Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 20,319
- 38,456
Kuna Hoja inazunguka humu JF kuwashangaa wabunge wa UKAWA na wale wa CCM kuungana dhidi ya aina ya mbinu anazotumia mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kwenye mapambano yake dhidi ya biashara haramu ya madawa ya kulevya. Imefikia mahali wengine wamehoji kama kuna haja ya kuwa na wapinzani iwapo katika hili la Makonda wameungana na CCM.
Kwenye Bunge mara zote wabunge wa upinzani huungana na Wabunge wa CCM linapokuja suala lenye maslahi kwa taifa ama kwao binafsi. Na wakati mwingine hata kuhatarisha uhusiano wao na wabunge wenzao toka vyama vingine vya Upinzani. Lakini mara zote ni wabunge wa CCM ndiyo hukataa kuungana na wabunge wa Upinzani kwenye masuala yenye maslahi mapana kwa taifa letu.
Wakati ule wa Kashifa za Meremeta, Tanglod, EPA, Richmond, Katiba Mpya, Operesheni Tokomeza,Buzwagi, na mengineyo mengi sana, ni wabunge wa CCM ndiyo wamekuwa kinyume na wabunge wa Upinzani.
Nakumbuka kuna wakati ndani ya bunge hupitishwa miswada Akidi ya wa wabunge ikiwa inatiliwa shaka kama inakidhi haja ya kupitisha miswada hiyo, lakini wabunge wa CCM huipitisha bila wasiwasi. Kwenye Bunge la Katiba misimamo wa wabunge wa CCM na wapambe wao ilikuwa ni kukubaliana kwa kila hali na mapendekezo yote yaliyokuwa yanaendena na mtizamo wa Rais wa wakati ule Jakaya Mrisho Kikwete.wakati Wabunge wa UKAWA walikuwa wanatetea maslalhi ya wananchi wataunganaje?
Nakumbuka Mnyika akiwa peke yake alipambana kujaribu kuzuia Mahakama kuingiliwa na mhimili wa Utawala kwa kupinga mswada ulioleta sheria ya kuwafanya wakuu wa mikoa na wilaya kuwa ni wenyeviti kwenye kamati za nidhamu za mahakimu. Wabunge wa CCM waliunga mkono kila pendekezo lililoletwa na serikali kwenye mswada huo. Hapa nani wa kulaumiwa?
Kwenye tukio la juzi ni Mbunge Mwita Waitara wa CHADEMA ndiye aliyeleta hoja lakini wabunge wa CCM ambao kwa sasa ndiyo wameanza kuona wanapoteza nafasi yao kwenye jamii kwa kukubali bunge kufanya kila linaloamuliwa na serikali, walimuunga mkono Waitara! Wakati ule wa mjadala wa Bunge kuoneshwa ama kutokuoneshwa Mubashara unadhani ni wabunge wa UKAWA ama wa CCM waliokuwa sahihi?
Tatizo la Bunge kutokuwa kitu kimoja haliletwi na wabunge toka Upinzani bali linaletwa na wabuge wa CCM!