Tatizo la maji mashuleni

Blue Bahari

JF-Expert Member
Aug 21, 2016
1,223
1,117
NI MUDA MUAFAKA SASA SERIKALI IHAKIKISHE KILA SHULE INAKUWA NA KISIMA CHAKE.

Wakuu habari!

Nikiwa kama mdau mmojawapo wa masuala ya kielimu, nalazimika kuleta mawazo yangu hapa jukwaani ili tupeane uzoefu wa namna sahihi ya kutatua tatizo la maji mashuleni..

Katika Shule nyingi za serikali, hususani Shule za vijijini, zinakabiliwa na uhaba mkubwa wa maji ya kutumia (kama vile kunywa na kupikia). Sote tunatambua maji ni mojawapo ya huduma ya msingi Kwa binadamu yoyote yule.

Kuna shule moja hapa nilipo kijijini nimeshuhudia wanafunzi wakinywa maji ya kidimbwi kilichopo karibu na shule husika. Kidimbwi hicho hukusanya maji ya mvua kutoka katika njia za maji yanayotiririka kutoka barabarani pindi mvua inaponyesha. Sasa, baada ya kuwauliza Kwa nini mnakunywa maji hayo ambayo yametulia kwa siku nne tangu yakusanyike (baada ya mvua kunyesha), wanafunzi walinijibu kwamba “wanakiu sana na hawana pesa za kununulia maji ya dukani”. Niliwauliza kwa nini wasiwe wanabeba katika chupa kutoka nyumbani kwao, wakanijibu “nyumbani maji hayatoshi kila Mwanafunzi kubeba maji kwenye chupa”.

Nilijitahidi kuwazuia wasinywe maji hayo, Kwa kuwa ni machafu, wao wakalalamika Kwamba “watakufa na kiu cha maji; hivyo, niwaache wanywe hivyo hivyo hata kama ni machafu”. Nilihuzunika sana kuona watoto wale waking’ang’ania kunywa maji machafu sababu niliiona hatari ya wanafunzi hao kuugua magonjwa ya tumbo kama vile kuharisha, typhoid au ukawa mwanzo wa mlipuko wa kipindupindu. Lakini hata ukifanikiwa kuwafukuza wasinywe maji hayo, wao hurudi tena kuyanywa wakishajua umeondoka.

MAONI: NINI KIFANYIKE?

Ni muda muafaka sasa serikali ikaja na mipango mikakati ambayo itahakikisha kila shule, kuanzia msingi hadi secondary, kunakuwa na kisima cha maji ili kuwasaidia wanafunzi (na shule yote kiujumla) ktk matumizi yao. kama ambavyo serikali ya Magufuli (Mwaka 2020) ilidhamilia kutenga bajeti ya Tshs 2 billion (taarifa ipo hapa BILIONI 2 ZATENGWA KWA AJILI YA MAJI MASHULENI) lakini sidhani Pesa hizo zingeweza/zinaweza kutosheleza Shule zote za sekondai na msingi hapa Tanzania; hususani ukizingatia Pesa hizo zilitengwa kusambaza maji mashuleni na katika vituo vya afya.. Kama ambavyo serikali imefanikiwa kuhakikisha kila shule imeunganishwa na Umeme wa TANESCO , ni matumaini yangu pia suala la upatikanaji wa maji shuleni linawezekana bila shida yoyote ile aidha Kwa uchimbaji wa visima vya maji au kuvuta kutoka idara za maji. Hili litafanikiwa endapo bajeti ya maji mashuleni itaongezwa mara dufu kwa kuwa Shule ni nyingi sana.

FAIDA ZAKE:

1. Wanafunzi wataokolewa kutoka katika hatari za kuugua magonjwa yatokanayo na matumizi ya maji machafu (water borne diseases). Zaidi soma hapa MAJI SAFI NA SALAMA CHANGAMOTO KWA WATOTO WENGI MASHULENI.

2. Itasaidia kutuliza akili za wanafunzi kwa kuwa hawatakuwa wakiwaza tena mahangaiko ya kupata maji Kwa ajili ya matumizi yao.

3. Program za shule ktk kufanikisha kuwapa chakula wanafunzi hazitakuwa ni za kusuasua sababu kutakuwa na uhakika wa upatikanaji wa maji. Shule nyingi sasa hivi, hususani za serikali za kata, zinapambana ili kuhakikisha wanafunzi wawe wanakula shuleni chakula cha mchana.

4. Kuongezeka Kwa kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi na shule kiujumla. Sababu kubwa ni Kwa kuwa wanafunzi watakuwa wakisoma ktk akili ya utulivu pasipo kuwaza maji Kwa ajili ya matumizi yao (ikiwemo kupikia).

Hayo ndiyo maelezo na maoni yangu mujarabu; ni matumaini yangu nimeeleweka ipasavyo huku nikiamini pia vigogo wa serikali nao wakipita humu kuchungulia mawazo yetu mbali mbali tunayotoa.

Asante!
 
Uzi wako unakaribia kumaliza mwaka bila kuwa nawachangiaji. Umeongea suala la msingi lakini jamii hawakuelewi.
1. Hatujali sana mambo ya kujikinga mpaka janga litokee.
2. Hatujali sana uhai wa watu wengine
3. Kama ni visima kila shule inauwezo wa kuchimba kisima chake kama wakiamua ila ni suala la no.2 bila kutegemea serikali.
4. Wananchi tunaitegemea serikali na serikali inatutegemea sisi ni tatizo.
5. Ungeanza wewe kuchangisha hizo pesa na jamii ijue ungefanya jambo la msingi sana.
MWISHO NI KWAMBA UKIWEKA HAYA MAMBO MATANO PAMOJA UTAPATA JIBU, KWA NINI SISI WEUSI TUTABAKI KUWA WEUSI NA MWEUPE ATABAKI KUWA MWEUPE. TUENDELEA KUOMBA KWA MOLA ILI TUJUE MATESO YA MWINGINE NI YAKO PIA.AMINA
 
Back
Top Bottom