Tatizo la screen ya PC kushake na kuweka mstari

cleokippo

JF-Expert Member
Dec 21, 2014
2,117
1,794
Wana jamvi, naombeni msaada hasa kwa wale wataalau wa IT. Nina PC yangu aina ya Dell, sasa juzi kuna tatizo limejitokeza hata sielewi limesababishwa na nini. Yaani nikiiwasha ile PC screen inakuwa inashake muda wote, pia ikakata mstari kati kati ya kioo kwa kwenda juu. Sasa kwa anayejua sababu ni kitu fulani naomba anijulishe jamani ili hata nikiipeleka kwa fundi nijue tatizo ni kitu fulani.

Asanteni.
 
Pole mkuu, hapo huna screen tena, fanya mchakato wa kuchange screen tu. Hata yangu ilianzaga mdogo mdogo kuwa na tatizo kama hilo watu wakawa wananipa moyo ni mkanda ila kumbe screen.
 
Mara nyingi husababishwa na mikanda ya display, jaribu kubadilisha mikanda huenda imepiga shoti. Ukiona bado ipo hivyo basi effect ya mikanda imesambaa mpaka kwenye kioo, yaani kioo kinakuwa hakifai tena.
 
Yaani yangu juzi ndio nimetengeneza imekaa kama miezi saba hivi, tatizo ni kioo. Badili kioo tu Mkuu.
 
Je, PC ikiingiliwa maji kweney screen kuna namna yoyote ya kuweza kuyatoa au yatatoka yenyewe mdogo mdogo?
 
Dawa ni kufungua na kusafisha. Kadri muda unavyosonga ndivyo maji yanavyharibu PC yako.

Mkuu PC yangu kioo kimechora mstari kinaonyesha upande mmoja na kama kuna mistari mweusi kimechora, je tatizo ni kioo, je kinatengenezeka kwa gharama gani?
 
Back
Top Bottom