1800
JF-Expert Member
- Dec 27, 2010
- 2,215
- 603
Leo ni siku ya kumi hakuna maji Morogoro,maeneo kama ya Kola,Bigwa,Nane nane nk ni makame kabisa na hakuna hata tone la maji,mamlaka husika (MOROWASA) imekaa kimya haitoi sababu yeyote wala haikutoa tahadhari yoyote kabla,mnatudondoshea ma bill tu na kukimbilia kuja kukata mabomba wakati huduma hamtoi na zinazidi kuzorota kadri ya siku ziendavyo!maji yakitoka ni machafu,yanakuja na mchanga na mizizi kama vile tumekwenda kuchota mtoni na si maji yanayokua treated na mamlaka husika!tunaomba kujuzwa ubabaishaji huu kwenye kila idara muhimu za serikali utakoma lini?tunahitaji maji Morogoro,sio blah blah!