Alimpeleka akakomae kidogo na pia yule hatoki bara ulaya, hivyo hakuwa na kibali bado cha kufanya kazi Uingereza. Ila sasa mambo yameshakaa sawa, na siku iliyofuata baada ya mechi ya Emirates cup dhidi ya Benfika, Wenger aliulizwa kama Campbell una timu yamtaka na je wako tayari kumuuza? Alichojibu wenger ni kwamba HAWEZI kumuuza wala kumpeleka kwa mkopo timu nyingine. Yupo kwenye mipango yake ya mwaka huu na kuendelea. Hivyo, dogo ndo kesharudi nyumbani, na kwa mechi kadhaa nilizomuona, dogo yuko poa! Hivyo natumai miaka ya neema ndo hiyo imerudi.