Tatizo la ajira - mbinu mpya ni kufanya internship

Tatizo la ajira - mbinu mpya ni kufanya internship

Kisendi

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2009
Posts
699
Reaction score
180
Ndg wana JF
Wadogo zetu wengi hawana ajira, na siri ya mjini huwezi kujiajiri kama huna pakuanzia. Walio wengi ambao mimi nawafahamu wamejiajiri wameajiriwa kwa hiyo kama kampuni zao zikienda mrama huengemea kwenye ajira lakini ukijiajiri na kampuni yako ikafa utalia na kusaga meno.

Mbinu nzuri kwa vijana wetu taufteni Kujitolea kama vijana wengi wa mataifa ya mbali wanavyofanya. Tafuta kazi ya kujitolea kama INTENSHIP Popote. Mhimu uwe na uwezo wa kupata nauli na chakula cha mchana. Kuna baadhi ya makampuni au ofisi za serikali zina mabus ya kubeba watumishi.

Vijana wangu niwaombe mtafute intenship mtapata..kuanzia hapo sasa ndo safari inaanzia.

Nawapenda wote.
 
Asante kwa ushaur me naufanyia kaz leo maana ntaandika barua nakupeleka kesho inshaallh..
 
Mimi binafsi sio kwamba sipendi kujitolea....hizo nguo nnazovaa kazini ntafulia nini? Ntakula nini?
 
Mimi mwenyewe niliomba kujitolea, nilikuwa napewa hela ya nauli tu, lakini baada ya mwezi mmoja tu nikasain contract na mshahara unaridhisha tu. Mwanzoni niliona hata huo mwezi sitaufikisha lakini nikajikaza kiume. Kwa hali ya sasa hivi ni bora kutafuta kujitolea kwanza.
 
aksante kwa ushauri mzuri....:smile-big::smile-big:
 
ushauri mzuri ,lakini nafasi za kufanya internship ni adimu sana .BINAFSI NATAFUTA NAFASI YA KUFANYA INTERNSHIP POPOTE ,ELIMU YANGU NI LLB
 
ushauri mzuri ,lakini nafasi za kufanya internship ni adimu sana .BINAFSI NATAFUTA NAFASI YA KUFANYA INTERNSHIP POPOTE ,ELIMU YANGU NI LLB

Serious Mkuu? Hata kama sio necessarily inahusu kada ya sheria?
 
hivi ukifanya internship katika ofisi za serikali, ambazo ajira zake zinatoka/zinasimamiwa na UTUMISHI, wewe utafaidika nini? isijekua mwisho wa siku wanakuja kukuramba kama kawaida tu.
 
sometimes kuajiriwa ni Bahati, au Mpango wa Mungu naona, ( sawa na kupiga chabo wakati wa final exam ukafaulu japo hukupitia kitu kwenye hilo pepa). unaweza ukafanya internship all over years (gvt offices) lakin ukapata ajira pengine na ukajutia kwa nini ulifanya hyo internship. Tusiamin asilimia mia mia kuwa inasaidia.. ni hayo tu..
 
tatizo kupata pa kujitolea napo ni shughuli, kwa mfano anayejua wanapopokea watu wa kujitolea a list tuzijue.....field tu mtihani hadi umjue sijui nan ..
 
Kuna kijana alikuwa akijitolea hapa ofisini kwetu kwa miezi kama 6 hivi. Ikatanganazwa nafasi ambayo yeye anaqualify, nafasi zilikuwa mbili....na ni taasisi ya serikali. HR wakamwambia aombe. Na kazi akapata bila taabu maana kazi alikuwa akifanya za nafasi zili zilizotangazwa na alizimud vizuri kabisa. Kwa kweli ukiwa pale unafanya kujitolea kazi ikiji lazima wakupe labda kama HR anaroho ya chui...
Naamini vijana mtatoka tu kikubwa usikate tamaaaaaaaaaaaa
 
Mimi niliwai kufanya internship mahali kwa muda wa miezi mitatu, na kabla ha yapo niliwahi kufanya ofice hiyo hiyo field kwa miezi sita, kwahiyo ukichukua hiyo miezi mitatu ya internship na iyo miezi sita ya field inakuwa jumla ya miezi tisa, na walikuwa wakinitumia kihaswa haswa, nilicho kuwa naambulia pamoja na kufanya kazi kwa kujituma ni pesa ya nauli tu, internship lakini sikuona dalili yoyote ya kuajiriwa na, na kuna post zilitoka za kitengo kingine ilikuwa ni kificho kifocho wakawaajiri watu wao, ila Mungu mwema nikapata kazi sehemu nyingine nilichoambulia kwenye office ile ni kupata uzoefu wa kazi tu, Unaweza ukawafanyia watu kazi mda mrefuuu, ukawaingizia pesa nyingi lakini wasiwe na shukrani hata kukuajiri parmanent, wataanza kutupiana mpita tu menager wako na HR ukiona hivyo wewe tafuta uzoefu tu ukiupata kazi sehemu nyingine wewe sepaaa!!
 
Internship zenyewe kwanza kupata shida pili ukipata unaweza usiajiliwe pindi unapomaliza. Bora hata voluntee ukionewa huruma unapewa ajira.
 
Kuna kijana alikuwa akijitolea hapa ofisini kwetu kwa miezi kama 6 hivi. Ikatanganazwa nafasi ambayo yeye anaqualify, nafasi zilikuwa mbili....na ni taasisi ya serikali. HR wakamwambia aombe. Na kazi akapata bila taabu maana kazi alikuwa akifanya za nafasi zili zilizotangazwa na alizimud vizuri kabisa. Kwa kweli ukiwa pale unafanya kujitolea kazi ikiji lazima wakupe labda kama HR anaroho ya chui...
Naamini vijana mtatoka tu kikubwa usikate tamaaaaaaaaaaaa

Mkuu, kumbuka kuna baadhi ya nafasi za kazi kutoka taasisi za serikalini zinatangazwa UTUMISHI na wao ndio wanaajiri. Ili unaliongeleaje?
 
Kwa vijana wa chuo, wapenda maendeleo Umri kati ya miaka 18-40, Kambi maalum ya kimataifa kwa vijana inatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 3-17, Agosti, 2014 na nyingine 31,Agosti- 13,September,2014. (Kwa muda wa wiki Mbili Kila moja.)
Jifunze, Shiriki, Jumuika, na Badili Fikra.
PROGRAMS;
ENVIRONMENTAL ISSUES
BUSINESS PLAN WRITING
RESEARCH AND REPORT WRITING SKILLS
HUMAN RIGHTS ADVOCACY
GOOD GOVERNANCE & LEADERSHIP SKILLS.
ENTREPRENEURSHIP SKILLS
HEALTH CARE AND LIFE SKILLS
VOLUNTEERISM PROGRAM
INTERVIEW SKILLS
+ TOUR DURING THE WORK CAMP TO (E.g MIKUMI NATIONAL PARK, ULUGURU MOUNTAINS, WATER FALLS AND OTHER TOURISTS AREAS to Promote National Tourism Sector).
Unaweza kutuma maombi yako sasa, Kwa Maulizo na Taarifa zaidi
Wasiliana nasi moja kwa moja.
Barua pepe: wwtyouthexchange@gmail.com
Simu/ Whatsapp: 0716 979 939/ +255 712 439 124/ 0756 438 070
Landline: 023 262 3036
Twitter: @IycepTanzania





 
Back
Top Bottom