Tatizo la mimba kwa wanafunzi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,005
9,872
Kwa muda mrefu tumekuwa na hili tatizo la mimba kwa wanafunzi, wa shule za msingi na sekondari. Naiona nia ya taifa katika namna za kutaka kutokomeza tatizo hili, lakini suluhu tunazotumia tunaendelea kutengeneza matatizo mengine. Kufukuzana shule au kutiana jela, kitu kinachozidisha umasikini wa nchi yetu.

Harakati za Haki Elimu na wanaharakati wa kielimu wapo katika wanadeal na matokeo kuliko chanzo cha tatizo.


CHANZO NI NINI?

Aisee! Wazazi na walimu wapo kimya kwenye kufundishana na watoto juu ya elimu ya ujinsia.

Ikumbukwe wakati husika, miili ya watoto inakuwa imeshawaka kibaiolojia, hivyo ni vigumu kuzuia wao kufanya ngono hata kama utaweka uzio wa umeme au kuwatishia kufungwa jela maisha.

Hatuna sababu ya kupinga utu, au maumbile. Bali kuangalia namna ya kupunguza risks. Ni vyema basi elimu ya ujinsia na kujilinda na mimba za utotoni kutiliwa mkazo kwa kiasi kikubwa.

Mahusiano na mapenzi hayatokoma eti kwa kuwa mtu yuko shuleni, mtu kuwa shule haimaanishi kuwa baleghe itamsubiri. Ni vyema kuwaguide watoto ili wasiweze kwenda kufanya mapenzi ambayo yatawaharibia future yao yanayotokana na ngono zembe nk.

Tunavyozidi kuipinga ngono kwa watu ambao tayari wamebaleghe, tunakuwa kama tunajaribu kuzipa jua kwa ungo. Elimu juu ya matumizi ya condoms, na njia nyingine za uzazi zifundishwe.

Ieleweke kuwa kumfanya mtoto asifanye ngono yako madhara mengi kisaikolojia, tuache uwongo wa kuwaambia vijana wasubiri hadi watakapooa, wakati mtu anabaleghe akiwa na miaka 15 na anatarajia kuoa akiwa na miaka 30. Ni uwongo kwa mtu alie vizuri kiafya kukaa miaka 15 bila kufanya ngono.

Ni vyema basi tuangalie upya ili tusiwape mzigo wasioweza kuubeba watoto wetu, tutawafukuza shule, tutawafukuza nyumbani, LAKINI CHANZO NI KUTAKA VISIVYOWEZEKANA.
 
Back
Top Bottom