Tatizo la kutokwa na uchafu ukeni- Pata ufafanuzi wa kina, ushauri na tiba ya tatizo hili

gunah,
A5853191-24E4-404F-A454-3DC96A5A6D9B.jpeg
 
Hili tatizo la kutokwa na uchafu unaotoa harufu mbaya sehemu za siri. Kitaalamu hali ya mwanamke kutokwa na majimaji (vaginal fluids) yenye rangi nyeupe au ya njano, ni hali ya kawaida na wala siyo tatizo endapo majimaji hayo siyo mazito sana na wala hayatoi harufu mbaya.

Lakini endapo majimaji yanayotoka yapo katika hali ya ute mzito wenye rangi nyeupe au kahawia, yanatoa harufu kali na yanawasha, basi hiyo ni ishara ya ugonjwa uitwao Vaginosis.

Majimaji au ute unaoteleza kutoka sehemu za siri ni njia inayowezesha viungo vya uzazi vya mwanamke kujisafisha na kuutoa uchafu wa seli zilizokufa na mabaki ya damu ya hedhi nje ya mwili.

Pia huvikinga viungo vya uzazi dhidi ya maambukizi ya bakteria au fangasi wanaosababisha magonjwa. Kwa kawaida huwa hayatoi harufu na huwa na rangi nyeupe au ya njano. Pia huwa na asidi ya Lactic ambayo huzuia kuzaliana kwa vijidudu vya maradhi na huzalishwa kwenye tezi za Bartholin (Bartholin’s glands) zilizopo kwenye shingo ya mlango wa uzazi (Cervix).

Kwa kawaida, mwanamke hutoa kiasi cha gramu 2 za seli zilizokufa kutoka kwenye mji wa uzazi na gramu 3 za ute mwepesi kila siku.

Kiwango hiki huweza kuongezeka au kupungua kutegemeana na mzunguko wa hedhi. Kuna wakati ute huwa mwepesi na unaovutika (kama ute wa yai la kuku) na kuna wakati huwa mzito kiasi na wenye rangi ya njano. Ute huu ni wa kawaida na huwatoka wanawake wote hususan baada ya kuvunja ungo.

Sababu za kutokwa na uchafu wenye harufu mbaya sehemu za siri
Kuna sababu nyingi ambazo husababisha mwanamke kutoa ute au majimaji yasiyo ya kawaida kutoka kwenye sehemu zake za siri.

- Maambukizi ya bakteria wanaosababisha
magonjwa kama Trichomoniasis, Candidiasis, Gonorrhea
Candida albicans, chlamydia
Hayo yote huweza kusababisha mwanamke kutokwa na uchafu unaoambatana na harufu mbaya.

- Pia mabaki ya vitambaa, tishu au pedi ambazo hazikutolewa wakati wa hedhi huweza kusababisha tatizo hili.

- Usafi wa sehemu za siri usipozingatiwa hususanimwanamke anapokuwa kwenye siku zake za hedhi, huweza kuwa mazalia mazuri ya bakteria wanaosababisha harufu mbaya.

Dalili za ugonjwa wa kutokwa na uchafu ukeni (VAGINOSIS)

Mwanamke mwenye tatizo la Vaginosis huwa na dalili kubwa ya kutokwa na ute na majimaji yasiyo ya kawaida (uchafu) kutoka sehemu za siri.

1. Uchafu huu huwa unatoa harufu kali kama shombo ya samaki au kitu kilichooza na huambatana na maumivu makali ya tumbo chini ya kitovu.

2. Wakati mwingine uchafu wenye rangi kama ya kijani hutoka.

3. Kuwashwa na kuchomachoma sehemu za siri, mgonjwa asipopatiwa tiba haraka husababisha vidonda sehemu za siri.

4. Mwanamke anapoona anatokwa na ute uliochanganyikana na damu hata kama hayupo kwenye siku zake, hii ni dalili nyingine ya Vaginosis.

5. Maumivu makali wakati wa tendo pia ni dalili za ugonjwa huu.

MATIBABU
Tatizo hili hutibika hospitalini baada ya vipimo vya kitaalamu kuchukuliwa na daktari mwenye uzoefu wa kutosha juu ya magonjwa ya wanawake.

Dawa za kupaka (Ointment/ Cream) na dawa za kumeza (Pills) huweza kutumika kutubu tatuzo hili.

Kumbuka: Ni makosa kutumia dawa bila kupata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa daktari.
Pia inatakiwa ufike katika kituo chochote cha afya pindi unapohisi unatatizo ili kufanyiwa vipimo na kupatiwa matibabu stahiki kulingana na tatizo litakalokuwa linakusumbua

Mema Announcement22.png


Karibu tujifunze na
Dr Sylvester John
Tel. No. 0753 518513
Email: johnsylvester022@gmail.com
 
Follow this link to join my WhatsApp group: MWANAMKE NA AFYA BORA🔥💃💃🔥

Ewe mwanamke karibu sana kujua yafuatayo
#afya yako ya mwili
#kujua magonjwa kiundani
#kujua kinga
#kujua tiba

NB:NI KWA AJILI YA MWANAMKE TUU

*PILI*/KUHUSIANA NA AFYA TUU

SHARE
*Ukimwelimisha Mwanamke ni kuieliamisha jamii*
🤝🤝🤝🤝🤝🤝
 
Kuna dem nimekutana nae siku zake za hatari lakin leo siku anatokwa na damu kidogo imechanganyikana na uchafu jeh tatizo nini kwake.

Ameblid tareh 19 mwez uliopita mpaka 21 ...
Nimesex nae siku yake ya 12 ambayo ni tarehe 30 mwezi uliopita... tukaendelea

Tukapiga show siku yake ya 14 na 16 ambayo ni jana...

Lakini jana ameshinda anakojoa tu pia kuna vdamu ametokwa mpaka leo asubui.

Damu inayotoka ni sio kali ni vidogo dogo na uchafu kama rangi ya shahawa.

Nikaamua nije kuomba ushauri humu jf wadau minisaidie mawazo

Pia analalamika akiinama anahisi kibofu kinajibana .

Ushauri wenu wadau

Pia mwez uliopita alitumia dawa ya clomitab.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom