Kurunzi
JF-Expert Member
- Jul 31, 2009
- 9,300
- 9,936
Wanabidi wataalamu wa afya naomba msaada wenu, mtoto wa ndugu yangu anaumri wa miaka 5, alikuwa analalamika sana kuwa anapata maumivu ya tumbo baada ya kula chakula na walipompeleka Hospitali madaktari walikuwa wanamuandikia antbiotic lakini hata huvyo hazikuweza kumsadia mpaka wiki mbili zilizopita alipokwenda hospitali na kumkuta dr. mmoja aliweza kubaini tatizo la huyo mtoto kuwa anatatizo la utumbo mpana ni mrefu kuliko kawaida hali inayopelekea uchafu kubaki tumboni na kumsababishia maumivu ya tumbo.
Kwa hiyo Dr. amemuandikia dawa za kutumia kwaajili ya kutoa uchafu then waangalie uwezekano wa kufanyiwa upasuaji.
Tokea kupewa taarifa hiyo wazazi wa mtoto wamekuwa na majonzi na hajui hatima ya mtoto wao. Napenda kwa niaba ya familia hiyo kuomba msaada wa mawazo na ushauri kwa wale ambao wanalijua au wamekumbana nalo tatizo hili tuweze kushare hapa,
Natanguliza shukrani za dhati.