Tatizo la Rhesus Factor

NGOSWE.120

JF-Expert Member
Jul 9, 2011
218
250
Madaktari, Heshima kwenu.

Pamoja na kuwa na majukumu mengi lakini nawaomba msaada wenu katika hili.

Mimi mke wangu ni mjamzito na baada ya kwenda klinic na kufanyiwa baadhi ya vipimo imeonyesha kuwa yeye ana Blood Group A-, Yaani A - Negative. Wakati huo huo Mimi nina blood group O Positive.

Ameshauriwa kwamba inabidi achome sindano kabla na baada ya kujifungua ili kumnusuru mtoto kutopoteza uhai mara tu baada ya kuzaliwa.

TATIZO:

Ameambiwa kuwa SINDANO hiyo gharama zake ni Tsh. laki mbili na nusu, hivyo sindano 2 ( kabla na baada ya kujifungua ni Tsh. laki tano), na huduma hiyo haipatikani sehemu nyingine except hapo alipoenda, na Muhimbili tu. Na bima haitumiki katika huduma ya sindano hiyo.

USHAURI NINAOMBA:-

1. Ni sehemu gani nyingine naweza kwenda (hospital) nikapata huduma hiyo kwa kutumia Bima ya afya (NHIF)? Na hata kama bima ya Afya (NHIF) haitumiki, Pia, ni Hospital gani naweza pata huduma hiyo kwa bei nafuu na SIO hiyo laki mbili na nusu x 2 = 500,000/=?
2. Ni kweli mtoto anaweza kufariki masaa machache tu baada ya kuzaliwa endapo mama hatachoma hiyo sindano? au mtoto anaweza pata tatizo lolote baadae?


Samahani kwa thread ndefu....lakini naombeni Ushauri wenu hasa sehemu ninayoweza tatua hilo tatizo bila kutumia gharama kubwa.

ASANTENI SANA.
 

Kingmairo

JF-Expert Member
Apr 7, 2012
4,945
2,000
Pole mkuu kwa complication hiyo. Pamoja na kusubiria wataalam, unaweza kupita mwenyewe kwenye Hospitali ingine ukasikia wanasemaje.
 

bitimkongwe

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
3,095
2,000
Loh nimesahau somo langu la sekondari la biolojia miaka 42 iliyopita!

Lakini Rh+ na Rh- havikubaliani. Ila kama umeandikiwa hizo sindano kwa bei hiyo jaribu kufunga mkanda ili mtoto ataekuja aweze kusurvive.
 

jingojames

JF-Expert Member
Mar 12, 2010
887
500
Pole sana!
Hiyo dawa lazima ufunguke cash bima mimi kadi ya AAR muhimbili walinigomea ikabidi nikanunue hiyo dawa ,inaitwa ANTI D...
uwa anachomwa mama baada tu ya kujifungua na kabla hajaanza kumnyonyesha mtoto!
sina uhakika kama NHIF wanagharamia ,hila kama unatumia huduma za NHIF watembelee kwy ofisi zao wakupe ukweli wa mambo!
 

NGOSWE.120

JF-Expert Member
Jul 9, 2011
218
250
Sasa ina maana lazima mama achome sindano zote mbili before and after.....au ni moja tu?? @ Evelyn Salt, Double R...and others above!
 

NGOSWE.120

JF-Expert Member
Jul 9, 2011
218
250
Pole sana!
Hiyo dawa lazima ufunguke cash bima mimi kadi ya AAR muhimbili walinigomea ikabidi nikanunue hiyo dawa ,inaitwa ANTI D...
uwa anachomwa mama baada tu ya kujifungua na kabla hajaanza kumnyonyesha mtoto!
sina uhakika kama NHIF wanagharamia ,hila kama unatumia huduma za NHIF watembelee kwy ofisi zao wakupe ukweli wa mambo!

Asante mkuu kwa ushauri wako, kwa hiyo inawezekana ukanunua dawa na wao wakakuchoma tu si ndio mkuu au? Na je bei ya hiyo dawa ndio inafikia kiwango hicho cha laki mbili na nusu? Wewe je alichoma mara ngapi......mara moja tu au alichomwa sindano kabla na baada ya kujifungua? Natanguliza shukrani Mkuu kwa majibu.
 

double R

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
2,324
2,000
Mtoto hawezi kusurvive hadi sindano

Nadhani hii taarifa uliyonayo si sahihi.
Mama ndo huathirika na rho-D za mtoto alizorithi kwa baba ake. Chance ni kama sikosei mpaka 16%.
Mama anachomwa sindano kabla kuepuka madhara endapo itatokea muingiliano wa damu mtoto akiwa bado tumboni na wakati wa kujifungua. Asipochomwa hiyo sindano yaweza mdhuru yeye au asiweze kuzaa tena baadaye. Ila wapo watoto wanaorithi za mama.
 

double R

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
2,324
2,000
Asante mkuu kwa ushauri wako, kwa hiyo inawezekana ukanunua dawa na wao wakakuchoma tu si ndio mkuu au? Na je bei ya hiyo dawa ndio inafikia kiwango hicho cha laki mbili na nusu? Wewe je alichoma mara ngapi......mara moja tu au alichomwa sindano kabla na baada ya kujifungua? Natanguliza shukrani Mkuu kwa majibu.
Anachoma mara mbili. Ila inawezekana ikawa mtoto karithi kutokea kwake so wakishampima mtoto damu anaweza asihitaji tena.
 

malimingiii

JF-Expert Member
Nov 20, 2013
902
1,000
Nenda hospitali yenye bima na yenye hiyo sindano watakuchoma kwa kutumia bima mkuu. Mimi kuna mshkaji wangu mke wake alichomwa hiyo sindano kwa kutumia bima ya afya (NHIF)
 

tbl

Senior Member
Mar 29, 2011
115
195
Binafsi nilisikia inatakiwa chomwa ndani ya masaa 72 baada ya mama kujifungua, kuhusu bei nenda tu kaulize ofisi za NHIF
 

ISLETS

JF-Expert Member
Dec 29, 2012
8,153
2,000
yani ukikiosa kabisa alternatives na pesa huna basi gharamia upasuaji wakati wa kujigungua kuepusha kugusana kwa damu kwa bahati mbaya na pia mama asinyonyeshe huyo mtoto...sasa hapo hapo mtoto atakuwa kwenye risk nyingine.... muhimu ni apate hiyo sindano, nenda ofisi za NHIF waulize,
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom