MIXOLOGIST
JF-Expert Member
- Mar 1, 2016
- 13,962
- 35,087
Habari za mchana wana JF,
Nimebahatika kufanya tafakari kidogo kwenye hili swala la viroba, kinachonitatiza ni kujua je tatizo ni viroba au wanywa viroba?
Tofauti na madawa ya kulevya ambayo yenyewe peke yake ni haramu kwa mujibu wa sheria za nchi, lakini kiroba kama kifungashio au kinywaji kilichopo ndani yake si vitu ambavyo ni haramu kwa minajili ya sheria zetu.
Zipo tafsiri ambazo siyo sahii kwamba pengine vifungashio vinaweza vikawa vinachafua mazingira na mawazo mgando ya namna hiyo. Ila bado suluhisho makini halijapatikana. Upo uwezakano wafanyabiashara hawa wanaouza hizo pombe wakaja kwa namna nyingine, wakaweka ujazo mdogo wa pombe hiyo hiyo kwa style nyingine. Sasa lazima serikali ileleze bayana inachozuia ni vile vikaratasi vinavyofungia pombe, pombe yenyewe au pombe yenyewe kwenye ujazo mdogo.
Nawaza kwa maandishi tu, Ahsanteni