Tatizo la mawe kwenye figo (kidney stones)

CTX

JF-Expert Member
Jan 3, 2015
1,273
984
Figo ni kiungo muhimu katikamwili wa binadamu, hufanya kazi ya kuchuja damu huku ikiondoa sumu zote za mwili ,figo hufanya kazi ya kurekebisha kiasi cha maji mwilini (electrolyte level) kabla damu haijapita katika figo, huwa imebeba maji na taka taka nyingi sana (urea) ,lakini inapopita katika figo huchujwa na vitu muhimu hurudishwa katika mzunguko wa damu lakini.

Masalia mengine ambayo hayafai tena katika mwili ikiwani pamoja na kiwango cha maji kilichozidi hupitishwa kwenye mirija miwili (ureters)kuelekea kwenye kibofu ( urinary bladder) nakisha kutolewa nje ya mwili kupitia njia ya mkojo (urethra) mkusanyiko wa kemikali hizi (chemical crystals), wakati mwingine hugandamana na kutengeneza chembechembe ya vitu kama mchanga.

,kadri siku zinavyozidi kuendelea ndivyo vinavyozidi kukua hadiwengine hufikia hatua ya kuziba njia ya mkojo katika figo yenyewe (neprone) au kwenye mirija yakupeleka mkojo kutoka kwenye figo kwenda kwenye kibofu (ureteter), hapo ndipo mtu anaanza kupata shida ya kukojoa na kusikia maumivu makali.

DALILI ZA UWEPO WA MAWE KWENYE FIGO;
Mtu mwenye mawe kwenye figo huonyesha dalili zifuatazo;
a.Maumivu ya mgongo na kiuno
b.Mkojo kutoka ukiwa na rangi ya damu
c.Kutokwa na jasho wakati wa usiku
d.Kupatwa na homa kali kwa wakati flani ikiambatana na kutetemeka mwili
e.Kuhisikichefuchefu na kutapika
f.Mkojo kuwa na harufu kali
g.Maumivu makali sehemu za mbavu
h.Miguu kujaa maji/kuvimba.
i.Maumivu ya tumbo chini ya kitovu upande wa kushoto au kulia kutegemea ni figo ya upande gani iliyoathirika.
j.Maumivu makali unapogusa upande wa figo iliyoathirika.

KISABABISHI CHA MAWE KATIKA FIGO (KIDNEY STONES);
1.Matumizi ya baadhi ya dawa husababisha mtu kupata mawe katika figo pindi anapozitumia kila mara.
2.Utumiaji wa vyakula vyenye kuongeza vitamin A na D, ambavyo huongeza kwa kiasi kikubwa madini joto mwilini
3.Kuishi kwenye mazingira ya joto sana bila kupata maji ya kutosha husababisha kiasi cha chemical kuongezeka katika figo na kusababisha zigandamane na kutengenezamawe ndani ya figo.
4.Maambukizi ya magonjwa ya figo kama renal tubulaacidocisctc, huongeza hatari ya kupata tatizo hilo.
5.Kurithi kutoka kwawazazi (wanakuwa na homoni ziitwazo antiduretic hormone)zisizoweza kufanya kazi yakuchuja damu kikamilifu na mwishowe hutengeneza mawekatika figo.
6.Utumiaji wa vyakula vyenye protini kwa wingi zinazotokana na wanyama na chumvi nyingi (huongeza hatari ya kupata tatizo hili)
7.Unene kupita kiasi

JINSI YA KUGUNDUA TATIZO;
1.Mgonjwa kufanyiwa X-Ray au scan
2.Vipimo vya damu (blood test)
3.Vipimo vya mkojo (urenarlulisis)
Tiba za tatizo hili la figo huwa ni gharama sana kiasi kwamba watu wengi wanshindwa kuzimudu.
Dawa zilizotengenezwa na mimea na zenye ubora mkubwa basi zina uwezo wa kutibu tatizo hili vizuri endapo utaliwahi mapema.
Baadhi ya dawa hizi ni:

a. TONIFYING
b.KODICEPS
Dawa hizi mbali na kutibu matatizo ya mawe katika figo zinauwezo wa;
1. kutibu saratani ya kizazi stage ya kwanza ,kusafisha mirija ya uzazi na kutoa maji katika mirija hiyo
2.Uvimbe ndani ya mwili
3.Kurekebisha hedhi iliyovurugika kwa akina mama (hasa waliowahi kutumia dawa za uzazi wa mpango)
4.Saratani ya ini na kibofu cha mkojo
5.Kusafisha mfumo mzima wa njia ya mkojo
6.Huwasaidia akina mama wenye kasoro mbalimbali katika via vyauzazi.
 
Asante mkuuu.


Zaman nikiwa mtoto nilikua najiuliza ,kidney stones inasababishwa nann???

**Basi nikawa ANAJUA inasababishwa nakula chakula chenye mawe mawe na michanga**...nachoshukuru Shauku ya kutaka kujua imenifanya niwe hivi nilivyo maana saizi nasaga mawe ya dhahabu apa Geita!!
 
Kisababishi no 1 hapo juu ni aina gani za dawa zikitumiwa zinasababisha mawe kwenye figo
mkuu tufafanulie zaidi
pia tuchukue hatua zipi kujikinga na maradhi haya
 
Kisababishi no 1 hapo juu ni aina gani za dawa zikitumiwa zinasababisha mawe kwenye figo
mkuu tufafanulie zaidi
pia tuchukue hatua zipi kujikinga na maradhi haya

Matumizi ya baadhi ya dawa husababisha mtu kupata mawe katika figo pindi anapozitumia kila mara.Dawa hizo ni kama vile za kutibu kansa na HIV,antibiotic kama ciprofloxacin,cefrtriaxone na madawa yenye sulphur kama metacalphin nk.

Hatua za kuchukua ili kujilinda na tatizo la mawe kwenye figo ni pamoja na;
-kunywa maji ya kutosha
-usile sana vyakula vyenye chumvi nyingi
 
Back
Top Bottom