Wanajamvi..
Kwa muda mrefu imekuwa nikitafakar tatizo has la timu yetu ya taifa kushindwa kufanya vzr ktk mechi zake mbalimbal,
nikagundua makocha tulionao sio wazur kwenye kutafuta ushindi...wachezaj wetu hawatofautian sana viwango na nch zingine nying za afrika ila tatizo ni kocha!!!...siku tukipata kocha sahihi...hakyanani tunaoboa afcon na hta wc
Matatizo ya timu ya taifa
Tatizo la kwanza ni AFYA
wachezaji wetu wana afya mbovu. Hii inatokana na ukweli kwamba tanzania misosi haba, lishe bora unatakiwa uanze kuipata tangu ukiwa mtoto mdogo, mifupa yako, misuli yako n.k vinakuwa vinajengeka vyema kadri unavyokua.
Kwa sisi unakuta mtu ameshavuka umri wa miaka 20 ndio anapata nafasi ya kula mlo unaostahili. Kabla ya hapo nyumbani ugali mkubwa kama nyama imepika siku hiyo huruhusiwi kuchukua kipande zaidi ya kimoja, vinginevyo unaambiwa unakomba mboga.
Kwa jinsi unavyopata chakula haba na mwili wako unajijengea mazingira ya kutohitaji chakula kingi ukila kidogo tu umeshiba. Kuna mchezaji mmoja wa tanzania alipelekwa kwenye majaribio ulaya, wakawa wanamuandalia chakula, wakati anasubiri msosi wakampa appetizer ale. Hakumaliza appetizer akampa muhudumu kwamba ameshiba. Jamaa wakashangaa huyu mtuu hata msosi wenyewe hajaletewa ameshashiba.
Wakampeleka uwanjani kumjaribu wakamuona stamina sifuri, wakaachana nae.
Ukiafuatilia wachezaji wa zamani kidogo walioleta sifa TZ mfano Pondamali, Peter Tino, Mohamed Yahya Tostao n.k utaona walikuwa ni watu wenye miili iliyoshiba na iliyokubali mazoezi.
Ukiangalia simba waliofika fainali ya kombe la CAF Hoza, Banda, Magoso, RP, Soma n.k utaona walikuwaje, kwenye timu ambaye alikuwa kidogo mdhaifu alikuwa marehemu Edo.
Tatizo la pili ni Nidhamu na kutojiwekea malengo makubwa na kuwa na kiu ya kuyatimiza.
Utakuta mchezaji mlevi, kitombi tu kutaka sifa za kijingajinga ambazo zinamuharibia kiwango chake cha uchezaji.
Wachezaji wameridhika na sifa wanazopewa wakiwa TZ na focus yao imeishia hapohapo TZ.