Responded Tatizo la Wizi wa Mita za Maji na pendekezo kwa mamlaka husika

Responded Tatizo la Wizi wa Mita za Maji na pendekezo kwa mamlaka husika

Asantehene

New Member
Joined
Nov 18, 2025
Posts
3
Reaction score
0
1770884723386.png

Wakuu nimekutana na hii hoja, nimeona niiweke hapa iwafikie wadau wengi zaidi, na DAWASA kama wanaweza kujibu itakuwa vizuri zaidi.

Majuzi tuliamka tukakuta mita yetu ya maji haipo. Cha kushangaza, mita tatu zilizo karibu hazikuguswa. Wazo la kwanza lililotujia ni kwamba huenda DAWASA wameitoa kwa sababu hatujalipa bili. Lakini swali likabaki: kwa nini mamlaka iondoe mita bila kushirikisha wateja?

Baada ya kupiga simu na kufanikiwa kumpata mhusika anayesoma mita mtaani kwetu, alitueleza kuwa hii ni taarifa ya 36+ kuhusu upotevu wa mita. Kwa mujibu wake, kuna wimbi la wizi wa mita za maji.

Nilipomuuliza kwa nini mita yetu pekee ndiyo imeibiwa, akasema kwamba mita za chuma ndizo “deal” mjini kwa sababu zina madini yanayoweza kuuzwa. Mita yetu ilikuwa ya chuma, na zile tatu zilizobaki sio za chuma, hivyo hazina thamani ya kifedha kwa wezi.

Hoja Kuu

Kile ambacho hakieleweki ni kwa nini DAWASA haijachukua hatua ya kubadilisha mita za chuma ambazo wanajua ni kivutio cha wezi, na badala yake kusubiri hadi wananchi waibiwe ndipo waanze mchakato wa kuripoti na kufunga mita?

Hali hii inaleta:
  • Upotevu wa muda na fedha: mchakato wa kuripoti na kusubiri fundi kufunga mita mpya ni mzigo kwa wananchi na gharama kwa mamlaka.
  • Usumbufu wa huduma: wateja hukaa bila maji kwa muda mrefu wakati wakisubiri mchakato wa kurejesha...ikitokea bahati mbaya huna 50K ya kulipia mita mpya itabidi uishi bila maji!
Mapendekezo

Ni muhimu DAWASA kuwa proactive badala ya kusubiri, hatua zinazoweza kuchukuliwa ni:
  1. Kubadilisha mita zote za chuma kwa mita za kisasa zisizo na thamani kwa wezi.
  2. Kuweka mita kwenye maeneo salama zaidi, si nje wazi.
  3. Kuongeza uhamasishaji wa wananchi kuhusu kuripoti mara moja na kushirikiana kulinda miundombinu ya maji.
NB. Nimeambiwa Arusha nako wanazipitia!

Pia soma ~ Milioni 2 kutolewa kwa watakaotaja wezi wa mita za maji Moshi
 
Back
Top Bottom