Tatizo la msongamano mizani kuisha

Tatizo la msongamano mizani kuisha

Cochabamba

Member
Joined
Feb 4, 2014
Posts
76
Reaction score
98
Wizara ya Ujenzi kupitia Waziri wake Dkt.Magufuli wamekagua mzani wa Kisasa kabisa na wa kwanza ktk nchi hii pale Vigwaza Mkoani Pwani. Mzani huo unaruhusu magari kupima bila kusimama, kwa kimombo " Weigh-In-Motion (WIM)".

Utaratibu huu utaondoa kabisa ile dhana yiliyozoeleka ya msongamano wa malori pindi yapimapo uzito. Mzani huu ni mwendelezo wa mizani ya kisasa inayojengwa nchini kote.

Katika safari hiyo Waziri huyo alipita na kukagua barabara ya Kibamba - Kwembe - Makondeko yenye urefu wa kilomita 17. Barabara hii itatoa huduma katika Chuo Kikuu cha Muhimbili kinachojengwa Mloganzila, Kibamba Jijini Dar es Salaam.

Matukio katika Picha:


1.JPG 9.JPG f8a32b8b3bb18722115733e1bc61f6cf.jpg
Mzani mpya wa Vigwaza Mkoani Pwani ambao ni wa kwanza na wakisasa kabisa kujengwa nchini ambao unaruhusu magari kupima bila kusimama na kuondoa ile dhana ya msongamano wa malori ktk mizani.

c9df24e3ccc23b3027611f1f6fb4e354.jpg 2.JPG
Mhandisi Kileo kutoka Wakala wa Barabara akionyesha jinsi Mzani mpya wa Vigwaza utakavyokuwa ukipima magari yakiwa yanatembea " Weigh-In-Motion".

3.JPG
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe kushoto akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa Mzani huo.

4.JPG
Waziri wa Ujenzi akizungumza na wananchi kuhusu Mzani mpya unaopima magari wakati yakitembea Vigwaza mkoani Pwani.

Ukaguzi wa kazi za ujenzi inayofanyika katika Chuo Kikuu cha Muhimbili kilichopo katika eneo la Mloganzila Kibamba nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Waziri alipitia akikagua ujenzi wa barabara ya Kibamba kupitia kwembe hadi Makondeko inayojengwa kwa kiwango cha lami yenye urefu wa Kilometa 17. Aliweza pia kuzungumza na wakazi wa Kwembe.

10.JPG 3.JPG
Katika ziara hiyo aliambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe (Aliyevaa koti jeusi), picha ya kushoto akizungumza na Meneja wa Wakala wa Barabara mkoa wa Dar es salaam Mhandisi Julius Ndyamukama kuhusu ujenzi wa Barabara yakutoka Kibamba-Kwembe hadi Makondeko yenye urefu wa Kilomita 17

Nawasilisha!
 
Hakuna jipya hapo...hizo ni kodi wanazokusanya...magamba na kikwete ni majanga
 
Na vipi kuhusu zile documents ambazo gari ikipima inabidi isubiri kwa dakika kadhaa ili wapimaji waprint na kuziandika andika?
Nazo zitakuwa zikitolewa bila gari kusimama?

Maana zile documents nazo zinachangia sana foleni inabidi waboreshe na hilo ili mabadiliko yaonekane.
 
Nielimisheni, je gari likionekana uzito umezidi pia halisimami? Vituo hivi vijengwe nje ya barabara ili visizuie magari yasiyohotajika kupima uzito.
 
Kwaiyo ulitaka waje wamuombe mama yako hela yakujengea miundo mbinu ya taifa?..acha uchadema ata kwenye hakuna.finyu wee.
Magamba full mapovu mpaka mnaandika vitu vya ajabu sijui ndo lugha za mapepo ya mbio za mwenge. Check kwenye red.
 
Magamba full mapovu mpaka mnaandika vitu vya ajabu sijui ndo lugha za mapepo ya mbio za mwenge. Check kwenye red.

Nawasiwasi na uraia wako...inawezekana nikawa na pingana na mrundi.hapo dada sijatumia kirundi kwenye hizo red zako. Mijasho itokanayo na migwanda mnayovaa inakufanya usielewe ata lugha yako.pole sana dada.
 
siku hiyo barabara ikipanuliwa ikawa two lanes each side, je huo mzani utabomolewa tena!!!? kwa nini wasingeujenga mbali kidogo ili kuepusha gharama za kuhamisha hamisha wakati wa upanuzi wa hiyo barabara ambao tunasikia uko kwenye mipango ya fast lane to chalinze.
 
siku hiyo barabara ikipanuliwa ikawa two lanes each side, je huo mzani utabomolewa tena!!!? kwa nini wasingeujenga mbali kidogo ili kuepusha gharama za kuhamisha hamisha wakati wa upanuzi wa hiyo barabara ambao tunasikia uko kwenye mipango ya fast lane to chalinze.

Mzani upo mbali na barabara na ile expressway itajengwa tofauti kabisa ni hii iliyopo kwa kuwa mradi huo utakuwa wa ubia kati ya Serikali na makampuni binafsi yaani PPP na hivyo kutenga njia ya watakaoshindwa kulipia(hii iliyopo sasa) na watakaolipia ( itajengwa kwa kutumia ardhi nyingine kabisa lakini parallel na ya sasa)
 
Sijui kama ulinielewa nilichosema hapo juu?

Pole kama sijajibu vema, gari inapoingia ktk mzani itajulikana portfolio yake yote ktk data base so no paperwork labda kama imezidi itapark yard ya pembeni kabisa mwa barabara kwa hatua zingine. Objective ni kuondoa au kumaliza kabisa congestion ya malori ktk Mizani, haina tofauti na mizani ya kisasa ya WIM ya huko walikoendelea!
 
Pole kama sijajibu vema, gari inapoingia ktk mzani itajulikana portfolio yake yote ktk data base so no paperwork labda kama imezidi itapark yard ya pembeni kabisa mwa barabara kwa hatua zingine. Objective ni kuondoa au kumaliza kabisa congestion ya malori ktk Mizani, haina tofauti na mizani ya kisasa ya WIM ya huko walikoendelea!
Hapo Sasa umejibu vema.
Shukrani.
Mkuu wewe upo tanroads au wizara ya ujenzi?
 
Nchi hujengwa na wenye mioyo, Magufuli fanya kazi yako Mungu anaona unavyowasaidia watanzania wenzako.
 
Back
Top Bottom