Tatizo la space kwenye Samsung tablet 2, naomba msaada

Tatizo la space kwenye Samsung tablet 2, naomba msaada

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,931
Reaction score
3,256
Wapendwa, ninamiliki tablet 2 Samasung huu mwaka wa pili. Kuna tatizo linanisumbua, kila mara inaonyesha kujaza data, wakati nimefuta karibu kila kitu kwenye gallery.

Je, itakuwa imejaza nini, au ni virus? Naombeni msaada wataalam.
 
Ukifuta kwenye gallery inaweza isisaidie kwa sababu hizi.

1.Picha hazili space sana unaweza futa maelfu ya picha ukafree mb 10 tu.

2.Vitu vya kwenye gallery vinaweza kuwa vimeseviwa kwenye memory card hivyo hapo unakuwa hujafree internal memory.

Chakufanya nenda setting then storage iache kwa mda iload then utaona allocation ya memory ipoje pengine kuna vitu usivyovijua ndio vinakula space.

Pia tafuta icon ya njano inaitwa my files ingia humo angalia folder la bluetooth, downloads, na mafolder mengine kama kuna vitu visivyo na maana vifute.
 
Back
Top Bottom