MIXOLOGIST
JF-Expert Member
- Mar 1, 2016
- 12,695
- 31,478
Habari za asubuhi wana JF.
Kwa heshima na taadhima naomba nitoe tathmini ya haki kwa utendaji wa Mh Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Kimsingi, miaka mitatu na nusu ni kipindi kizuri cha kupima utendeaji na kutolea mapendekezo ya kuboresha kwenye kipindi cha mwaka mmoja na nusu uliobakia, kama hatakuwa na nia ya kugombea kipindi kingine.
Kwanza kabisa naomba nieleze bayana ninampima Raisi kwa kutumia vigezo vifuatavyo:
1. Ustawi wa uchumi wa Taifa;
2. Ustawi wa kiuchumi wa wananchi wa Tanzania;
3. Usalama wa nchi;
4 Usalama wa wananchi na mali zao; na
5. Uhimilivu kwenye siasa za kimataifa
Ustawi wa Uchumi wa Taifa
Uchumi wa taifa unakua kwa kiwango cha kuridhisha, japokuwa imani ya wawekezaji ilipotea hapo awali lakini uwekezaji unaanza kuja japo si kwa kasi sana. Ila uchumi upo imara na uwekezaji katika miundombinu ni wa hali ya juu sana. Kwangu mimi, nampa sifa nyingi sana kwa uwekezaji unaofanyika hususani kwenye reli, barabara, viwanja vya ndege, bandari, maji na umeme. Hali hii ikiendelea kwa miaka mitano ijayo taifa letu litakua limeingia kwenye kundi la nchi za uchumi wa kati.
Ustawi wa kiuchumi wa wananchi
Kimsingi serikali kazi yake ni kutengeneza miuondombinu wezeshi itakayofanya wananchi waweze kujiongeza kiuchumi. Miundombinu wezeshi ipo na sehemu kubwa ya wananchi wamepewa fursa kufanya shughuli zao bila ya kubugudhiwa na intervention mbali mbali zimefanyika ili kuweka mazingira wezeshi na hili pia nampongeza sana Mh. Raisi.
Usalama wa Nchi
Nchi yetu iko salama na hili si lakuzungumza sana
Usalama wa wananchi na mali zao
HIli kidogo linaleta mjadala, kuna hisia baadhi ya wananchi hawapo na mali zao hazipo salama na sehemu kubwa ya wananchi hawa ni wale wakosoaji. Naendelea kusisitiza wanachi wote na mali zao wanapaswa wawe salama bila kujali mitazamo yao kiitikadi. Kwa hili kidogo Mh. Raisi anapaswa kulifanyia kazi
Uhimilivu kwenye siasa za kimataifa
Niko kifua mbele kuona nchi yangu inasimamia mambo inayoyaamini bila kuogopa wala kujali mashinikizo kutoka kwa nchi zilizoendelea. Kwangu mimi hili ni jambo linalonipa faraja kuona tunapigania sovereignty yetu. Hongera sana Mh. Raisi, tulipata uhuru 1961 hakuna kurudi nyuma
Haya ni maoni yangu kama unayo ya kwako si vibaya ukaendelea bila kutokwa na povu