Tatizo la ajira kwa walimu...

Tatizo la ajira kwa walimu...

Rebeca 83

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2016
Posts
15,669
Reaction score
33,691
Hello JF,

Haiwezekani 90% ya walimu wanaohitimu wawe unemployed...

kuna tatizo mahali...

I just think,mfumo wa kuwapata walimu hawa ndio tatizo..

sina uhakika sababu sijalifanyia utafiti ila nadhani viwango vilivyowekwa kwa watu kusomea ualimu ni vidogo,hivyo kufanya watu wengi kukimbilia ualimu baada ya kuona kwengine haiwezekani kuingia….

,na kama wanaosomea ualimu ni wengi,then tatizo la ajira zao lazima liwe expected....

serikali iwe honest,kutochukua intake ya walimu wengi,ndio suluhisho...

sio umfundishe mtu then usimpe kazi….

kuwa realistic unahitaji walimu wangapi,

idadi yao ndio utoe nafasi wasome...

its soo unfair ,kuchukua walimu wote hawa uwasomeshe huku ukijua nafasi ni chache...

another solutionni ku raise the bar; Vigezo vya kuchukua wanafunzi wa ualimu viongezwe...

wachache wata qualify kuingia na wakihitimu,watakua na uhakika wa ajira….
 
Tatizo la ajira si walimu pekee, ni kada zote.

Ukidahili walimu wachache, hao wengine wataenda kada zingine, na watajaa kama walimu.

Suluhiso ni serikali kuangalia namna bora ya kuaaidia vijana wanaomaliza chuo kikuu waweze kujiajiri au kuajiriwa. Serikali ikuze sekta binafsi nk.
 
Hee hapo ni ualimu tu.
Vuta picha taaluma kama za kifedha,sijui mambo ya development na makorokoro mengine....
Watu wanasubiri ajira.
 
Watumishi wa serikali hawafiki milioni 1.

Tupo milioni.....

Uki-control udahili wa walimu je hao walioachwa na vigezo vya udahili si wanaenda kuwa Jobless pia.

Ajira ni tatizo la dunia....ukija kwa sera zetu kuanzia mfumo wa elimu wa hapa kwetu ndiyo kabisaaa...unashindwa uanzie wapi kulijadili. Nadhani hata watunga sera huwa wanachanganyikiwa pia maana nao wameandaliwa na mfumo huo huo.
 
Umeandika kivivu ati vigezo vya ualimu Ni vidogo kwahiyo hata wa diploma,degree não Ni vigezo kidogo? Acha zako
Tatizo serikali haina uwezo wa kuajiri mbona miaka ya nyuma wote waliajiriwa?
Kamati ya bunge ilisema shule za msingi Zina uhaba wa waalimu 123000 secondary 86000 Sasa unaaemaje kuwa Hakuna uhitaji wa waalimu?
Sema serikali haina pesa kuwaajiri
 
Tatizo la ajira si walimu pekee, ni kada zote.

Ukidahili walimu wachache, hao wengine wataenda kada zingine, na watajaa kama walimu.

Suluhiso ni serikali kuangalia namna bora ya kuaaidia vijana wanaomaliza chuo kikuu waweze kujiajiri au kuajiriwa. Serikali ikuze sekta binafsi nk.

Mkuu,serikali ikicheza na figures sidhani kama tatizo litakua kubwa namna hio..almost 90%??? hapana,this is cheating...….....

I agree with you kwenye serikali kuandaa vijana kujiajiri na kuajiriwa..thanks.
 
Unafikiri watu wajikite kwenye kozi zipi, waachane na ualimu?
 
Umeandika kivivu ati vigezo vya ualimu Ni vidogo kwahiyo hata wa diploma,degree não Ni vigezo kidogo? Acha zako
Tatizo serikali haina uwezo wa kuajiri mbona miaka ya nyuma wote waliajiriwa?
Kamati ya bunge ilisema shule za msingi Zina uhaba wa waalimu 123000 secondary 86000 Sasa unaaemaje kuwa Hakuna uhitaji wa waalimu?
Sema serikali haina pesa kuwaajiri

yaani kuna uhaba wa walimu,at the same time kuna kundi kubwa la walimu hawajaajiriwa,it doesn't make sense sir!

serikali haina pesa kuwaajiri,kwani miaka yote pesa ilikuwa wapi?? mbona na wewe unaandika kivivu…??

nimesema again sijalifanyia uafiti,ila nikichunguza na kujua kama ualimu vigezo ni vidogo kuingia….nakuja kukuchapa fimbo,lol 😳😳
 
Unafikiri watu wajikite kwenye kozi zipi, waachane na ualimu?

sijasema waachane na ualimu,ila serikali iwe honest,kutochukua intake kubwa wakati kuajiri nafasi ni chache,kila mtu asome anachokipenda ndugu,kama ualimu ni kitu unachokipenda then somea tu ndugu
 
Watumishi wa serikali hawafiki milioni 1.

Tupo milioni.....

Uki-control udahili wa walimu je hao walioachwa na vigezo vya udahili si wanaenda kuwa Jobless pia.

Ajira ni tatizo la dunia....ukija kwa sera zetu kuanzia mfumo wa elimu wa hapa kwetu ndiyo kabisaaa...unashindwa uanzie wapi kulijadili. Nadhani hata watunga sera huwa wanachanganyikiwa pia maana nao wameandaliwa na mfumo huo huo.

ujobless uko kila mahali ila kusomesha watu wengi wakati una uhakika hutawapa ajira..this is cheating,kwanza hio hela/gharama kubwa ya kuwafundisha ingekua invested somewhere else ingeweza kucreate jobs somewhere else....sijakataa watu wasiwe walimu ila kwa kweli ukiangalia figures za walimu ambao wamekosa kazi,its heartbreaking….
 
Solution ni Serikali inabidi iwekeze sana kwenye elimu ya Ujasiriamali mashuleni pamoja na mavyouni vilevile Serikali inabidi iwekeze hela nyingi kwenye Miradi ya Kifedha itakayokuwa inawapatia watu mitaji bila ya Riba na Masharti Magumu

Lakini tukiendelea na mfumo huu wa elimu ni shida siku hizi wanaituhuzia Underwear, leso, Boxer, soxi, mahindi ya kuchoma, karanga na machungwa ni MaGraduate
 
Elimu sio kwa ajira tu.

Suala la kuwasomesha walimu ni mtambuka.

Navyoelewa mfumo wa HESLB.

Wanatoa mikopo kwa vigezo vikubwa Uwezo wa kiuchumi wa mwanafunzi, course na ufaulu wake.

Kozi za ualimu ziliwekwa kama kigezo cha kupata mkopo kwasababu ya uhaba wa walimu. Ila kwasasa huu utaratibu wa kumpa kila mwalimu mkopo umepungua...aidha ukidhi vingine ndiyo unapata.

Ajira haipo kwa kada zote...sema walimu ni wengi kutokana na mfumo uliyowekwa hapo mwanzo.

Ajira ni tatizo.
 
hili swala silijui kwa undani..hapo nilipobold,mfumo ulikuwaje mpaka ukazalisha walimu wote hawa?
 
Solution ni Serikali inabidi iwekeze sana kwenye elimu ya Ujasiriamali mashuleni pamoja na mavyouni vilevile Serikali inabidi iwekeze hela nyingi kwenye Miradi ya Kifedha itakayokuwa inawapatia watu mitaji bila ya Riba na Masharti Magumu

Lakini tukiendelea na mfumo huu wa elimu ni shida siku hizi wanaituhuzia Underwear, leso, Boxer, soxi, mahindi ya kuchoma, karanga na machungwa ni MaGraduate

Uko sahihi mkuu...lazima kitu kifanyike...kubadiisha hii hali,otherwise tusitegemee embe chini ya mnazi...miaka mitano baaadae sipati picha walimu wasiokua na ajira watakua wamefikia wangapi...kama hili tatizo halitakua fixed.
 
Yaani kuanzia mwaka 2015 direct employment za Walimu serikalini ilianza kutetema mwaka 2017 ikaja OTEAS kwa nafasi finyu sana kisha 2019 OTEAS imerudi kuchukua wengine tena kwa ufinyu Bora Enzi za Kikwete alijitahidi sana kutoa ajira lakini Awamu hii hela imeelekezwa kwenye Ndege, Miundombinu na kununua wapinzani, kufanya uchaguzi basi ajira sio kipaumbele tena

Usiache mbachao kwa msala upitao!!!!
 
Nimependa michango yako mkuu kwenye hii topic..lol ...
 
hili swala silijui kwa undani..hapo nilipobold,mfumo ulikuwaje mpaka ukazalisha walimu wote hawa?
Kwa ufupi...kulikuwa na uhaba wa walimu baada ya shule za kata.

Njia ilikuwa wapatikane kwa namna yoyote.

Ukiachana na walimu wa kupigwa msasa kwa miezi kadhaa kipindi cha awamu ya kwanza ya JK.

Utaratibu ukawa...vyuo viongeze udahili wa course za ualimu na board ya mikopo iwape kipaumbele wanaoenda kusoma ualimu.

Nani asiyependa mkopo aslimia 100?

Vyuo binafsi navyo vinahitaji pesa...ni mmiliki gani wa chuo asiyehitaji wanafunzi wanaolipiwa ada asilimia zote na serikali? Wakaongeza courses za education.

Lingine ikawa ukimaliza chuo kwa shahada ya elimu unapangiwa moja kwa moja..hivyo ikawa ukidahiliwa ualimu unaajira yako moja kwa moja.

Mwishowe asilimia nyingi ya wanafunzi ikachagua ualimu.
 
Asante mkuu...

sasa hio crisis haipo tena,

kwa nini bado wanatoa mikopo na vipaumbele,huku wakijua ile ilikuwa as a response to crisis??

au wanaogopa kupata uhaba tena…???

mnhh..

kwa kweli hii trend ikiendelea..sijui miaka mitano ijayo,tatizo litakua na magnitude gani….mmmmnhhh
 
Tuanzishe shift career... Yan MTU unafanya kazi miaka kumi zen waondoka wanakuja wengine.
 
ujobless uko kila mahali ila kusomesha watu wengi wakati una uhakika hutawapa ajira..this is cheating,kwanza hio hela/gharama kubwa ya kuwafundisha ingekua invested somewhere else ingeweza kucreate jobs somewhere else....sijakataa watu wasiwe walimu ila kwa kweli ukiangalia figures za walimu ambao wamekosa kazi,its heartbreaking….

Hivi, kwa mtazamo wako, jobless rate katika taaluma ya ualimu ndiyo the highest jobless rate miongoni mwa jobless rates za taaluma zote? Nitashangaa kama ndivyo. Serikali ilishaacha au kupunguza kasi ya kuajiri watu wa taaluma zingine nyingi kitambo sana (kabla ya slowdown ya ajira za walimu)!

Kwanini walimu kukosa ajira ni “heartbreaking” lakini wataalamu wengine kukosa ajira is no big deal?
 
Back
Top Bottom