Akizungumza baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mizani ya kisasa Vigwaza, mkoani Pwani, Dk Magufuli alisema Ruvu ina eneo kubwa linalotosha kujenga bandari kavu na pia kuna reli ya Tazara inayotoka bandarini, hivyo itakuwa ni jambo jema malori ya mizigo yakiwa yanaanzia safari katika eneo hilo na kuendelea mikoani na nchi za jirani"
Chalinze.
Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli ameshauri kuanzishwa kwa bandari kavu katika Mji wa Ruvu ili kupunguza foleni katika Jiji la Dar es Salaam na kuzuia malori kuingia katikati ya jiji.
Akizungumza baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mizani ya kisasa Vigwaza, mkoani Pwani, Dk Magufuli alisema Ruvu ina eneo kubwa linalotosha kujenga bandari kavu na pia kuna reli ya Tazara inayotoka bandarini, hivyo itakuwa ni jambo jema malori ya mizigo yakiwa yanaanzia safari katika eneo hilo na kuendelea mikoani na nchi za jirani.
"Kulikuwa hakuna sababu ya kuyapeleka malori makubwa mpaka bandarini yakatengeneze foleni Barabara ya Morogoro na Mandela wakati Ruvu ina maeneo makubwa ya kutosha na Reli ya Tazara inapita, hii ni changamoto ya kwetu sote na siyo wizara pekee," alisema Dk Magufuli.
Alisema suala la udhibiti wa foleni jijini Dar es Salaam linahusisha taasisi nyingi za serikali wakiwamo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Wizara za Uchukuzi na Ujenzi na Serikali za Mitaa kupitia sheria zake ndogondogo.
Iwapo wazo hilo litakubaliwa, Dk Magufuli alisema watafunga mizani ya Kibaha na kutumia ya Vigwaza.
Mizani ya kisasa ya Vigwaza ni ya kwanza nchini ambayo itakuwa iking'amua magari yaliyozidisha mizigo pekee ili yapimwe na kutozwa faini kwa uvunjifu wa sheria.
Akizungumzia mizani hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mhandisi Mussa Iyombe alisema imegharimu Sh11 bilioni na itasaidia kupunguza foleni za magari ambayo hupitia mizani bila ya kuwa na mizigo au kuzidisha uzito.
Chanzo:Mwananchi