Tatizo nini? 38% ya watoto wa Mbeya wamedumaa

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,735
Miaka yote tunaaminishwa Mbeya kuna misosi hatari. Vyakula kama chips unaweza kupewa hadi ndoo nzima kwa Buku. Watu wa Mbeya ni wakubwa kimiili. Wanawake ndio usiseme wakubwa kimiili na wababe.

Imekuwaje leo tena watoto wengi wanadumaa hivyo? Maana wakidumaa mwili na Ubongo unasinyaa wakiwa watu wazima Mbeya inakuwa na watu wa ovyo ovyo...

Mlioko huko mtusaidie, Tatizo nini...

Chanzo: The Citizen la leo
-----------

UPDATE: Nimeattach Document ya Research on poverty alleviation(REPOA): Institutional anaysis of nutrition in Tanzania japo hii ni ya zamani kidogo hali ilipokuwa nzuri zaidi. Page ya Saba ramani ya asilimia ya watoto walivyodumaa kwa mikoa
 

Attachments

  • Special_Paper_09.31_.pdf
    589.3 KB · Views: 29
Ebu elezea wamedumaa kivipi.na useme mbeya ya wapi?
20170403_043137.jpg

soma heading pale juu, ila nadhani ni wastani.
au ukubaliani na hii habari
 
Nadhani tatizo ni aina ya chakula kinacholiwa. Unakuta mtu anakula wanga peke ake from morning to morning.. Na hilo tatioz mikoa kama Dodoma na mengime ya kanda ya kati ni worse, hiko percentage ya udumavu utaona Mbeya kuna afadhali. Lishe inamaanisha chakula chenye virutubisho vyote
 
sio mbeya tu mikoa yote ya nyanda za jutw mito imekauka samaki hakuna wanakula wanashiba starch wanasahau kuwa kuna protin na vitamin zinatakiwa mwilini,we kitoto kinapewa kiazi au mihogo kila siku unategemea nini
 
Tatizo la wakinamama Wengi wazazi wako bize kufanya biashara na kusahu suala la malezi pamoja na lishe bora kwa familia. Utakuta mama ametoka kujifungua ndani ya wiki tu lakin yupo sokoni na kitoto kichanga.

Hivyo chakula sio tatizo, Tatizo ni muda wa kuandaa hicho chakula chenye lishe bora kwa watoto.
 
20170403_043137.jpg

soma heading pale juu, ila nadhani ni wastani.
au ukubaliani na hii habari
Nmekuuliza hivyo kwakua hiyo habar licha yakutokukubaliana nayo ,siyo ya kweli labda kama kuna kudumaa kwa aina nyingine .naifahamu mbeya nje ndani .
 
Hiyo kitu nimeiona hata mkoa wa rukwa watoto wengi wana matumbo makubwa hadi huruma.
 
Tatizo la wakinamama Wengi wazazi wako bize kufanya biashara na kusahu suala la malezi pamoja na lishe bora kwa familia. Utakuta mama ametoka kujifungua ndani ya wiki tu lakin yupo sokoni na kitoto kichanga.

Hivyo chakula sio tatizo, Tatizo ni muda wa kuandaa hicho chakula chenye lishe bora kwa watoto.
Kweli mikoa ya mikoa ya mbeya rukwa na katavi wakina mama ndo watafutaji wa ela na walezi wa watoto kiukweli hali inatisha katika hiyo mikoa nimejionea mwenyewe siyo ya kuhadithiwa
 
Nmekuuliza hivyo kwakua hiyo habar licha yakutokukubaliana nayo ,siyo ya kweli labda kama kuna kudumaa kwa aina nyingine .naifahamu mbeya nje ndani .
Huu utafiti umefanywa na repoa. kupita parabarani na kuona watu sio utafiti mkuu.
Tuheshimu watafiti ili tupate sakafu ya kuanzia kutatua tatizo.
Watoto wa chini ya miaka 5 wanadumaa na ukuaji wao uko chini ya kiwango.
Ila nashangaa Why mbeya inazidiwa na Tabora.
 
Kule wanaamini sana nguvu za giza na usikute wanakomoana wenyewe kwa wenyewe, matokeo yake wanajaza mkoa na mataahira kibao ili washindane na mkoa wa Tabora unaoongoza kuwa na mataahira hapa nchini.
 
Unalosema ni kweli , mbeya ina wilaya nyingi. Na ni mkoa mkubwa. Ulikua mkubwa zaidi kabla hawajaigawa kuwa mokoa mowili, mkoa dada ukiwa ni songwe.

Tatizola mbeya sio upatikanaji wa chakula.
Ila shida ni elimu ya lishe. Wakazi wa mbeya hasa wa vijijini wana elimu ndogo, sana ya lishe hivyo hawazingatii ulaji wa lishe bora hasa kwa watoto wao.

Njia ya kutatua hilo ni kuwapelekea wataalau wanlishe ili wawapatie elimu, pamoja na kuwahamasisha wakaazi juu ya lishe bora. . .

Naamini serikali imeshaliona hilo kabla ya hata ripoti hiyo ya gazeti la mwananchi. Na ninaamini juhudi zilishaanza kuboresha lishe ya watoto wa mbeya.
 
Tafiti za kibongo bwana usikute twaweza. Au utafiti ambao umefanywa na watu kama akina bashite
 
Back
Top Bottom