CHA The GREAT
JF-Expert Member
- Nov 11, 2010
- 651
- 854
Anaandika [HASHTAG]#luqman maloto[/HASHTAG]
Hali ya kisiasa iliyopo nchini, ikionekana kuwepo kwa chuki kati ya watawala na wapinzani, inaamsha macho ya tofauti na kuzungumza kizalendo kwa sababu uzalendo wa kweli ni kupenda nchi na watu wake.
Huwezi kujiita mzalendo wakati unamchukia raia mwenzako kwa sababu za kiitikadi, dini au kabila. Uzalendo wa kweli unaelekeza mapenzi na uvumilivu kwa wale ambao unatofautiana nao. Mpende mwenzio japo ni chama tofauti. Mwache ajivunie haki yake ya kikatiba ya kukupinga. Huo ndiyo uzalendo.
Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe, alipata kuandika kwenye ukurasa wake wa Facebook, wosia ambao alipewa na Waziri Mkuu wa zamani wa Malaysia, Mahathir Mohamad, walipokutana mwaka 2010.
Mahathir alimwambia Zitto: “Put your country at heart, don't destroy your country for political expediency or for fulfilling your ambition. Serve your country."
Kiswahili: Iweke nchi yako moyoni, usiiharibu nchi yako kwa ajili ya mtaji wa kisiasa au kwa kutaka kutimiza tu ndoto zako binafsi. Itumikie nchi yako.
Hekima za Mahathir kwa Zitto zinapaswa kupenya kwenye ubongo wa kila mwanasiasa, aliye madarakani au mpinzani, Tanzania, Kenya, Afrika yote na dunia kwa jumla. Kila mmoja aiweke nchi yake moyoni na ajiepushe na vitendo vyenye kuivuruga nchi kwa maslahi ya kisiasa.
Mzalendo wa kweli, anayeiweka nchi yake moyoni kabla ya kitu chochote, anapoingia kwenye siasa, hupaswa kutambua kuwa kuna nafasi yake kisiasa na nafasi za wapinzani wake. Kwa utambuzi huo hutakiwa kuwaheshimu na kuwavumilia anaopingana nao hata kama atakuwa anakerwa.
Muhimu zaidi ni kuwa mwanasiasa mzalendo anapoona kuna hali ya kisiasa inabeba sura ya kuhatarisha amani ya nchi au kuwagawa wananchi, hukimbilia kwenye mazungumzo, maana mtunza amani wa kweli huamini kwamba hakuna linaloweza kushindikana chini ya mazungumzo.
Mjumbe wa Amani wa Umoja wa Mataifa, Jane Goodall, raia wa Uingereza, amepata kusema: "Change happens by listening and then starting a dialogue with the people who are doing something you don't believe is right."
Kiswahili: Mabadiliko hutokea kwa kusikiliza kisha kuanzisha majadiliano na watu ambao wanafanya vitu ambavyo huamini kuwa ni sahihi.
Watu wakiwa wanapinga upande wa kushoto, wewe unang'ang'ania ya kwako ukiwa kulia, ni lini mtakutana kuweka mambo sawa? Na kukaa mezani haimaanishi uache mitazamo na itikadi zako ili ufuate za unaopingana nao, bali kujenga maelewano ya kuenenda kwa amani baada ya kukubaliana kutokukubaliana.
Ni kama Rais wa Israel, Reuven Rivlin alipopata kusema: "A multicultural society does not reject the culture of the other but is prepared to listen, to see, to dialogue and, in the final analysis, to possibly accept the other's culture without compromising its own."
Kiswahili: Jamii iliyostaarabika haikatai utamaduni wa mtu mwingine, bali huandaliwa kusikiliza, kuona, kujadili na katika mchanganuo wa mwisho kuwa na uwezekano wa kuukubali bila kuusaliti utamaduni wake.
Hicho alichokisema Rivlin ndicho ambacho kinatolewa muongozo kupitia falsafa ya kisiasa inayoitwa multiculturalism, kwa maana ya ustaarabu wa kijamii, watu na tofauti zao za kiitikadi na kisera, kuelewana, kushirikiana na kuheshimiana huku wakitofautiana.
USTAARABU NI UMOJA
Kwa nukuu ambazo nimezitumia na uchambuzi wenyewe wa maudhui hadi kufikia hapa, unabaini kuwa hakuna uzalendo katika jamii ambayo watu wake wamekosa ustaarabu. Na msingi unaoleta jamii iliyostaarabika ni mazungumzo.
Pale ambapo inaonekana kuna upungufu unajitokeza au makosa yanafanyika, kabla hali haijawa mbaya, watu wanakutana na kuzungumza. Hapo unazingatia maneno ya Goodall kuwa lazima kusikilizana baina ya pande mbili zisizoelewana ili mabadiliko yatokee.
Kumbe sasa mazungumzo na majadiliano yenye sura ya kupata amani ya kijamii au nchi ndiyo uzalendo wenyewe. Kupitia tafsiri hiyo ni kuwa wanasiasa wabishi, wasiotaka mwafaka, wenye kuamini katika siasa za jino kwa jino au nguvu za mamlaka, hao ndiyo siyo wazalendo.
Mmoja kati ya zawadi bora kuletwa duniani, Mahatma Gandhi alilionya suala la ubishi wa kutotaka mazungumzo, aliposema: "An eye for an eye will only make the whole world blind."
Kiswahili: Jicho kwa jicho litaifanya tu dunia yote iwe kipofu.
Tafsiri ya Gandhi ni kuwa lazima watu wajishushe na kuketi mezani kuzungumza kwa usalama wa dunia. Maana pana ni kwamba kila mmoja akijifanya anajua, mwisho hakuna atakayejua, dunia nzima itakuwa kipofu.
Inapotokea wanasiasa ndiyo ambao wanakuwa wagumu kuielekea meza ili kuzungumza na kupata mwafaka hata kama ni kutokukubaliana, hao wanakuwa wameingia kwenye fani ambayo si maji yao. Demokrasia ilianza kisha siasa na vyama vya siasa vilifuata miaka mingi baadaye kwa lengo la kuitetea demokrasia.
Ikiwa vyama vya siasa vipo kwa ajili ya kukuza demokrasia, uwepo wa wanasiasa wanaochukiana kwa sababu ya tofauti za itikadi na vyama ni matokeo ya watu ambao ama hawaijui au hawaimudu siasa. Vijana mtaani wangesema: "Disko limeingia Mmasai."
Siasa ni jukwaa la maisha ya watu sasa na miaka mingi ijayo. Wanasiasa kwa nafasi zao hupaswa kuielekea salama ya watu na kuikwepa hatari. Anapotokea mwanasiasa akawa hajali usalama, kwa hivyo akajielekeza kwenye mgawanyiko kwa ubishi au ujivuni, huyo ndiye Mmasai mwenyewe ndani ya disko.
Mwana mkakati wa Chama cha Democratic, Marekani, Peter Fenn ambaye ni mshauri na mchambuzi wa masuala ya siasa Marekani, alipata kusema: "A basic tenet of healthy democracy is open dialogue and transparency."
Kiswahili: Msingi wa imani kwa afya ya demokrasia ni majadiliano ya wazi na uwazi.
Hivyo ukiitaka siasa sharti uwe mpenda demokrasia na kufanikisha hilo unapaswa kukubali au kushawishi majadiliano, kinyume chake unakuwa umeingia kwenye fani ambayo siyo yako. Unakuwa unabebwa na msemo wa disko limeingia Mmasai.
Wanasiasa wa Tanzania wanatakiwa kuthibitisha kuwa wapo kwenye fani yao. Hivyo, tofauti za sasa wazitibu kwa majadiliano. Hakuna jambo gumu lisilozungumzika kama maslahi ya nchi yatatangulizwa mbele. Siasa ni jukwaa la kuombea uongozi, sio la kugawa watu na maisha yao.
Uwepo wa wanasiasa wenye kugawa watu badala ya kuwaunganisha, hapo maana yake watu ambao siyo wanasiasa wamevamia fani. Ndiyo kusema disko limeshaingia Mmasai.
Ndimi Luqman MALOTO