Tatizo la Gonjwa la Sukari (Diabets Mellitis): Fahamu chanzo, aina na ushauri wa tiba ya tatizo hili

JamiiForums

JF Official Account
Nov 9, 2006
6,202
5,014

Kumekuwepo kilio na maswali mengi ya wadau mbalimbali wakitaka kujua masuala kadhaa kuhusu ugonjwa wa kisukari; tumetengeneza mnakasha huu ili kurahisisha majibu (si yote) kwa wenye uhitaji wa maswali yao.

Zingatia: Ni vema kwenda hospitali kwa tiba ya uhakika, hapa utapata majibu yanayokupa mwanga wa nini cha kufanya.

Case studies, mapendekezo ya tiba, waliopata kutibiwa, madaktari wanaopendekezwa na wadau kwa tiba n.k ndivyo vitawekwa kwenye bandiko la kwanza
===
UFAFANUZI WA KINA KUHUSU UGONJWA HUU
Kisukari ni nini? Kisukari ni ugonjwa unaosababisha glukosi kuzidi kwenye damu (damusuziada) kwa sababu ya ukosefu wa insulini au kongosho kutoa insulini isiyotosheleza mahitaji ya mwili.

Kuna aina ngapi za ugonjwa wa kisukari?
Kuna aina tatu za ugonjwa wa kisukari:

Aina ya kwanza ya kisukari:
Ugonjwa wa kisukari unaosababishwa na kongosho kushindwa kutoa insulini kabisa. Katika ugonjwa kisukari wa aina hii mgonjwa lazima achome sindano ya insulini kila siku kwa sababu kongosho haitoi insulini kabisa.

Aina ya pili ya kisukari:
Ugonjwa wa kisukari unaosababishwa na kongosho kutoa insulini isiyotosheleza mahitaji ya mwili. Aina hii ya kisukari inaweza kutibiwa kwa kutumia vidonge au kwa kupunguza tu kiasi cha sukari kwenye chakula ua kiasi cha chakula chote unachokula.

Kisukari cha ujauzito: Kuna baadhi ya wamama ambao sukari kwenye damu zao hupanda wakati wa uja uzito na huteremka mara wanapojifungua. Baadhi ya wamama hao sukari inaweza isiteremke tena hata baada ya kujifungua na wakabakia wagonjwa kisukari moja kwa moja hasa kama ni wanene kupitiliza na baada ya kujifungua mimba nyingi. ·

Nini tofauti ya aina ya kwanza na ile ya pili ya kisukari?




Dalili


Aina ya kwanza


Aina ya pili
Umri wa kuanza ugonjwa Miaka chini ya 40. Miaka zaidi ya 50.
Muda wa dalili za ugonjwa kabla hajagundulika kuwa na kisukari. Wiki Miezi hadi miaka.
Uzito wa mgonjwa wakati anagulika kisukari Wa kawaida au pungufu Mnene.
Ketoni kwenye mkojo Zipo Hazipo.
Kifo cha haraka hasipotumia insulini. Ndiyo. Hapana.
Matokeotata ya kisukari wakati anagulika kisukari Hakuna. Yapo.
Mtu mwingine mwenye ugonjwa wa kisukari katika familia. Kwa kawaida hayupo Yupo.

Je, Ugonjwa huu unasababishwa na kula sukari nyingi?
La hasha. Kula sukari nyingi sio sababu ya ugonjwa kisukari. Lakini lazima tuseme kwamba kula sukari nyingi si nzuri kwa afya yako kwani utaongeza uzito na kuweza kuathiri uwezo wa mwili wako kujikinga na maradhi tofauti. Hivyo sukari tutumie lakini kwa uangalifu.

Kitu gani husababisha ugonjwa wa kisukari?
- Magonjwa ya ini.
- Unene kupita kiasi.
- Msongo wa mawazo.
- Kurithi kutoka kwa wazazi.
- Kuvuta sigara wakati wa ujauzito.
- Kutumia nyama ilivyofukizwa moshi.
- Kuondolewa kongosho kwa upelesheni.
- Kuharibika kongosho kwa ajali au moto.
- Magonjwa ya kongosho mfano uvimbe kwenye kongosho unaosababishwa na pombe au virusi (mfano: Rubella, mumps, HIV
- Dawa: § Phenytoin. § Thiazide mfano bendrofluazide. § Steroidi mfano prednisolone, dexamethasone n.k.
- Utapia mlo wa mtoto kabla hajazaliwa (intrauterine malnutrition).
- Utumiaji wa maziwa ya ngombe kwa mtoto kabla ya umri wa miezi 3.
- Magonjwa ya yanayotengeneza antibodizi zinazoshambulia mwili (autoimmune disease).

Nini dalili za kisukari na damusuziada?
- Kukonda.
- Kutoona vizuri.
- Kuumwa na kichwa.
- Kuchoka bila ya kufanya kazi.
- Kula sana kwa sababu ya kusikia njaa sana.
- Kunywa maji sana kwa sababu ya kujisikia kiu mara kwa mara.
- Kusikia ganzi, kuchomwachomwa au maumivu kwenye mikono na miguu.
- Kujisaidia haja ndogo mara kwa mara, Mgonjwa hujisaidia zaidi ya mara tatu usiku.

Utafahamuje kama ugonjwa wa kisukari umeutawala vizuri?
Kama huna dalili zozote na unajisikia vizuri. Huamki usiku kujisaidia haja ndogo zaidi ya mara moja. Kama unapima glukozi kwenye damu na unakuta hakuna damusuziada (hyperglycaemia). Glukozi kwenye damu ni sawa ikiwa kati ya miligramu 80-144 kwa kila desilita ya damu (kati ya milimoli 4-8 kwa kila lita ya damu).

Kwa nini uhangaike kuutawala ugonjwa wako wa kisukari?
Utakuwa huna dalili zozote. Utaishi maisha marefu zaidi. Kwa hiyo utaweza kuishi maisha karibu ya kawaida. Mwili utakuwa na nguvu zaidi za kupigana na maambukizo. Utazuia matokeotata (complications) mengi yanyoweza kusababishwa na ugonjwa wa kisukari.

Je, ugonjwa wangu wa kisukari unaweza kupona?
Kwa ujumla, ukishapata ugonjwa wa kisukari utakuwa nao maisha. Lakini hakuna sababu kwa nini usiweze kuishi maisha ya kawaida na mazuri.

Kwa dawa za hospitali mpaka sasa hakuna dawa ya kuondoa moja kwa moja ingawa hasa kwa aina ya 2 watu baada ya kurekebisha vyakula wanaweza kujiweka katika hali hali ambayo mwili unaweza kutumia insulin yake kidogo bila ya kula vidonge au sindano.

Kuna utafiti wa kufanya transplant ili kuongeza insulin mwilini kwa kutumia sehemu (pancreas) ya mtu mwengine lakini bado haujafanikiwa kuweza kutumika kama ni matibabu.

Je, watoto wangu wanaweza kuurithi?
Wakati mwingine zaidi ya mtoto mmoja katika familia wanaweza kuwa na ugonjwa huo. Lakini urithi wa ugonjwa huu kwa watoto ni mdogo sana kwa kawaida. Kwa hiyo usiwe na wasiwasi.

Je, nikiwa na ugonjwa wa kisukari ninaweza kuoa au kuolea na kuwa na watoto?
Ndiyo. Ugonjwa huu haumzuii mtu kuoa au kuolewa.

Je, ni zipi athari za ugonjwa huu?
Baada ya muda mrefu ugonjwa wa sukari huleta athari ya mishipa ya fahamu na kusababisha kupoteza hisia za ngozi na viganja au nyayo na kupungua nuru ya macho. Pia athari ya mafigo huweza kujitokeza na uzungukaji wa damu unaweza kupungua katika baadhi ya sehemu na kusababisha kufa kwa sehemu za mwili.

Kujitokeza kwa dalili hizi kunategemea ni kiasi gani matibabu yamefanikiwa na wakati wa kuanza kwa matibabu hayo baada ya kujuilikana kwamba mtu ana ugonjwa huu.

Je, ugonjwa wa kisukari ni ugonjwa wa kuambukiza kama vile kifua kikuu au ukoma? Hapana. Huwezi kuambukizwa ugonjwa wa kisukari.

Vipi naweza kujikinga na ugonjwa huu?
Ikiwa unayo historia katika familia sio lazima kwamba utapata ugonjwa huu. Lakini kwa wale ambao wanaweza kuupata wanaweza kuuchelewesha kwa kujitahidi kuishi maisha ya afya nzuri kwa kula chakula bora, mazoezi, kula mboga mboga kwa wingi na kujiepusha na uzito wa mwili. Pia kupima damu baada ya kila muda ikiwa una historia katika ukoo au una wasi wasi kutokana na dalili zilizotajwa hapo juu.
===
1. AINA YA MLO UFAAO KWA WAGONJWA WA KISUKARI
---
2. MATOKEO YA KUTODHIBITI UGONJWA WA KISUKARI
===

UFAFANUZI, USHAURI NA MAONI YA WADAU KUHUSU TATIZO HILI:
---
---
---
---
---

===
PIA UNASHAURIWA KUSOMA MADA HIZI:
- Tambua siri ya kupatwa na ugonjwa wa kisukari - JamiiForums

- Dawa nyingi mbadala za Ugonjwa wa kisukari zinazotangazwa ni utapeli mtupu, fuata ushauri huu - JamiiForums

- Usizidharau ishara hizi 8 za ugonjwa wa kisukari - JamiiForums
 
Siku hizi watu wengi khususan watu wazima, wanaume na wanawake wanataabika sana kwajili ya ugonjwa wa sukari.

LISHE KWA MGONJWA WA KISUKARI

Suala la lishe kwa wagonjwa na hapa tunamuangalia mgonjwa wa kisukari. Kama tulivyokwisha ona katika makala nyingine zilizopita, mgonjwa yeyote wa magonjwa hatari kama presha, moyo, saratani, kisukari n.k, ni lazima ajue vyakula anavyopaswa kula au kutokula.

Elimu ya lishe ni muhimu sana, kwani madhara ya ugonjwa huonekana haraka na hata kusababisha kifo upesi, iwapo mtu ataendelea kula bila kujijua vyakula vilevile vilivyosababisha tatizo la kiafya alilonalo.

Kwa ujumla, mgonjwa wa kisukari (Diabetic), hana mipaka mingi ya vyakula, anaweza kuendelea kula vyakula vingi kama kawaida iwapo atajua jinsi ya kula, kiasi gani na kwa wakati gani. Hata hivyo, kama ulaji wake ulikuwa hauzingatii ulaji sahihi, baada ya kuugua hana hiyari bali kufuata kanuni za ulaji sahihi.


Kanuni kuu ya ulaji anayopaswa kuzingatia mgonjwa wa kisukari ni kula kiasi bila kushiba sana, kula kwa muda uleule kila siku, na kula mchanganyiko wa matunda, mboga na nafaka zisizokobolewa. Hii ina maana kwamba mgonjwa anatakiwa asisikie njaa wala shibe muda wote wa siku.

KITU GANI UNAKULA?

Bila kujali kama una kisukari au la, afya bora iko mikononi mwako kwa kuwa na hiyari ya kuchagua unachokula. Lakini unapokuwa tayari mgonjwa, unakuwa huna hiyari tena ya kuacha kuzingatia ulaji sahihi, vinginevyo unakiita kifo haraka. Kimsingi, mgonjwa wa kisukari azingatie zaidi ulaji wa vyakula vitokanavyo na mimea, aache kula vyakula vya kusindika, vyenye sukari na mafuta mengi.

WAKATI GANI WA KULA?
Suala la kujali muda wa kula kwa mgonjwa wa kisukari ni la lazima, kwa sababu atatakiwa wakati wote kudumisha kiwango cha sukari mwilini mwake kwa kula kwa wakati uleule ili kuepuka kusikia njaa ambayo husababisha sukari kushuka kwa kasi.

KIASI GANI UNAKULA?
Vilevile suala la kula kiasi kwa mgonjwa wa kisukari si la hiyari tena, bali ni la lazima. Hata mtu akila vyakula bora vyenye virutubisho vya hali ya juu kiasi gani, kama akivila kupita kiasi huweza kusababisha unene ambao ni sababu moja wapo ya ugonjwa wa kisukari, hivyo ni muhimu kuzingatia kiasi.
Mgonjwa wa kisukari hahitaji kuwa na chakula maalumu, bali anatakiwa kutilia maanani ulaji wa mboga, matunda na nafaka zisizokobolewa. Lishe ya mgonjwa wa kisukari ni ya kawaida tu yenye vyakula vyenye virutubisho vingi na mafuta kidogo na kiasi kidogo cha wanga.

ZINGATIA

Mgonjwa wa kisukari anashauriwa kula matunda, lakini anakatazwa kunywa juisi za matunda. Halikadhalika, matunda kama ‘Apples’, ‘Peas’ na mengine ya jamii hiyo, ni bora yaliwe pamoja na maganda yake.
Miongoni mwa matunda bora kabisa kwa mgonjwa wa kisukari ni zababi mbivu, hizi zikiliwa kila siku mara tatu kwa siku, huweza kuwa tiba kabisa ya kisukari.

Halikadhalika majani ya embe nayo ni dawa ya kisukari. Loweka majani mabichi ya mwembe, kiasi cha kiganja kimoja (gramu 15), kwenye nusu lita ya maji usiku kucha, kisha asubuhi yakamue upate maji yake, kunywa kila siku asubuhi na unaweza kukidhibiti kisukari, hasa kile kinachopanda nyakati za asubuhi.
 
Salaam!

Katika milo yote iwe kifungua kinywa, mchana, usiku ama kati ya hiyo- mgonjwa wa kisukari anatakiwa kupunguza vyakula vya wanga- wali, ugali n.k.

Kwa ujumla vyakula vinavyoshauriwa ni vile vyenye "glycemic index ama glycemic load" ndogo.

Vyakula kama 'wholegrains' zina fibre kibao na ndio vizuri zaidi. Kwa hiyo ni vizuri kula matunda na mbogamboga zaidi.

Vinywaji visivyokuwa na sukari pia sio mbaya. Ikiumbukwe kuwa vinywaji vyenye sukari, soda za kawaida kwa mfano sio nzuri hata kwa wasio na kisukari! Zaleta tatizo la kuongezeka uzito-

Kisha mazoezi ni muhimu sana kwa mgonjwa wa kisukari.

Diet ya kuangalia tu kwenye mtandao sio nzuri sana- ingawa waweza kuangalia baadhi ya vyakula, ni nzuri zaidi kuongea na daktari wako ili muweze kupanga nini cha kula- kutokana na mahali mtu anapoishi.

Pombe ni ya kuepuka vilevile.

Kila la kheir.
 
Insulin resistance hutokea kwa watu wote ambao ni obese na hii husababishwa na kemikali ambazo hutolewa na adipose tissue,lakini hii hali(insulin resistance) uweza kusababisha ugonjwa wa kisukari kama pancrease itakuwa haifanyi kazi vizuri,ila kama itakuwa inafanya kazi vizuri itaweza kuzuia hali hiyo hivyo kuweza kuzuia tatizo lisitokee.

Causes of diabetes
TYPE I-caused by completely abscent of insulin hormone due to auto destruction of the pancrease gland.

TYPE 2-caused by few number of insulin receptors (GLUT-4) or their abnormality,another cause is insulin resistance ,only possible if the portion of the pancrease responsible for secrection of insulin is not able so secrete sufficient amount so as to overcome this resistance.
 
DAWA YA UGONJWA WA KISUKARI

Upate aina za dawa zifuatazo, kila moja kiasi cha gram 100, saga pamoja na dawa zifuatazo:

1. Shubiri
2. Ubani
3. Mvuje
4. Ukwaju
5. Habasoda (kiasi cha dawa hizi hazijatwangwa, hivyo jaribu kukadiria mwenyewe) baada ya kusaga vizuri, gawanya katika mafungo matatu yaliyosawa.

Changanya fungu moja na maji kiasi cha chupa mbili na uchemshe kwa dakika kumi. Ipua na iwache ipoe, chuja na hifadhi katika chupa nadhifu. MATUMIZI YA DAYA YENYEWE Tumia kila siku kikombe kimoja cha kahawa kabla ya kula chochote asubuhi kwa muda wa siku 13. Ikiisha dawa hii basi chukua fungu la pili na uchemshe kama ulivofanya kwa fungu la mwanzo. Tumia daya hii tena kwa muda ule ule wa siku 13.

Itakapokwisha dawa hii basi chukua fungu la tatu na uitayarishe kamaUlivyofanya mafungu mawili ya mwanzo. Tumia dawa hii kama dawa hizo mbili za mwanzo ila tu kwa muda wa siku 14 , hii itafanya jumla ya siku za kunywa daya kuwa siku 40. Baada ya siku hizo 40 utajisikia kuwa ugonjwa wa kisukari umekwisha na unaweza kuanza kula vitu vyote ulivyokuwa umekatazwa. Inshallah kwa kudra zake mwenyezi mungu utakuwa umepona maradhi hayo.

Ndugu yangu muislam, ninakuomba unisaidie kuieneza karatsi hii bila malipo ya kipesa na inshallah utapata malipo yaliomema hapa duniani na kesho akhera. Kufanya hivyo utakuwa unaendeleza bidii kubwa iliyofanywa na Kadhi mkuu wa Tabuk Shaikh Saleh Mohammed Al-Tanjisiy amabaye alifanya juhudi kubwa kwa muda mrefu kufanya majaribio ya dawa hii. Mwenyezi mungu amjaze na kumfikishia kila la kheri duniani na akhera pamoja na sisi sote, Amein.

Maandishi haya yamechapishwa upya na Hamoud Hilal Al-Rawahy kwa Nia ya kuyaboresha maandishi haya na kwa nia ya kusambaza ujumbe huu kwa watu wengi inavyowezekana.
 
Nimekuwa na diabetes kwa miaka 12 uzito nilikuwa 92kg,miaka ya karibuni nimeanza kufanya mazoezi mara 3 kwa wiki,kukimbia,kupunguza kula,kulala mapema na kunywa maji mengi.

Kwanza nilikuwa nameza vidonge 8 kwa siku,baada ya kuanza mazoezi nikapunguziwa mpaka 2 kwa siku.Sasa nina uzito 78kg na niko fit sichoki nikikimbia au mozoezini.Kwa muda wa mwezi sijahitaji kumeza dawa mwili umeweza kumudu.

Daktari kanishauri niendelee kupima glucose asubuhi na usiku mwenyewe na kit yangu kwa muda wa mwezi mwingine na kama nitaendelea hivi nitakuwa nimepona.Nilikuwa na type 2 nawashauri wenzangu wenye diabetes wajaribu haya labda nao watafaidika.
 
@Lagatege,
Same here. Nilikuwa kama wewe, uzito huhuo, nimefanya mazoezi, dieting, kuepuka kula mafuta na vyakula vya starch, kula mboga za majani, matunda etc, acha pombe hasa beer, utajikuta uko fit kwa kila hali.
 
Asante sana,hata mie ninakisukari lakini situmii dawa mara nyingi nakula brown bread na jioni sile chochote,nataka kuanza mazoezi hivi karibuni kwani nilikuwa nimeacha sababu ya kazi, nakunywa maji sana,asante kwa ushauri
 
Nadhani mazoezi na dieting ni njia natural kwa kupamabana na ugonjwa huu. Nawashauri wenye kazi za kukaa na usafiri wa gari watumie ngazi badala ya lift.
 
Ndugu naomba mpangilio wa diet yako kwa mfano je hizo mbogamboga zinakuwa chukuchuku au,je diet sodas zinafaa na je ndio kwamba huwezi kula ugali au.
tafadhali nisaidie huo mpangilio wa unavyokula,
asante
 
Ndugu naomba mpangilio wa diet yako kwa mfano je hizo mbogamboga zinakuwa chukuchuku au,je diet sodas zinafaa na je ndio kwamba huwezi kula ugali au.
tafadhali nisaidie huo mpangilio wa unavyokula,
asante
Inafaa tukumbuke tena kwamba ugonjwa wa kisukari ni ugonjwa wa shahamu (cholesterol) vile vile.

Mtu anaweza kuendelea kula chakula chake cha kawaida ili mradi anakumbuka kwamba ni suala muhimu sana kupunguza utumiaji wa mafuta, siagi, samli na margarin.

Mtindo wa kumimina mafuta moja kwa moja katika sufuria au kikaangio si mtindo wa busara hata kidogo. Ni jambo la maana na busara kutumia kijiko cha kulia katika kupima kiasi gani cha mafuta mtu anatia katika mapishi:

Hakikisha kwamba unatia kijiko kimoja cha kulia kwa kila mtu mmoja katika ukoo.

Chakula cha kuchemsha ni cha siha zaidi kuliko cha mikaango kwa sababu ya upungufu wa mafuta.

Afadhali kula chapati/mkate wa kusukuma wa ngano nzima upikwao mkavu bilaya mafuta kushinda ule unaokaangwa kwa mafuta.

Epuka pilau na wali wa nazi na afadhali ule wali wa maji.

Hakikisha kwamba unaitoa, kuikeketa na kutupa shahamu yote ya nyama kabla hujaitia chunguni.
 
Nilipogundulika nina diabetes nilichanganyikiwa na masharti mengi niliyoelezwa na madaktari na watu wengine kuhusu kula mpaka nilipoelekezwa na doctor mmoja kuwa naweza kula vyakula vya kawaida lakini badala ya kula milo 3 mikubwa nile milo 5 midogo kwa siku,mafuta yanayokatazwa ni yanayotokana na wanyama,kijiko 1-2 cha mafuta yoyote ya mimea ni nzuri.

Badala ya kula matunda mengi mara 1 na kupandisha glucose kula kwa mfano ndizi asubuhi,kipande cha papai mchana na embe jioni.Vegetables unaweza kula kiasi utakacho.Kuna kitu ambacho kila mwenye diabetes inabidi ajue,kijiko kidogo cha dalasini-abdalasini(cinammon) katika chai au kahawa asubuhi kinapunguza asilimia 20% ya glucose mwilini na kwa mtu ambaye sukari yake haiko juu sana inatosha kuidhibiti.
 




Watu walio na ugonjwa wa Sukari (kama watu wale wengine) lazima watilie mkazo afya yao ya kila siku.Tofauti imo: walio na ugonjwa wa Sukari, kila siku lazima wapime sukari, wafanye mazoezi na wazingatie afya yao. Ikiwa wewe au mtu unayemjua ana ugonjwa wa Sukari na ameamua kuishi maisha yenye afya, basi Sehemu ya Kujifundisha itakuongezea maarifa kuhusu huu ugonjwa na kukuelekeza kuishi ukiwa na afya.
Hatua ya 1: Jifunze kuhusu ugonjwa wa Sukari
Ni vizuri kujua mambo mengi kuhusu ugonjwa wa Sukari ili uweze kuukimu. Hapa ni yale unayotakikana kujua na kufanya.
Jua ni aina gani ya ugonjwa wa sukari unayo na hatari zake


Usiogope kuuliza maswali na kujua pale utakapopata majibu.

Elewa kuhusu kiwango cha sukari damuni mwako na ni tiba ipi utakayo tumia.

  • Fanya mtihani mdogo kuhusu Insulini.
  • Insulini 101
  • Video: Insulini
  • Ugonjwa wa sukari: Kile unachohitaji.
  • Fungua uchapishe hati, inayokufundisha kufuatilia kiwango cha sukari damini yako.
Fungua uchapishe mpango wa afya nzuri waliye na Ugonjwa wa Sukari.

 
Uja Uzito Na Ugonjwa Wa Sukari

Vidokezi kwa kina mama waja wazito
Unapojiandaa kusheherekea furaha tele kwa kupata mtoto, ni muhimu ujue namna ya kukabiliana na ugojwa wa sukari. Hapa vidokezi vitano vya kuweka akilini kila mara:
1. Husiana kwa karibu na kundi la maafisa wa afya bora ambao ni pamoja

  • Daktari au muhudumu wa kiafya aliye na ujuzi wa kutunza wagonjwa wa Sukari
  • Daktari aliye na maarifa ya uzalishaji anayeweza kushughuikia matatizo katika uja uzito na ambaye amewahi kushughulikia kina mama waja wazito walio na ugonjwa wa Sukari
  • Daktari wa watoto au wa watoto wachanga ambao wamezaliwa ambaye anajua kutibu shida maalum zinazoweza kuwakumba watoto wanaozaliwa na kina mama wanaougua ugonjwa wa Sukari
  • Muhudumu wa ulaji aliyesajiliwa anayeweza kukupangia na kukubadilishia chakula wakati wa uja uzito na baada ya kujifungu
  • Daktari wa ugonjwa wa sukari anayeweza kukusaidia kukabiliana na ugonjwa huu wakati wa uja uzito.
2. Uwe maakini sana na madawa yako: Iwapo unatumia tembe za ugonjwa wa Sukari, inaweza kuwa vigumu kuendelea nazo wakati wa uja uzito. Daktari wako anaweza kukupa ushauri wa kujitibu kwa kujidunga dawa ya Insulin ya kusawazisha kiwango cha sukari mwilini badala ya kuendelea na hizo tembe.

3. Kagua kiwango cha sukari katika damu yako: vile tu unavyoagizwa na daktari au muhudumu wako wa afya bora.

4. Zingatia ushauri wa mjuzi wa lishe bora: fuata mwongozo wake wa aina za vyakula unavyostahili kuvitumia ili kiwango cha sukari mwilini mwako kithibitiwe.

5. Mazoezi ni muhimu katika kutibu ugonjwa wa Sukari: Haijalishi iwapo wewe ni mja mzito au la. Zungumza na daktari wako akueleze iwapo kuna tatizo lolote linaloweza kutokea iwapo utafanya mazoezi ukiwa mja mzito. Ni muhimu kujua hasa kwa wale ambao wana ugonjwa wa Moyo pamoja na, au kiwango cha juu cha sukari mwilini.
 
Niko hatarini kiasi cha kwamba naweza kupata ugonjwa wa Sukari?

Wanasayansi wameshindwa hasa kutambua kinachosababisha ugonjwa wa Sukari mwilini. Pia hakuna hatari zilizo wazi za kuonekana kwa macho kwa aina ya kwanza (Diabetes 1). Lakini aina ya pili (Diabetes 2) ina dalili:
Unene – Hii ni dalili ya kwanza hatari.Mtu akiwa mzito, ana nafasi kubwa ya mwili mwake kukataa aina ya dawa ya insulin kwa sababu mafuta huzuia namna mwili hutumia dawa yainsulin.

Ulegevu na uzembe – Maisha ya mtu kukaa tu ndee si mazuri hasa iwapo mtu huyo ni mnene sana. Mazoezi hufanya moyo kupiga vizuri na kuzuia hali mbaya za kiafya mwilini. Mwili ambao una misuli tu ni rahisi kutumia vizuri Insulini kuliko ule ambao umejaa mafuta katika seli (cells). Hivyo basi, mtu anaweza kurahisisha utendaji kazi wa Insulini kwa kusonga hapa na pale. Pia mazoezi hurudisha chini kiwango cha sukari mwilini na hivyo basi kufanya Insulini kufanya kazi yake vizuri zaidi mwilini. Vile vile kupunguza uzito kitu kizuri. Hivyo basi wacha uzembe!

Mazoea mabaya ya kula: Wagonjwa wengi ambao wamepatikana kuwa na aina ya pili ya ugonjwa wa Sukari pia ni wanene mno. Hawana mazoea mazuri ya ulaji. Chakula kikiwa na mafuta mengi na chakula kilichowekwa kemikali, kile hakina nyuzinyuzi za kutosha, chakula kilicho na kabohaidreti (wanga) nyepesi, vyote huchangia katika kumfanya mtu kupatikana na ugonjwa wa Sukari mwilini. Kula unavyostahiki kwa weza kuzuia aina ya pili ya ugonjwa wa Sukari au hata kuupindua.

Historia ya familia: Wakati mwingine huwa katika jeni (genes) na unarithishwa katika familia. Watu ambao wana jamaa waliopatikana kuwa na aina ya pili ya ugonjwa wa Sukari wao wana nafasi kubwa sana kupata ugonjwa huu. Hali ya maisha ya mtu ndio hasa hufanya mtu apate au asipate ugonjwa wa Sukari.
 
Maswali ambayo yameulizwa sana kuhusu ugonjwa wa Sukari

Ugonjwa wa Sukari ni nini?

Ni ugonjwa ambao hufanya sukari iwe nyingi sana damuni. Walio na ugonjwa huu pia wanaweza kuwa na magonjwa mengine kama vile, ugonjwa wa moyo, figo, shida za macho, na hali zingine tata zinazolingana na hizi.

Kuna tofauti gani kati ya aina ya kwanza na ya pili ya ugonjwa wa Sukari?

Aina ya kwanza, sana sana hupatikana kwa watoto na vijana. Mwili hausawazishi kiwango cha sukari kabisa. Aina ya pili sana sana hupatikana kwa watu wazima. Mwili hujenga sukari lakini huwa haitoshi kulingana na kile kiwango kinachotakikana.

Unapataje ugonjwa wa Sukari?

Huwezi kuzuia aina ya pili ya ugonjwa huu. Husababishwa na mazeoa mabaya ya ulaji, kunenepa sana, na kukaa tu ndee bila kujishughulisha na shughuli zozote muhimu.

Unawezaje kutibu ugonjwa wa Sukari?

Aina ya kwanza hutibiwa kwa dawa ya kusawazisha kiwango cha sukari mwilini (Insulin). Aina ya pili hutibiwa kwa kutumia dawa ya kusawazisha kiwango cha sukari mwilini na tembe. Pia, mtu anastahili kufanya mazoezi, kuwa na ratiba nzuri ya ulaji na kupunguza unene.

Je, dawa ya kusawazisha kiwango cha Sukari mwilini ni nini? (Insulin)

Ni kemikali iliyoundwa katika kongosho (pancrease). Husaidia kusawazisha kiwango cha sukari mwilini.

Hebu sema baadhi ya shida za kudumu za ugonjwa wa Sukari?

Ugonjwa wa Sukari huweza kusababisha magonjwa mengine kama vile ugonjwa wa Moyo, Figo, Kupofuka, Kukatwa kwa viungo vya mwili, huharibu mishipa ya fahamu (neva) na magonjwa ya figo. Ni muhimu ujitunze kwa kutumia dawa zako inayostahili, usikae tu ndee bali ujishughulishe na mambo na ule ulaji unaofaa kwa afya nzuri.

Ni hali gani hatari inayoweza kusabisha na kukuza ugonjw wa sukari?

Sababu na hatari za aina ya kwanza ya ugonjwa wa Sukari bado hazitambulikani. Sababu muhimu kubwa ya aina ya pili ni unene kupita kiasi. Hatari zinginezo ni pamoja na uzee, kutofanya mazoezi, historia ya familia, kabila (sana sana watu wa asili ya Afrika, Waresia na wa asili ya Amerika ya Kilatino) na walio na msukumo wa juu wa damu mwilini na Choresterol

Ni nini baadhi ya njia ambazo kwazo mtu akizifuata atajizuia kupata aina ya pili ya ugonjwa wa sukari?

Zingatia uzani unaofaa kupitia kwa mazoezi na ratiba mwafaka ya ulaji mwema. Kula vyakula vya madini mwilini visivyo na mafuta mengi na sukari nyingi. Jishughulishe kila wakati kwa kufanya mazoezi: usikae tu ndee. Iwapo unaona kuwa uko hatarini na kuna uwezekano kuwa, unaweza kupata ugonjwa huu

Je, kuna dawa ya kutibu ugonjwa huu?

Kwa wakati huu haipo. Hata hivyo kuna dawa nyingi ina matibabu mengi unayoweza kutumia kwa mfano dawa ya kusawazisha kiwango cha sukari mwilini. Matibabu pia huhusisha mtu kupunguza uzani (unene) wako na kuwa na shughuli nyingi pasipo kukaa tu ndee.
 
Njia tano za kufuata kama mwongozo wa kukabiliana na ugonjwa wa Sukari

Mara tu unapoambiwa kuwa una huu ugonjwa, linaweza kuwa ni jambo ngumu kulikubali na kukabiliana nalo. Hisia za kushtuka, hasira, kutamauka, kuogopa na kuwa na majonzi ni za kawaida kwa yeyote baada ya kupata habari kuwa ana ugonjwa wa sukari. Hata hivyo una maisha yako ambayo ni muhimu uyaokoe. Fuata hizi njia tano, kwa uangalifu ili ujue la kufanya wakati wa kukabiiana na hiyo hali yako mpya ya kuwa mgonjwa wa ugonjwa wa sukari.

Hatua ya 1: Jifunze yote yanayokupasa kuhusu ugonjwa huu.

Jifunze na uelewe kila kitu ili ujue unachoshughulikia. Muulize daktari ambaye anajua yote kuhusu ugonjwa huu na aliye na uwezo wa kujibu maswali yako yote. Tambua aina ya ugonjwa wa sukari unaokusumbua. Ni hali gani inayokufanya ujipate hatarini?

Jua vyema kiwango cha sukari kilichoko mwilini mwako na aina ya dawa ya kusawazisha kiwango cha sukari mwilini mwako itakayokufaa maishani mwako. Ni shida gani zinazotarajiwa iwapo utashindwa kuuthibiti ugonjwa huu kwa kiwango kinachotakikana, kulingana na mhudumu wako wa kiafya. Utafiti wako umekusaidia kupata maarifa unayostahili. Kuweza kukabiliana na ugonjwa huu kikamilifu.

Hatua ya 2: Badili mtindo wako wa ulaji

Ili kuweza kukabiliana na kiwango cha sukari mwilini mwako ni muhumu upunguze uzani usiofa, kiasi cha chakula unachojipakulia ni lazima kipungue usifikirie kwa misingi ya utaratibu na ulaji bali njia bora ya kutunza afya yako kwa kula chakula kifaacho vyakula vifuatavyo, visikose kwenye orodha ya vyakula unavyohitaji katika taratibu wako wa ulaji; mboga, matunda, chakula cha kutunza mwili na cha kupatia nguvu mwili wako. Zungumza na daktari wako wa utarativu wa ulaji bora kuhusu mpangilio mwafaka wa mlo utakaouzingatia kwa wakati huu.

Hatua ya 3: Panga mpangilio wa kila siku wa kudumu

Watu wengi walio na ugonjwa huu mara nyingi huwa wanene kupita kiasi na wenye uzani mzito. Hivyo basi ni muhimu, ufanye mazoezi ya kila mara kama njia mojawapo ya kukabiliana na ugonjwa huu. Ni lazima kuwa daktari wako atakupa ushauri utakaoutaka upunguze uzito. Mazoezi mwafaka zaidi ni kuwa na mpangilio utakaokufanya uwe na nguvu za uthibiti wa moyo wako kwa kufanya mazoezi yanayolenga hayo mambo mawili. Baada ya ushauri wa daktari unaweza kuamua kujiunga na chumba au kiwanja cha michezo ya kuzoeza viungo vya mwili ama ujiunge na kundi la YMCA/YWCA ili upate msaada unaohitaji kuendelea kuyathibiti maisha yako na hali yako ya wakati huu. Kama sivyo, kuna namna nyingi za kujipangia mazoezi ya kibinafsi pale pale tu nyumbani.

Hatua ya 4: Meza dawa zako inavyotakikana

Watu wengine walio na aina ya pili ya ugonjwa huu huhitaji kumeza tembe zao inavyostahili ama kujidunga dawa ya kusawazisha kiwango cha sukari mwilini ili miili yao itumie sukari iliyomo katika matunda na mimea kupata nguvu. Aina hii ya sukari huvunjwavunjwa tena wakati wa kuyeyusha chakula kinywani na tumboni ili kifae kuchukuliwa na damu mwilini kama ifanyikavyo na chakula cha namna kilichomo katika nyama, ute wa yai na samaki (chakula cha kutunza mwili) Dawa ya kusawazisha kiwango cha sukari mwilini haipatikani kwa hali ya tembe. Yaliyo chini ya ngozi yako ili ingiie mara moja ndani ya damu yako.

Hatua ya 5: Tafuta usaidizi (msaada)

Huenda ikawa, utaweza kukabiliana na huu ugonjwa bila shida lakini ni muhimu utambue kuwa unahitaji msaada wa watu wengine ili mzigo ukuwie mwepesi kidogo. Tegemea jamaa na marafiki wakutegemewa ambao watakuwepo kila mara utakapohitaji msaada wao, katika hiyo hali yako mpya ya kisasa. Jishughulishe na vikundi vya watu walio na hali sawa na yako, pia jihusishe na shughuli za kijamii na kutafuta pesa na kuelimisha watu wanaoishi karibu nawe kuhusu ugonjwa huu.
 
DAWA YA UGONJWA WA KISUKARI

Dawa ya Sukari ! Wabilahi Taufiq


Dawa ya Sukari (Diabetes)

Sheikh Saleh Mohammed Tuwaijiri (May Protection of Allah be on him),

Qadhi Mkuu wa korti ya Tabuk kafanya uchunguzi mkubwa kwa kuvumilivu

na kwa subira kubwa mpaka kupata hii dawa ya magonjwa ya sukari.


Siku hizi watu wengi khususan watu wazima, wanaume na wanawake

wanataabika sana kwajili ya ugonjwa wa sukari.



Ingredients
:



1 – Unga wa ngano 100 gm


2 – Gundi (umefanan na ubani wa kiarabu lakini hauna harufu) 100 gm


3 - Shaair 100 gm


4 - Habba Soda 100 gm



Namna ya kutengeneza



Chemsha hivyo vitu juu katika vikombe 5 vya maji kwa muda wa dakika

10.
Zima moto na wacha ipowe. Ikisha kupowa chuja na utie katika chupa.



Matumizi



Kunywa kikombe kidogo kila siku asubuhi kabla ya kula chochote kwa

muda wa siku 7.
Wiki ya pili kunywa siku moja na uwache siku moja.

Insha-Allah baad hizi wiki mbili utapona na utaweza kula chakula kama

dasturi.
Sheikh anaomba muwapelekee wenzune wapate na wao

kunufaika.
Insha Allah Allah atajaalia iwe dawa kwa kila mwenye haya

maradhi. Aameen.
Kwa hisani zenu musiwasahau kwenye dua zenu Sheikh,

alieye tarjum kwa Kiswahili na kila anaye ipeleka mbele.
 
Kisukari ni ugonjwa unaosumbua sana naomba kujua tule chakula gani? ukiondoa kufanya mzoezi, naomba msaada mnaojua vizuri.
 
Pole ndugu,
Kuna aina nyingi ya vyakula ila nitakuambia vichache, kwanza natakiwa ajue ni nini hatakiwi kula

Aina zote za nyama kama Ya ng`ombe (beef) with brown rice, brown bread.
Kuku, aina zote za samaki, (sea food)
Mayai
Maziwa
Mboga mboga kwa wingi na matunda Green beans, uyoga, vitunguu, maboga, nyanya.

CORNWELL QUALITY TANZANIA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…