Tatizo la kukaa na kinyongo

Galacha Maestro

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2011
Posts
1,353
Reaction score
2,231
TATIZO LA KUKAA NA KINYONGO

Mjadala huu

Ni kwamba unakosa nafasi ya kufuatilia mambo mengine muhimu kwako.Unaweza kujiaminisha kwamba kinyongo ulichomwekea mtu unastahili kabisa.
Alininyanyasa sana nilipokuwa mdogo...

Alinitesa sana katika mapenzi/ndoa....

Alinisababishia hasara kubwa kwenye biashara yangu...

Alisababisha kifo cha mtu muhimu sana kwangu...

Na sababu nyingine nyingi unazojipa kwamba kuweka kinyongo kwa mtu ni haki yako kabisa.

Lakini hebu niambie, kwa kuwa na kinyongo hiko kumekusaidia nini mpaka sasa?

Je, alichokufanyia mtu huyo kipindi hiko kimebadilika?

SAMEHE?
Kukaa na kinyongo ni kuendelea kujitesa, kujinyima nafasi ya kufanya mambo ya msingi kwako na yatakayokupeleka kwenye mafanikio.Na kinyongo hiko hakikusaidii wewe wala yule ambaye umemwekea.
 
Mkuu post zako ni nzuri sana,Hongera.
 
Kukaa na kinyongo ni sawa na kunywa sumu ya panya alafu utegemee mtu mwingine afe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…