Tatizo letu kama Nchi bado tunafikiri kijamaa wakati tupo kwenye mfumo wa ubepari.

JERUSALEMU

JF-Expert Member
Sep 19, 2012
3,112
3,536
salamu kwenu wanabodi.

Viongoz na wanao ongozwa wote tatizo lao ni moja! wanawaza na kutenda kijamaa wakati tupo kwenye mfumo wa kibepari. Na hili limejidhihirisha dhahiri katika awamu hii ya tano kuliko wakati mwingine wowote.Tukijitahidi kutoka katika tope hili tunaweza kupiga hatua kubwa kiuchumi.Nitajitahidi kufafanua kila jambo ili wanajamvi waweze kunielewa.

Tatizo la kuadimika na kupanda bei kwa sukari kwa kiasi kikibwa limesababishwa na serikali. kwanini? serikali inasema inataka kulinda viwanda vya ndani kwahiyo wafanyabiashara wakazuiwa kuleta sukari kutoka nje ya Nchi!Wewe jiulize wale wenye viwanda siyo wafanyabiashara? ni wafanyabiashara.Tena kwakuwa hawako wengi wanaweza kuamua kutengeneza mazingira ya sukari kuadimika ili wapandishe bei kwa visingizi mbalimbali kama kupanda kwa gharama za uendeshaji.Dawa ya kuzuia bei ya bidhaa isipande kiholela ni kuifanya bidhaa hiyo ipatikane kwa wingi kuliko mahitaji ili wauzaji washindane kuuza kwa be inayo vutia wateja na siyo vinginevyo.

Hebu fikiria hivi, kama muagizaji wa madela yale mavazi ya akina mama angekuwa mmoja tu Nchi nzima unajua bei yake ingekuwaje? pengine dela moja lingeuzwa kwa shs 200,000/!! bei ya madela haipandi ovyo kwasababu waagizaji wako chungu nzima kwahiyo bei sokoni imejirekebisha yenyewe wala hatuhitaji EWRA wa mavazi

Kuna jambo baya lina anza kujitokeza sasa mingoni mwetu, nayo ni chuki ya wasio nacho dhidi ya walio nacho.Ukiangalia kwa undani utagundua kuwa mtazamo wa wasio nacho ni kama wanaona kila mwenye nafuu fulani ya maisha ni fisadi! kulipwa mshahara mkubwa sasa hivi ni dhambi! na ndio maana utawasikia baadhi ya watu wakisema , afadhali sasa tutafanana na heshima itapatikana! wanataka tajiri afanane na masikini badala ya kutamani masikini afanane na tajiri! ndio kuwaza kijamaa.tunawaza juu ya jamii isiyo na matabaka yaani jamii ya watu wasio na uchu wa mafanikio. bila ushindani hakuna mafanikio.Unatamani mtu mwenye Phd alipwe sawa na darasa la saba!
 
Ndugu yangu, Tanzania haijawahi kuwa kwenye mfumo wa ubepari; na hata sasa hatuko kwenye mfumo wa ubepari kwa sababu hatuuwezi. Mabepari wenyewe walishaushindwa.
 
Ndugu yangu, Tanzania haijawahi kuwa kwenye mfumo wa ubepari; na hata sasa hatuko kwenye mfumo wa ubepari kwa sababu hatuuwezi. Mabepari wenyewe walishaushindwa.
Bora mabepari karibu wote wana nafuu ya maisha kuliko ujamaa ambao hata mwanzilishi wake alikiri ulimshinda. Kwani ubepari ni nini? in its simlest definition is SURVIVAL IS FOR THE FITTEST! baasi maana yake you donot struggle to survive you die.Hata katika biashara waache watu washindane wajaze bidhaa sokoni utaona bei haipande ovyo.
 
Ndugu yangu, Tanzania haijawahi kuwa kwenye mfumo wa ubepari; na hata sasa hatuko kwenye mfumo wa ubepari kwa sababu hatuuwezi. Mabepari wenyewe walishaushindwa.
MM, kwa sasa tuko kwenye mfumo gani? Ujamaa hatupo, Ubebari hatupo, tupo kwenye MFUMO HOLELA!
by the way, Ujamaa ni mgumu, ni China pekee inauweza. Wenzetu China angalau wanajitosheleza, sisi bado hatujitoshelezi. Kule China makampuni yote makabwa ni State Owned kama siyo Jimbo, Jeshi au Serikali kuu. Makampunu mengi ni ya Serikali! Je sisi kama ni Wajamaa, Serikali ina makampuni ya Biashara? Kiuhalisia, sera yetu HAIKO BAYANA, yaani Ujamaa hatupo, upebari hatupo!
 
hakuna nchi yeyote dunian na kama hipo basi itakuwa kuzimu au peponi lakini c dunian ambayo imeendelea bila kupitia kama ambavyo Leo Tanzania tunapitia ktk kipind hiki huwez kuendelea bila kuwa na heshima na fedha ilifikia watanzania tunatumia kadri tunavyopata so hasara ya kufanya uchumi holela kila mtu ana access ya kufanya anachotaka kwa kigezo cha haki za binadamu na biashara huria hata marekani ambako kuna wafanya biashara kweli kwani huku kuna wachuhuzi tu wamarekani wanaheshimu serikali yao na heshima cku zote uanzia kwa wazazi ambayo ktk level ya nchi ni serikali naamini sasa watanzania tutajifunza kusave tutajifunza kutumia si kadri tunavyopata bali kadri inavyobidi

leo tukikubali kikundi cha watu wachache wakaamua hatma ya watanzania wote kwa kigezo cha biashara huria leo nani anaweza kunitajia mfanya biashara gani anaweza kuisumbua serikali ktk hizo nchi mnazozitolea mfano kimaendeleo na kiuchumi? ? najua ukipeleka amri kumi za mungu kuzimu wataisi wanaonewa na ndo watanzania hatukuzoea kuishi ktk misingi ya kuheshimu mamlaka na kufata sheria na taratibu

najua watanzania tumekosea kidogo tu lakini kama tukijua tulipokosea na kupafanyia kazi tatizo leo wanaokwenda kufanya kazi serikalini wengi ni wale waliokuwa vilaza na wajinga mashuleni lakini wale smart kichwani wanakwenda private sector kitu ambacho ni tofauti na wenzetu ma great thinkers wengi huwa serikalini so tunakosa watu wenye mawazo chanya ya kutuvusha hapa tulipo
 
Back
Top Bottom