Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Meya wa Kinondoni Boniface Jacob amesaini mkataba wenye thamani ya TSH Bil. 1.6 kwa lengo la kutengeneza madawati 12, 097, Meza 6552 na viti 6552.
Makundi ya wadau wa Manispaa yaani watu binafsi, Wafanyabiashara, Makampuni , Taasisi, na Mashirika ya ndani na nje yameombwa kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali kuu na Halmashauri kumaliza changamoto zote za elimu nchini kwa kuweka mazingira mazuri ya kutoa elimu bure katika shule za msingi na sekondari ili elimu inayotolewa iwe bora katika shule hizo.Hayo yamesemwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mh Boniface Jacob katika hafla ya kusaini mikataba ya kutengeneza madawati katika shule za msingi na Sekondari za Manispaa ya Kinondoni yenye thamani ya Bilioni 1.6 itakayowezesha kutengeneza madawati 12,091 kwa shule za msingi na viti 6,552 na meza 6,552 kwa shule za Sekondari.
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imeamua kutoa zabuni kwa wakandarasi 9 ili kuwezesha kazi hiyo kukamilika kwa wakati na kwa ubora utakaolingana na thamani ya fedha itakayotumika (Value for Money)
Makampuni yaliyopewa zabuni na kiasi cha madawati, viti na meza wanayotakiwa kutengeneza na thamani yake ni pamoja na:-
• MSIKALE GENERAL BUILDERS AND RENOVATION (Madawati 500, Meza 500, Viti 500 kwa Tsh 87,500,000/=)
• MTWEVE WORKSHOP (Madawati 1,000, Viti 500, Meza 500 kwa Tsh 132,500,000/=)
• HIGHLAND TRADERS & GENERAL SERVICES (Madawati 500, Meza 500, Viti 500 kwa 87,500,000/=)
• MAI HARDWARE SUPPLIES (Madawati 500, Meza 500, Viti 500 kwa Tsh 87,500,000/=)
• EDOSAMA HARDWARE LTD (Madawati 5,091, Viti 2,052, Meza 2,052 kwa Tsh 662,610,000/=)
• UNIPRO SOLUTIONS LTD (Madawati 2,000/=, Viti 500, Meza 500 kwa Tsh 222,500,000/=)
• BWANZA INVESTMENT COMPANY (Madawati 500, Viti 500, Meza 500 kwa Tsh 87,500,000/=)
• BENEMA ENTERPRISES COMPANY LTD (Madawati 500, Viti 500, Meza 500 kwa Tsh 87,500,000/=)
• MAZONGERA FURNITURE & DECORATION SUPPLY (Madawati 1,500, Viti 1,000, Meza 1,000 kwa Tsh 220,000,000/=)
Mh Boniface Jacob amewahakikishia wananchi wote wa Kinondoni kuwa Manispaa iataendelea kushirikiana na wadau wengine kutatua kero mbalimbali katika sekta ya elimu na sekta nyingine ili kufikia malengo ya kutoa huduma bora kwa wakazi wake kama ilivyokusudiwa na kwa mipango iliyojiwekea.