steveson manumbu
JF-Expert Member
- Apr 1, 2014
- 887
- 178
Mchambuzi na mwelimishaji wa mambo ya vijana kutoka ENREDO .
Tatizo letu Vijana tumekuwa ni watu wenye kusubiri kitu kikubwa kitokee ndipo tuchukue hatua jambo ambalo ni kinyume na kanuni za mafanikio.
Jambo la msingi kwako kijana tambua kuwa tabia ya kudharau au kushindwa kuanza na jambo dogo ndio imekuwa likitufanya vijana wengi tushindwe kufanikiwa maana hatuthamini mambo madogo ili hali mafanikio yanahitaji tuanze na mambo madogo na hatimaye tunakomaa na kufikia mambo makubwa zaidi na zaidi. Hivyo basi kwako wewe kijana unayesitasita kuanzisha mradi wako eti kisa una mtaji kidogo vunja hofu hiyo na nenda kaanzishe biashara yako.
Jiulize uliona wapi mtoto akaanza kutembea kabla ya kutambaa?, sasa mbona tunakimbilia kwenye kutembea kabla ya kutambaa? Ni jambo ambalo haliwezekani, ni muhimu kujifunza kuwa tunaweza kuanza na kiasi kidogo cha fedha hatimaye nidhamu, uvumilivu, juhudi na malengo vikatuongoza mpaka kuweza kufikia hatua ya kuwa wafanyabiashara na wajasiriamali wakubwa