Tatizo la kuwashwa chuchu

katika kukuwasha zinaambatana na kuongezeka ukumbwa kidogo yaani kama kuvimba kiasi? kingine ni baada ya muda gani au ukikaribia siku zako?
kama ni hivyo ni mabadiliko ya homoni ila kama zimekuanza sasa hivi
kwanza labda una mimba kama ulikutana na mwanaume
kama hujawahi kuzaa na huna mimba nakushauri nenda kafanye uchunguzi wa afya yako Kansa ya matiti ni ugonjwa unaowatesa wengi kwa sasa jali afya yako
 
Inawezekana ni madhara ya kuvaa blazia/ sidiria za mitumba
Kweli STUNTER,achunguze material ya blazia zake,anaweza akafanya majaribio kwa siku za weekend akaacha kabisa kuvaa blazia kwa siku hizo mbili nakuona tatizo kama limepungua au vipi,vitu vingine ni body spray, perfumes pamoja na lotion anazotumia zinawezakumsababishia,asitishe kimoja baada ya kingine kuuangalia ni kipi kinaweza kuwa ni sababu ya tatizo.Kama shida ikieendelea nenda hospital watakupa ushauri na matibabu kwa usahihi.Dawa za kuzuia miwasho zipo ni nyingi tu,mfano.Hydrocortisone cream 1%,Bethamethasone cream 0.065% au 0.1%.Ila fanya udadisi wa kugundua ni nini hasa sababu na ukishindwa kupata nafuu nenda hospital usitumie dawa bila kuonana na wataalamu wa afya.
 
Habari wanaJF,

Msaada jamani, Mimi ni binti wa miaka 20. Mara nyingi sana chuchu huwa zinaniwasha. Je tatizo hili linasababishwa na nini?

Natanguliza shukrani
Kachunguze material ya blazia zako,unaweza kufanya majaribio kwa siku za weekend ukaacha kabisa kuvaa blazia kwa siku hizo mbili nakuona tatizo kama limepungua au vipi,vitu vingine ni body spray, perfumes pamoja na lotion unazotumia zinaweza kukusababishia,usitishe kimoja baada ya kingine kuangalia ni kipi kinaweza kuwa ni sababu ya tatizo.Kama shida ikieendelea nenda hospital watakupa ushauri na matibabu kwa usahihi.Dawa za kuzuia miwasho zipo ni nyingi tu,mfano.Hydrocortisone cream 1%,Bethamethasone cream 0.065% au 0.1%.Ila fanya udadisi wa kugundua ni nini hasa sababu na ukishindwa kupata nafuu nenda hospital,usitumie dawa bila kuonana na wataalamu wa afya.
 
Hata mm huwa nawashwa Alf sanasana nikikaribia kuingia p
Nawewe nenda hosp uwezijua labda ni tatizo ambalo linakuwa siku adi siku jiulize nawenzio wakikalibia siku zao inakuwa ivo kama jibu ni hapana bhasi wahi hosp usichukulie easy
 
Pole sana mdogo wangu ningekuwa karibu yako ninge kusaidia ila kwa vile niko mbali chukua bra inayobana uyabane hata ukiwa unalala... utapata nafuu na baadae kupona kabisa..
Pole sana.. hamna haja hata yakunitumia picha nazijua na najua unavyokerekwa na hio situations..

Meza panadol uyalalie hio pia itasaidia
 
Habari wanaJF,

Msaada jamani, Mimi ni binti wa miaka 20. Mara nyingi sana chuchu huwa zinaniwasha. Je tatizo hili linasababishwa na nini?

Natanguliza shukrani
Kumbe hata JF kuna binti wa miaka 20! Ni nilidhani humu wamo wa-bibi tu.
 
Back
Top Bottom