Tatizo la kupata choo kigumu au kukosa choo kwa muda mrefu (Constipation). Fahamu chanzo na tiba yake

Wewe unaweza kuwa na intestinal obstruction maana week 4 ni nyingi sana...ingekuwa ni constipation ya kawaida isingefika siku zote hizo..

Sababu ya intestinal obstruction inaweza kuwa una load kubwa ya minyoo kama ascaris n.k
Kwahip fanya uende hosptali waone kama tatizo ni obstruction au nini...
 
Tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu ni jambo tunalolikwepa kwenye mazungumzo yetu ya kila siku. Hata hivyo ni tatizo kubwa katika jamii na mbaya zaidi wengi hawajuwi madhara yake ni nini ya kuendelea kulivumilia tatizo hili.

Kupata choo kigumu au kufunga choo ni ishara ya tatizo lingine baya zaidi mwilini. Kama kuna jambo unapaswa uliepuke kwa nguvu zote basi ni hili. Kwa afya bora kabisa hakikisha unapata choo kila siku mara 2 hata mara 3.

Choo kilaini siyo kigumu na chenye maumivu. Wakati mwingine utakapopata tatizo hili naomba usiwe na aibu kulisema wazi hata kwa boss wako ili upate matibabu kwa haraka. Kufunga choo au kupata choo kigumu ndiyo CHANZO KIKUU CHA UGONJWA WA BAWASIRI kwa waTanzania wengi na hii inachangiwa kwa sehemu kubwa kwa kula ugali wa sembe na kutokunywa maji mengi kila siku. Pamoja na hayo, hakuna ugonjwa rahisi kutibika kama huu ikiwa utaamua kushughulisha kichwa chako kidogo hasa kwa kuangalia unakula na kunywa nini kila siku.

Dawa mbadala 10 zinazotibu kufunga choo au choo kigumu:

1. Mafuta ya Zeituni Mafuta ya zeituni (olive oil) yanatosha kutibu hili tatizo.
Yana radha nzuri mdomoni na ni dawa pia. Kama unaweza yafanye pia kama mafuta yako ya kupikia vyakula vyako mbalimbali, mafuta haya huweza kuliwa pia bila kupitishwa kwenye moto na hivyo ni mafuta mazuri kuweka kwenye kachumbari au saladi mbalimabali.

Matumizi: Chukua kijiko kikubwa kimoja cha mafuta ya zeituni changanya na kijiko kidogo kimoja cha chai cha maji maji ya limau na unywe asubuhi ukiamka tu tumbo likiwa bado tupu. Fanya hivi kila siku mpaka utakapopona.

2. Juisi ya Limau
Juisi ya limau inatumika kutibu tatizo la kupata choo kigumu au kufunga choo.
Chukua maji maji ya limau kutoka katika limau kubwa 3 na uchanganye na juisi ya matunda kupata kikombe kimoja (ml 250) na unywe yote kutwa mara 1 kila siku kwa siku kadhaa mpaka umepona. Ukiacha hilo la kutibu kufunga choo limau ina vitamini C nyingi na hivyo itakuongezea kinga yako ya mwili kwa haraka zaidi (usizidishe hata hivyo).

3. Mazoezi ya kutembea
Kama unataka kupata choo kilaini na cha kawaida basi jitahidi uwe mtu wa kutembeatembea na si kukaa tu kwenye kiti kutwa nzima. Maisha yetu ya kisasa na kazi za ofisini zinatulazimisha kuwa watu wa kukaa kwenye kiti masaa mengi wengine huamua tu kukaa kwenye kiti sebureni akiangalia TV asubuhi mpaka jioni!.

Aina hii ya maisha ni hatari zaidi kwa afya zetu kuliko hata madawa ya kulevya. Jitahidi kila siku uwe unapata muda wa kutembeatembea kwa miguu mpaka dakika 60 au zaidi. Hii itakusaidia kuondoa tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu sana.

4. Vyakula vya nyuzinyuzi (fiber)
Mara nyingi utasikia watu wakisisitiza juu ya umhimu wa kula vyakula vya asili na vyenye nyuzinyuzi. Chakula cha asili kina nafasi kubwa katika kuimarisha afya yako kwa ujumla. Kinachonishangaza ni kuona watu bado wanaendelea kula ugali wa sembe ilihali inajulikana wazi ugali mweupe ndiyo chanzo kikuu cha kupata choo kigumu ikiwemo ugonjwa wa bawasiri.

Ninakusihi sana uanze kula ugali wa dona kuanzia sasa na kuendelea. Hakikisha pia asilimia 80 ya mlo wako kwa siku ni matunda na mboga za majani. Matunda kama ndizi na parachichi ni mhimu ule kila siku kadharika tumia unga au mbegu za maboga.

5. Mshubiri (Aloe Vera)
Mshubiri unajulikana wazi kwa kutibu tatizo hili la kufunga choo au kupata choo kigumu. Ni mhimu utumie mshubiri fresh kabisa kutoka kwenye mmea moja kwa moja kuliko kutumia za dukani au za kwenye makopo. Usitumie zaidi ya vijiko vikubwa viwili vya jeli ya shubiri kwa siku.

Matumizi: Changanya vijiko vikubwa viwili vya jeli ya aloe vera ndani ya kikombe kimoja cha juisi ya matunda uliyotengeneza mwenyewe nyumbani (hasa juisi ya parachichi) na unywe yote kutwa mara 1 hasa nyakati za usiku unapokaribia kwenda kulala kwa siku kadhaa au mpaka umepona.

6. Baking soda Baking soda ni dawa nyingine ya asili nzuri kwa tatizo hili. Inafanya kazi vizuri kwa zaidi ya asilimia 95. Sababu ya bicarbonate iliyomo ndani yake itakusaidia kupumua nje vizuri gesi au hewa yoyote ilisongamana ndani ya tumbo pia inasaidia kupunguza asidi mwilini. Baking soda ni ile wamama huitumia katika kupika maandazi au mikate inapatikana katika maduka ya kawaida hata hapo nje kwa Mangi ipo.

Matumizi: -Changanya kijiko kidogo kimoja cha chai cha baking soda ndani ya nusu kikombe cha maji ya uvuguvugu (ml 125) na unywe yote kwa haraka kutwa mara 1 kwa siku 7 hivi au unaweza kuacha siku yoyote kabla kama tatizo litakuwa limeisha.

7. Mtindi
Unahitaji bakteria wazuri zaidi wakati huu unapokabiliwa na tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu. Utahitaji pia kuacha kula vyakula vya kwenye makopo (processed sugars and foods). Namna rahisi kabisa ya kuhakikisha mwili wako unapata bakteria wazuri ni kwa kutumia mtindi. Tumia mtindi wowote ule uliotengeneza mwenyewe nyumbani au hata wa dukani (ila wa dukani usiwe umeongezwa vitu vingine ndani yake – sweetened yogurt).

Matumizi: Kunywa kikombe kimoja (robo lita) cha mtindi wakati wa chakula cha asubuhi na kikombe kingine usiku unapoenda kulala kwa wiki 1 hata 2.

8. Fanya mazoezi ya kusimama na kuchuchumaa (squat)
Fanya mazoezi ya kuchuchumaaa na kusimama (squatting). Hili ni zoezi mhimu kwa mtu anayesumbuliwa na tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu sana. Fanya kuchuchumaa na kusimama mara 25 na upumzike dakika 1 kisha unaendelea tena unachuchumaa na kusimaa hivyo hivyo mara 25 kwa mizunguko mitano (5 rounds) huku ukipumzika dakika 1 kila baada ya mzunguko mmoja.

Fanya zoezi hili kila siku mara 1 na usizidishe sana, ni mara 25 kwa mizunguko mitano inatosha na uzuri ni kuwa unaweza kufanya zoezi hili mahali popote. Wakati huo huo unashauriwa kutumia choo cha kuchuchumaa yaani vile vyoo vya zamani na siyo hivi vya kisasa vya kukaa kama vile upo ofisini. Vyoo hivi vya kukaa ndiyo moja ya vitu vinavyochangia upate pia ugonjwa wa bawasiri (kuota kinyama sehemu ya haja kubwa na kupata maumivu wakati unajisaidia).

9. Matunda
Asilimia 80 ya chakula chacko kwa siku iwe ni matunda na mboga za majani. Unapoumwa na hili tatizo pendelea zaidi parachichi, papai na juisi ya ukwaju. Kula matunda siyo mpaka uumwe au ushauriwe na daktari, fanya kuwa ndiyo tabia yako kila siku na hutakawia kuona mabadiliko makubwa kwa afya yako kwa ujumla.

10. Maji ya Kunywa Maji ni uhai.
Asilimia 75 ya mwili wako ni maji. Asilimia 85 za ubongo wako ni maji. Asilimia 94 ya damu yako ni maji. Hakuna maisha bila maji. Inashangaza sana kuona mtu anamaliza siku nzima au hata siku 2 hajanywa maji! Kama wewe si mpenzi wa kunywa maji ya kutosha kila siku SAHAU KUWA NA AFYA NZURI MAISHANI MWAKO.

Hakikisha unakunywa maji kila siku lita 2 mpaka 3, kidogo kidogo kutwa nzima bila kusubiri kiu na hutaugua tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu. Dawa nyingine nzuri kwa ajili hii ni unga wa mbegu za mlonge
 
Mi nshakunywa kichupa cha dawa lakini wapi. Nikachange matibabu, naweka maji kwenye kopo, naweka sabuni inaweka povu, naweka mafuta ya nazi, nachukua syringe najiwekea huku hivi, dakika tano nyingi tatizo linaisha.
 
Mi nshakunywa kichupa cha dawa lakini wapi.
.Nikachange matibabu, naweka maji kwenye kopo, naweka sabuni inaweka povu, naweka mafuta ya nazi, nachukua syringe najiwekea huku hivi, dakika tano nyingi tatizo linaisha.


Wait... Una maanisha hiyo sindano yenye mapovu unajiingizia kwenye puru?
 
Sijaona juice ya ukwaju kwenye list yako ambayo ndio tiba inayotambulika na wataalamu wengi kwa kutibu constipation. Pia tafuna big g almaarufu kama jojo kila baada ya kumaliza kula.

Mate unayomeza yanasaidia kulainisha chakula na kufanya mmeng'enyo wa chakala kuwa rahisi. Kula dona, usipendelee kula wali ni chanzo cha tatizo. Pia kula matunda kwa wingi na maji kama alivyoshauri mleta uzi hapo juu!
 
nina tatizo la kupata choo mara chache naweza pitiliza siku mbili hata tatu bila kupata choo, ila chakula nakula kama kawaida....Je? nisaidieni sijui tatizo nn? na nilitatueje?
Tumia kirutubisho hiki kinaitwa C24/7 kina virutubisho 22,000 kinasaidia kurahisisha mmengenyo wa chakula hivyo utapata choo kila siku kwa maelezo zaidi kuhusu C24/7 Karibu +255625606806
 
Aisee..! I know someone who has almost given up on finding a cure for this problem.. will fwd these details to her
 
Mi nshakunywa kichupa cha dawa lakini wapi. Nikachange matibabu, naweka maji kwenye kopo, naweka sabuni inaweka povu, naweka mafuta ya nazi, nachukua syringe najiwekea huku hivi, dakika tano nyingi tatizo linaisha.
OMO inavyo unguza mikono, huko si itachinja kabisa?
 
Mzizimkavu,

Mimi huwa nina tatizo moja. Naweza kuamka asubuhi naenda mbwewe nasikia harufu mbaya balaa.

Je hii husababishwa na nini na dawa yake?
Hii inamanisha una mgandamano wa taka nyingi kwenye utumbo mpana ambao umeoza sasa.
Nami nilikuwa na tatizo hilo mpaka mpale nilipoambiwa bidhaa moja inaitwa *Splina Liquid Chlorophyll* mpaka Leo Niko poa.

Mwenye naomba hii atakusaidia +255743171395 jielezee kwake.
 
Mzizimkavu,

Mimi huwa nina tatizo moja. Naweza kuamka asubuhi naenda mbwewe nasikia harufu mbaya balaa.

Je hii husababishwa na nini na dawa yake?
Hii inamanisha una mgandamano wa taka nyingi kwenye utumbo mpana ambao umeoza sasa.
Nami nilikuwa na tatizo hilo mpaka mpale nilipoambiwa bidhaa moja inaitwa *Splina Liquid Chlorophyll* mpaka Leo Niko poa.

Mwenye naomba hii atakusaidia +255743171395 jielezee kwake.
 
Dawa ya kukosa choo ni kula PAPAI kula papai zima au nusu daily tatizo kwa heri.

Constipation = coronary cancer,blood and kidney diseases such as diabetes nakadhalika kuleni mapapai tena yale ya kienyeji sio haya ya kisasa...kama unakula milo angalau mitatu kwa uchache unafaa kukata gogo si chini ya mara 2 kwa siku.
Papai hoiyee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
UKOSEFU wa choo ni tatizo sugu miongoni mwa watu wengi. Bila kujua kuwa ni tatizo ambalo linahitaji tiba ya haraka, watu wengi hupuuzia na kuona siyo tatizo kubwa na ni hali ya kawaida.

Ukosefu wa choo wa muda mrefu, huwa ndiyo chanzo cha magonjwa mengine hatari.

Mtu anapokosa choo kikubwa kwa siku kadhaa, uchafu hujikusanya tumboni na unapokosa sehemu ya kutokea hukimbilia kwenye damu na kuingia kwenye mfumo mzima wa damu.

Uchafu huo unapoingia kwenye mfumo wa damu huwa sumu na chanzo cha maradhi mengine ambayo hujitokeza baadae na kuanza kumuathiri mtu, bila kujua chanzo chake.

Kwa kawaida mtu unapaswa kupata choo cha uhakika japo mara moja kwa siku, kutegemeana na mlo wake wa kila siku, unapokosa choo kwa siku nzima ili hali una kula milo yote kwa siku, elewa una tatizo katika mfumo wako wa kusaga chakula hivyo unapaswa kuchukua hatua haraka.

MTU MWENYE TATIZO HILI ANA DALILI GANI?

Mtu mwenye tatizo la ukosefu wa choo huwa na dalili kadhaa, ikiwemo kutumia nguvu na muda mwingi wakati wa kujisadia haja kubwa.

Pili ulimi wake huwa na utandu mweupe na hutoa harufu mbaya mdomoni. Mtu huyu pia hukosa hamu ya chakula na wakati wote tumbo huwa limejaa.

NINI HUSABABISHA TATIZO?

Tatizo la ukosefu wa choo husababishwa zaidi na ulaji mbaya wa vyakula, kuacha kula matunda na mboga na staili mbaya ya maisha ikiwa ni pamoja na kutokunywa maji ya kutosha kwa siku.

NINI KIFANYIKE?

Ili kuondoa tatizo kabla halijawa sugu, fanya moja miongoni mwa haya yafuatayo:

Kunywa maji ya uvuguvugu asubuhi mapema, kisha tembea tembea, baada ya muda utasikia haja ya kwenda Choo. Ili usifanye haraka na upate muda wa kutosha kujiandaa kwenda kazini, amka mapema zaidi.

Kula kiasi cha kutosha cha salad ya mboga mboga na juisi ya matunda halisi asubuhi kabla ya kula chochote.

Kila siku kabla ya kwenda kulala, kunywa maji ya uvugu yaliyochanganywa na kijiko kimoja cha asali. Kunywa maji ya uvugu yaliyochanganywa na limau asubuhi na mapema kabla hujala kitu chochote. Kunywa ‘castor Oil' muda mfupi kabla ya kwenda kulala.

Ili kujiepusha kabisa na tatizo la ukosefu wa choo, jenga mazoea ya kunywa maji mengi, kula mboga na matunda kwa wingi kila siku na kuacha kabisa ulaji wa vyakula vilivyoondolewa virutubisho kama vile mikate myeupe, ugali wa unga mweupe, keki vyakula vyenye sukari nyingi na vyakula vingine vitamu.

Je likishakua sugu je? ufanyeje
 
UKIWA NA SHIDA HII INABIDI KUANZA NA SUPLEMENT ZA MATUNZA KAMA COMPLETE PHYTO ENERGIZER AU C24/7. PPIA ZINAKUKINGA NA MAGNJWA KAMA CANCER YA UTUMBO N.K KWA MAWASILIANO ZAIDI NICHEKI WHATSAPP +255620495989
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom