Tatizo la kupata Hedhi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tatizo la kupata Hedhi

Discussion in 'JF Doctor' started by Dena Amsi, Mar 19, 2011.

 1. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #1
  Mar 19, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 160
  Naomba msaada maana mie nimeshindwa.

  Msichana wangu wa kazi ameanza kupata siku zake toka mwaka 2008 na alikuwa hana shida yoyote mpaka juzi mwezi wa kwanza ameanza kuumwa sana na tumbo last month ndo kazidiwa kabisa hata kazi hakuwa akifanya sasa jana kaanza tena yuko hoi tumbo linauma mno ila blood inatoka kama kawaida tu si nyingi si kidogo.

  Wataalamu hebu nisaidieni shida ni nini??
   
 2. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #2
  Mar 19, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  hata ukisema unasumbuliwa wewe mwenyewe hakuna tatizo mwone Dr. au wahi Loliondo tu
   
 3. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #3
  Mar 19, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Nadhani ni kawaida...imewahi kunitokea!Anywe maji kwa wingi ya uvugu vugu kama anaweza na kukanda ile sehemu ya chini ya tumbo kwa chupa au kitambaa chenye maji ya moto inasaidia!Dawa za maumivu kama panadol na asprini...na wakati anakaribia kuanza siku zake apunguze vitu vyenye sukari kama soda and the likes!Pia awe anakunywa maji yaliyochemsha na tangawizi mara kwa mara!
   
 4. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #4
  Mar 19, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 160
  We we Fidel yaani umenikosea heshima kabisa yaani mimi nianze kupata hedhi 2008 kweli umenichoka haaa.

  Mie hedhi yenyewe ishakoma siipati tena unichanganye na watoto?? KWA KWELI LEO UMENIKWAZA SANA.
   
 5. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #5
  Mar 19, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 160
  Ubarikiwe ila za maumivu nampatia tena zile za kina mama wanita buscopan (sijui spelling zake vizuri) zinampatia nafuu kidogo tu muda tena maumivu mda wa siku tano si mchezo.

  Asante kwa ushauri Lizzy
   
 6. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #6
  Mar 19, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  LInaweza likawa tatizo la kawaida ambalo linaweza kwisha lenyewe baada ya muda. Lakini inawezekana pia wakati alipokuwa akipata siku zake, kulikuwa na kiasi kidogo cha damu (uchafu) kilikuwa kinabaki na hivyo kutengeneza donge kidogo kidogo ambalo baada ya muda linakuwa kubwa na kuanza kuleta matatizo kama hayo. Ni vema ukawaona wataalamu wamchunguze ili kupata uhakika
   
 7. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #7
  Mar 19, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Tatizo la ss weusi kuficha ficha mambo

  Weka wazi tu mwenzenu nasumbiliwa na tatizo hili nifanyaje

  Hapo ndipo tunakaa tunapiga Tusker zetu huku tukikusaidia kwa ushauri hata kukuitia Dr. papo hapo.
   
 8. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #8
  Mar 19, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Hilo tatizo linawapata watu wengi wenye umri wake ingawa severity inatofautiana, kitaalamu wanaita dysmenorrhoea, kwa umri wake na jinsi inavyotokea itakuwa spasmodic dysmenorrhoea, wengine maumivu yanakuwa makali mpaka anashindwa kufanya kazi. Sababu za hayo maumivu ni nyingi lakini nyingi ya hizo husababisha mwili kuzalisha vichocheo vinavyoitwa prostaglandins kwa wingi kuliko kawaida kwa watu wenye dysmenorrhoea, hizo prostaglandins husababisha spasmodic myometrial contractions (misuli ya uterus inakakamaa - inacontract - sijui kama ni tafsiri sahihi) ambayo ndio husababisha maumivu, yaani mtu anakuwa na maumivu kama ya uchungu wa kuzaa vile.

  Matibabu yake ni kumpa dawa ambazo zinapunguza uzalishwaji wa hizo prostaglandins, hizo dawa zinajulikana kama non-steroidal antiinflamatory drugs (NSAIDS) zikijumuisha asprin, ibuprofen, mefenamic acid, indomethacin nk. Ibuprofen na mefenamic acid ni nzuri zaidi, ukimchanganyia na paracetamol, ataendelea na kazi zake kama kawaida. Hizi dawa atumie tu kwa muda akiwa kwenye hedhi akimaliza anaacha anasubiri mzunguko mwingine kama atapata maumivu tena. (Akitumia hizi dawa asipopata nafuu niPM nitakurudishia gharama zako, ingawa wewe hunilipi kwa ushauri wangu huu ninaokupa, ninajua zitamsaidia)

  Maumivu yakiendelea anaweza akatumia combined oral contraceptive pills, natumaini hana mpango wa kuzaa kwa sasa, hizi nazo zimethibitishwa kufanya kazi vizuri, hupunguza maumivu ya hedhi, hupunguza kiasi cha damu kinachotoka na vile vile hupunguza duration ya menses.

  Wengine pia wanaadvocate kutanua njia ya kizazi (cervical dilatation), hii inasaidia kwa wale ambao shida ni cervical stenosis (njia ya shingo ya kizazi kuwa nyembamba sana kwa hiyo hedhi inabidi itoke kwa kulazimishwa na huleta maumivu, lakini huyu wa kwako kwa sababu hedhi inatoka ya kutosha nadhani hana stenosis.

  Wengi shida hii inakwisha wanapozaa, wengine huendelea nayo lakini severity ya maumivu hupungua.

  Kuna watu wazima wengine pia huwa wanapata maumivu wakati wa hedhi, lakini hii ni aina nyinge ya dysmenorrhea, hii chanzo huwa ni tatizo kwenye kizazi, yaweza kuwa uvimbe, endometriosis (sijui kiswahili chake lakini hapa mtu anakuwa na vinyama vya ndani ya kizazi vimeota sehemu nyingine ya mwili kwa hiyo wakati wa hedhi vinamletea maumivu ya ajabu), au shida nyingine yoyote na dawa yake ni kutibu hicho chanzo.
   
 9. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #9
  Mar 19, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,590
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Kama ni binti wa kazi huenda ni janja ya kujipa likizo! Mara nyingi maumivu hupungua with time, sio kuomgezeka!
   
 10. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #10
  Mar 19, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 160
  Tatizo la kuanza pombe mapema huku unataka uwe na huku JF. Kila la heri
   
 11. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #11
  Mar 19, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 160
  Nashukuru tatizo likiendelea nita ku PM kama ulivyonishauri. Asante sana
   
 12. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #12
  Mar 19, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  inawezekana pia kaHG ketu kanahitaji mwenza . labda ukaanzishie sredi ya kutafuta kule MMU. (NB: nina master ya saikolojia)
   
 13. nnunu

  nnunu JF-Expert Member

  #13
  Mar 19, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 656
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  MPE POLE HUYO DADA WA NYUMBANI ,,naamini mkifuata ushauri wa DR KAPOTOLO tatizo linaweza kwisha ila ukiona hapati nafuu ni vizuri pia ukimpeleka hosp akafanyiwe check kabisa,,,,,
   
 14. Sware

  Sware Member

  #14
  Mar 19, 2011
  Joined: Dec 12, 2010
  Messages: 92
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Jamani mpe pole sana na uhakika utapa tu ushauri humu ndani!!
   
 15. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #15
  Mar 19, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 160
  Asante nimepata tayari
   
 16. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #16
  Mar 19, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 160
  Huu ushauri kiboko bado mdogo sana bana
   
 17. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #17
  Mar 19, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 160
  Kapotolo kweli kanisaidia sana namshukuru
   
Loading...