princess square
Member
- Dec 5, 2019
- 62
- 99
Wanajamvi natumai nipo sehemu sasa ambapo naweza kupata msaada kutoka wa wataalam wa JF.
Wakati nipo Dar nilikuwa natumia mtandao wa TTCL kwenye vifurushi vya internet na kasi yake ilikuwa ni ya kuridhisha kulingana na matumizi yangu.
Wiki iliyopita nimeingia Kigoma ndipo nimeanza kupata tatizo na kero za huu mtandao speed yake ni ndogo sana inasoma 0B/s.
Nikawapigia huduma kwa wateja nikakutana na kero nyingine zaidi ya dakika 20 wananisilikizisha visauti vyao bila kupokea simu yangu.
Nilipiga zaidi ya mara 3 na kutumia dakika 57 bila kupokelewa simu yangu.
Nilivyo mzalendo nikajifika kwenye ofisi zao Kigoma Mjini karibu na ofisi ya posta "niliambiwa eneo niliopo halina tatizo lolote labda tatizo lipo kwenye simu yangu".
Nikajikuta namtazama mtoa maelezo nikibaki nasikitika maana maelezo aliyokuwa ananipa sijui amesoma wapi kwa kweli niliumia sana.
Binafsi sina elimu ya mambo ya IT lakini JF imenitoa ushamba.
Nikaenda kwa mhudumu mwingine kupata msaada zaidi, naye akanidirect kwa mtu wa data kwa kunirudisha kwa mtu yule yule.
Hasira zikaanza kunipanda maana nilikuwa na kazi ya muhimu kuifanya ilinibidi niondoke tu bila tatizo langu kutatuliwa
Naombeni msaada namna ya kusolve hili tatizo au mwenye namba ya mtaalamu wa data kutoka Dar es salaam aweze kunisaidia.
NB: Nimeanza kutumia TTCL mwaka 2015 lakini sasa naona uzalendo utanishinda kwa kweli.
Naomba kuwasilisha kwenu.
Sent using Jamii Forums mobile app