Tatizo: Hatuna chama hata kimoja kizuri Tanzania

Tatizo: Hatuna chama hata kimoja kizuri Tanzania

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
9,590
Reaction score
14,921
Baada ya kufuatilia kwa muda nimegundua tatizo mojawapo tulilonalo ni la kisiasa. Tanzania hatuna na hatujawahi kuwa na chama chochote cha siasa kizuri. Hivyo tuna chaguzi ambazo wananchi tunalazimishwa kuchagua nani mbaya kidogo kuliko wengine.

CCM chama tawala kama wangekuwa wazuri wasinge kuwa na haja ya kutumia watendaji na wafanyakazi wa serikali kubana upinzani ambao u a asilimia ndogo sana ya wabunge.

Tatizo ni kwamba wanajua hawapendwi hivyo. Kuna viongozi wanapendwa CCM lakini sio chama wala sera zake. Hizo wanazoita ilani ni za miaka ya 46 maana siku hizi Dunia inabadilika kila siku na ndiyo maana huwezi kutegemea ilani ya miaka 3 au 4 ikafanikiwa kwa miaka hii.

Dunia ya sasa ni full capitalist hivyo hata miradi itatekelezwa sio kwa ilani bali upatikanaji wa pesa ambazo nyingi zinatoka kwenye mabank ya nje! Sasa kuna ilani gani imesema nenda world bank kuomba pesa na mikopo ya maji au daraja ? Hakuna.

Lakini vilevile chama kama CCM wanajali zaidi kubaki madarakani kuliko kuweka sera za kusaidia nchi. Yaani wana watu mpaka vijijini wa uenezaji lakini huwezi kusikia wataalamu wowote vijijini kama wa kilimo, technology na ubunifu na ndiyo maana ni sifa watu badala ya kuongelea maendeleo vijijini wanataka kuongelea chama. Vilevile ajira, sera za land bado ni changamoto

Kwa wapinzani bado hawana movement yeyote ya maana. Upinzani hawajafikia hatua ya kuweza kuweka msukumo kwasababu ya kubanwa lakini vilevile upinzani unagawanyika sana badala ya kuwa wamoja mfano wamengekuwa na agenda ambazo ni mmoja kama ajira. Lakini bado kuna mambo ya Zanzibar, udini, ukanda kwenye vyama.

Hivyo Watanzania hatuna chagua zuri bali tunachagua kati ya wabaya. Mungu atasaidia tutabadilika miaka ijayo
 
Tanzania hakuna chama cha siasa zaidi ya CCM ,vingine ni asasi za kisiasa za mikopo, vingine ni asasi za kuhamasisha migomo na maandamano na shughuli nyingine nyingi za asasi hizo
 
Tanzania hakuna chama cha siasa zaidi ya CCM ,vingine ni asasi za kisiasa za mikopo, vingine ni asasi za kuhamasisha migomo na maandamano na shughuli nyingine nyingi za asasi hizo
Hata hiyo ccm haina hadhi.Ccm ni genge tu lililopora mamlaka ya wananchi.
 
Ukiweka ushabiki na mapenzi na chuki binafsi kwa vyama na viongozi, upo sahihi sana.

Wapo watu wanavipenda sana vyama vya upinzani, siyo kwa sababu ni bora bali ni kwa sababu wanaichukia CCM kwa mambo yake ya hovyo mengi. Wapo watu wanaichukia sana CCM na serikali kwa sababu ya Magufuli. Lakini wapo watu wanaojua kuwa CCM haina chochote cha maana lakini wanaishabikia sana kwa sababu ya Magufuli.

Lakini ukienda kwa undani na kwa uhalisia, vyama vyetu vya siasa, viongozi wake, na wanachama wao - kote kuna shida.

CCM ni chama kinachofanya sisa za hila. Ni chama ambacho kimekosa mvuto kutokana na kufanya siasa dola.

Vyama vya upinzani vinafanya siasa zilizokosa mikakati. Vinaridhika kwa sababu tu kuna watu wanaviunga mkono japo uungwaji mkono wenyewe unakosa agenda ya msingi ambayo ina uwezo wa kuwabeba wapinzani wote na wananchi wanaochukia hila za CCM kwenye behewa moja.
 
Unaweza kuwa na chama cha upinzani imara ndani ya mfumo kama huu?!
Screenshot_20191016-224559-picsay.jpeg
 
Tatizo ni kwamba hatuna DIRA ya Taifa ambayo ingekuwa mwongozo kwa tunaowapa dhamana kutuongoza. Tunategemea kuongozwa na sera/ilani za vyama, matokeo yake jana kilimo kwanza, leo Tanzania ya viwanda/miundombinu. Haieleweki atakayekuja kesho atasimamia nini. Vululu vululu.

Rasimu ya Katiba ya Warioba ingetusaidia sana.
 
Mtoa mada unaanza kukua kifikra.

Kunahitajika mageuzi makubwa sana kwenye uwanja wa siasa. Vyama vipo ila wa kuendesha vyama hivyo, kupanga sera watakazoziamini na kuzikinai wamekosekana.

Kila mtu kwenye chama anajali nyama kwanza chama baadae.

Ni sawa na mlinzi anayemsaliti bosi wake kwa majambazi wenye silaha za moto kwa ajili ya kuokoa uhai wake.
Halafu kwa nini unataka upinzani uungane? Huoni tutakuwa na vyama viwili badala ya vingi???
 
Back
Top Bottom