuli...

Wateule

JF-Expert Member
Sep 17, 2010
390
368
Albert Einstein aliwahi kusema "A problem cannot be solved with the same mind set that created it." Watangulizi wake pia waliunda tume na kuja na report kama hizi, lakini mwisho wa siku na wao walifanya yao na kuondoka. Kwa mfano, report imetaja mawaziri na viongozi wengine wa serikali za awamu ya tatu na nne. Lakini, mawaziri hawa waliweza vipi kufanya madudu yale kwenye mikataba mikubwa kama ile bila mawaziri wakuu na marais wa awamu hizo kujua?

Magu ameshatangaza kwamba katiba sio kipaumbele chake, sasa je atawashughulikia vipi (kama anao ujasiri huo) marais hawa wastaafu (JK na Mkapa) kwa katiba hii ambayo ina walinda wasishtakiwe kwa makosa ya urais wao? Vipi ile kauli yake ya kwamba yeye "atawalinda wastaafu"?

Ukijiuliza maswali hayo na kupata majibu sahihi, utaona kwamba huu ni muendelezo tu wa kucheza na hisia (appeal to emotions) za Watanzania ili kujipatia umaarufu wa bei nafuu (cheap publicity). Hii inadhihirika kwenye mbwembwe na shamrashamra za makabidhiano ya report hizo (mambo yanafanyika LIVE wakati Bunge LIVE hataki lionekane). Tukirudi kwenye ile kauli ya "A problem cannot be solved with the same mind set that created it" utagundua kwamba tatizo sio Magu wala hizo report zake mbili, tatizo ni CCM ambayo imejaa watu walafi na wabinafsi, na watu hao hawagusiki na CCM wenzao.
 
Hyu anajisumbua tu na porojo zake hizi...

Watanzia sis n watu wa ajabu sana hiv waziri anaweza kusain bila Rais kujua????

Magu asituletee porojo zake
 
Huyu bwana anacheza tu na emotions za watu..

Anatufanya sisi wote mazuzu..

Abadili katiba akamate Mkapa na Kikwete kama yeye kweli ana uchungu na Madini yetu..

Hawezi kufanya hilo he has no right kutudanganya..

Watanzania wa leo sio mazuzu.
 
Back
Top Bottom