Tatizo la kuona kwa mjamzito

matwin

Senior Member
Jan 7, 2016
124
134
Habari zenu.

Naomba kupatiwa ufafanuzi mimi ni mjamzito sasa kwa muda si mrefu saana nona vitu vinapita kwenye macho kama mistari isiyo na shepu ( eye floaters) nimeenda kwa gyno zaidi ya mara nne anasema ni kawaida kwa sababu vipimo vyote vipo sawa... presha ipo sawa.

Damu ipo sawa. Sukari ipo sawa. Uzito upo sawa.. maralia hakuna.. kila kitu kiko vizuri maji nakunywa mengi tu... sasa nashindwa kuizoea hii hali...

Nimejaribu kusoma napo wanasema ni normal.... naombeni mnisaidie kwa mawazo yenu yatanisaidia nianzie wapi tena.. au waliokutana na hali hii walifanyaje...asanten
 
Acha kulala Chali au wakati wa kuamka usiamke chali!

Ukilala lala upande, ukitaka kunyanyuka Kama umelala Basi nyanyuka kiupande upande, Hali hiyo si nzuri na inaweza kuleta athari kwa Mtoto Kama itaendelea kwa Muda mrefu, Ina uhusiano wa karibu na Pressure!

Tumia Muda Mwingi kupumzika na kuepuka Matumizi ya ku chosha ubongo hasa Matumizi ya simu
 
Asantee
 
Mkuu pamoja na kuwa huna pressure angalia sana chumvi kuwa makini siyo kitu kizuri wala sio kawaida kama unavyoweza kudhani.. Kila la heri
 
Back
Top Bottom