Tatizo la wanasiasa wa kuibuka, na uzuri wa wanasiasa wa kutumikia Umma daima

Yoyo Zhou

Member
Jun 16, 2020
72
111
Uchunguzi mpya uliofanywa na chuo kikuu cha Harvard cha Marekani umeonesha kuongezeka kwa kiwango cha raia wa China kuridhika na utendaji wa serikali ya nchi hiyo tangu mwanzoni mwa karne hii kimeongezeka na kuwa zaidi ya asilimia 90, kufuatia kuboreshwa kwa maisha yao. Ripoti hiyo imesema kuanzia mwaka 2003, kiwango cha wananchi kuridhika na serikali kimekuwa kikiendelea kuongezeka kwa pande zote. Kuongezeka huko kunatokana na matokeo yaliyopatikana kwenye utekelezaji wa sera za taifa hadi utendaji wa maofisa wa serikali za mitaa. Raia wa China wanaona serikali imekuwa na uwezo na ufanisi mkubwa zaidi wa kutatua changamoto zao kuliko zamani

Tarehe 20 Julai tovuti ya rasmussesn inayofuatilia uungaji mkono wa wananchi kwa serikali ya Marekani imetangangza kuwa asilimia 33 ya wananchi waiunga mkono serikali ya rais Trump, na asilimia 45 hawaiungi mkono serikali hiyo. Moja kati ya mambo yanayofanywa serikali ya sasa ya Marekani kuwa na uungaji mkono mdogo, ni kushindwa kushughulikia ipasavyo changamoto za wananchi kama vile maambukizi ya virusi vya Corona na kushangaza watu, ni kuwa serikali ya nchi hiyo imekuwa na changamoto kubwa kwenye mapambano dhidi ya virusi vya Corona. Sababu moja ya hali hiyo ni Rais wa Marekani Donald Trump kutokuwa na mipango mizuri ya kukabiliana na hali hiyo. Kwani toka mwanzo alipoingia madarakani, anapenda ufuatiliaji wote uwe kwake, na sio kwa wengine.

Tukijaribu kuangalia baadhi ya sababu za kuwepo kwa tofauti hizi, tunaweza kuona kuwa kuna tofauti kubwa sana kwenye namna ya kuchagua viongozi wa utumishi wa umma kwa pande hizo mbili. Kwa wanaofahamu historia ya Bw. Trump watakumbuka kuwa huyu ni mtu aliyekuwa alikuwa ni nyota wa televisheni, na mfanyabiashara anayeshughulikia na biashara ya ujenzi na uuzaji wa nyumba.

Mtindo wa kuendesha vipindi vyake vya televisheni na kampuni yake ya biashara ya nyumba, ni wa yeye kuamua kila kitu kama anavyopenda. Tabia hiyo amejaribu kuingia nayo Ikulu, na kuleta matatizo makubwa kwenye mambo ya utawala. Amekuwa akitofautiana na wataalamu ambao wanapenda kinyume na maoni yake, na kuona kama wanajaribu kuzuia umaarufu wake. Inawezekana hii ni moja ya sababu kuu za kufanya uungaji mkono wake uwe mdogo.

Kwenye siasa za China ni vigumu kupata kiongozi kwa njia kama ya Marekani, yaani nyota anaibuka kutoka kusikojulikana na baada nusu mwaka anakuwa rais. Kuwa mwanasiasa nchini China hadi kufikia hatua ya kuwa kiongozi, mtu anatakiwa awe amepita kwenye mchakato mrefu na awe rekodi safi ya utumishi wa umma.

Hakuna uwezekano wa mtu kuibuka leo kuwa diwani au mbunge, na kesho kuwa waziri au balozi. Kwa hiyo mwanasiasa anapoingia kwenye nafasi yoyote, ufanisi wa utendaji wake kimsingi unahakikisha na sio wa kubahatisha. Inawezekana kuwa hii ni moja ya sababu za serikali ya China kuwa na uungaji mkono mkubwa.

Kila nchi ina mfumo wake wa kuchagua viongozi, lakini bila kujali ni mfumo gani unafuata, jambo la muhimu ni kuwa mfumo huo unatakiwa kuleta viongozi wanaotatua matitizo ya wananchi, na si vingevyo. Siasa za kuchagua viongozi kwa njia ya “sandakarawe” ni sawa na kufanyia bahati nasibu matatizo ya wananchi.

1595318459797.png

1595318468051.png
 
Back
Top Bottom