Tatizo la mkojo kutoka kidogo au kuchelewa kutoka

Luoman

Member
Jul 2, 2020
20
44
Wakuu mimi ni kijana wa miaka 22 ndio nipo kidato cha sita mwaka huu, lakini nimekuwa na tatizo la kutoka kwa mkojo mdogo sana au kutoka kwa shida na ata ukitoka bado nahisi kama kuna mkojo umebaki kwenye kibofu lakini nikijaribu kuutoa wote haiwezekani tena.

Tatizo hilo limenitesa sio chini ya miaka 6 mpaka sasa, nilijaribu kwenda kituo cha afya kupima mkojo wakaniambia hawaoni tatizo
Je,kuna uwezekano wa tiba mbadala kwa huu ugonjwa?

Je, naweza kuathiri mpaka njia ya uzazi?

Ombi: kwa mtu mwenye uelewa kuhusu huu ugonjwa anifahamishe maana ninateseka sana
 
Tatizo ni wewe mwenyewe kwa KUSUSA kunywa maji. Rekebisha hiyo tabia haraka sana.

Nishawahi kunywa maji mengi sana nilijiwekea ratiba lazima kwa siku nimalize 1 litre lakini baada ya kuacha tatizo likarudi kama kawaida
 
Pole sana, Hapo njia yako ya haja ndogo imebana na ilianza kidogokidogo ndio maana imechukua miaka sita, mpaka siku utajikuta mkojo hautotoka kabisa, ni vizuri ukwahi hospigali kubwa wakupige x ray tatizo lipo kwenye njia na sio kibofu, then watakufanyia upasuaji wa kuongeza hiyo njia then utakaa sawa (ni vizuri kuwahi hospital mapema, ni tatizo hatari unaweza kupoteza maisha kama ikatokea umeshindwa kabisa kukojoa at lest siku moja na. Pia unaweza kukuletea matatizo kwenye viungo vingine figo n.k
 
Pole sana, Hapo njia yako ya haja ndogo imebana na ilianza kidogokidogo ndio maana imechukua miaka sita, mpaka siku utajikuta mkojo hautotoka kabisa, ni vizuri ukwahi hospigali kubwa wakupige x ray tatizo lipo kwenye njia na sio kibofu, then watakufanyia upasuaji wa kuongeza hiyo njia then utakaa sawa( ni vizuri kuwahi hospital mapema, ni tatizo hatari unaweza kupoteza maisha kama ikatokea umeshindwa kabisa kukojoa at lest siku moja na.. pia unaweza kukuletea matatizo kwenye viungo vingine figo n.k
Daah asante sana kwa ushauri mkuu ntaufanyia kazi muda sio mrefu
 
Kafanye uchunguzi wa Afya, ndugu. Hata tatizo la tezi dume, lina dalili kama hizo. Ila vipimo ndio vitatoa majibu.
 
Nishawahi kunywa maji mengi sana nilijiwekea ratiba lazima kwa siku nimalize 1 litre lakini baada ya kuacha tatizo likarudi kama kawaida
Tatizo lako kama langu ila Mimi ni mvivu wa kunywa maji ila saiz iyo hali imepotea sijui imepotea na maji bado situmii sana yan ilikuw kila nikikojoa nikimaliza tu napata maumivu siwez kukaa chini hadi upite mda flani bas nikawa nakaa na cephalexin nikion iyo hali nakunywa vidonge viwil baada ya dk chache inaacha.

Nilikuwa na mazoea ya kutokwenda kukojoa kwa wakati kwaiyo hii hali ilikuwa inatokea hasa nikiwekeleza mkojo ila nikikojoa kwa wakati ilikuwa haisumbui sana

Sent from my itel S31 using JamiiForums mobile app
 
Nishawahi kunywa maji mengi sana nilijiwekea ratiba lazima kwa siku nimalize 1 litre lakini baada ya kuacha tatizo likarudi kama kawaida
Lita moja tu kwa siku halafu unajisifu?,mie nakunywa lita 3,kunywa angalau lita 2 utaona mabadiliko
 
Lita 1 kwa siku haitoshi..unatakiwa kunywa at least lita 2 na kuendelea.Lakini tatizo lako difficult in passing urine au feeling of incomplete bladder emptying linaweza likasababishwa pia na kukiwa incomplete blokage in ur urinary sytem ambayo inasababishwa na vitu vingi..either narrowing of urine pathway katika sehemu flani (stricture) or a stone blocking the pathway.

Je, unasikia maumivu wakat wa kuanza au kumaliza kukojoa? je, unapata homa?je unasikia maumivu chini ya kitovu, or on the flanks or sehemu ya chini ya mgongo?Je mkojo unatoka rangi ya kawaida au unachanganyika na damu?Je frequency ya kwenda chooni kukojoa imeongezeka kupita kawaida au ipo sawa tu?

Je, una historia ya kuumwa Urinary tract infection mara kwa mara? (UTI), historia ya kuumwa kichocho? Au historia ya kuumwa magonjwa ya zinaa?au historia ya kupata ajali au kuumia iliyohusisha jeraha kweny flanks, sehemu ya chini ya kitovu na sehemu za siri?

Nikushauri uende hospitali kubwa uchek mkojo( urine analysis) lakini pia ufanye imaging ya mfumo wa mfumo wa mkojo.
Ukikutana na urologist itakuw vyema zaidi.

Get well soon
 
Nishawahi kunywa maji mengi sana nilijiwekea ratiba lazima kwa siku nimalize 1 litre lakini baada ya kuacha tatizo likarudi kama kawaida
We jamaa 1litre ndo unasema maji mengi? Nadhani average ni lita tatu Hadi nne na nusu kwa siku.

Sent
 
Tatizo lako kama langu ila Mimi ni mvivu wa kunywa maji ila saiz iyo hali imepotea sijui imepotea na maji bado situmii sana yan ilikuw kila nikikojoa nikimaliza tu napata maumivu siwez kukaa chini hadi upite mda flani bas nikawa nakaa na cephalexin nikion iyo hali nakunywa vidonge viwil baada ya dk chache inaacha.nilikuwa na mazoea ya kutokwenda kukojoa kwa wakati kwaiyo hii hali ilikuwa inatokea hasa nikiwekeleza mkojo ila nikikojoa kwa wakati ilikuwa haisumbui sana

Sent from my itel S31 using JamiiForums mobile app

mkuu hapa kwenye cephalexin ulkua unajiumiza tu mwili wako kwa iyo dawa
 
Luoman, Inawezekana una urethral stricture, stones au bph (tezi dume imevimba nb:sio kansa) kwaio kikubwa uende hospital ukaeleze vizuri ufanyiwe vipimo kuthibisha kati ya hayo then utibiwe
 
Sijawahi kupata magonjwa ya zinaa,UTI au kichocho ila wakati unaanza nilikuwa naenda aja ndogo mara kwa mara lakini kwa sasa imepungua sana naweza nikakojoa mara moja au mara mbili kwa siku
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom