Tathmini ya Mikopo ya Elimu ya Juu

Aug 15, 2013
55
23
Tupe Maoni Yako ( Matusi Hapana )

Serikali yatumia bilioni 459 kwenye mikopo
ya wanafunzi kwa mwaka wa masomo
2015/2016.
Serikali imetumia bilioni 459 kuwakopesha
wanafunzi wa elimu ya juu katika kipindi cha
mwaka 2015/2016 ambapo jumla ya wanafunzi
122,486 wamenufaika.
Hayo yamesemwa na Meneja wa Habari Elimu na
Mawasiliano wa Bodi ya Mikopo kwa wanafunzi
wa Elimu ya Juu Bw. Omega Ngole wakati wa
mkutano na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es
salaam.
“Walionufaika na mikopo katika kipindi cha
2015/2016 ni wengi na haijwahi kutokea katika
Historia tangu kuanzishwa kwa Bodi na haya ni
matokeo ya utendaji mzuri wa Serikali ya awamu
ya tano “alisisitiza Ngole
Akizungumzia utolewaji wa mikopo Katika kipindi
cha mwaka 2014/2015 Ngole alibainisha kuwa
jumla ya wanafunzi 99,069 walipata mikopo na
jumla bilioni 341 zilitolewa .
Pia Ngole alibainisha kuwa Serikali imeongeza
idadi ya wanaufaika wa mikopo kwa kuzingatia
vipaumbele vinavyotokana na mahitaji ya Taifa.
Ngole amebainisha kuwa mafanikio hayo ni
matokeo ya utekelezaji wa Falsafa ya Serikali ya
awamu ya tano inayosema Hapa Kazi tu.
Aliongeza kuwa Bodi hiyo inaendelea kufanya kazi
kwa kuzingatia kasi ya Serikali ya awamu ya tano
itakayowezesha kutoa mikopo kwa wakati kwa
kuzingatia sheria Kanuni. na Taratibu za utoaji
mikopo.
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya juu ni
Taasisi ya Serikali iliyoanzishwa kwa mujibu wa
sheria Na.9 ya mwaka 2004 na kuanza rasmi
mwezi julai, 2005 ambapo Katika mwaka wa
Masomo 2005/2006 idadi ya wanafunzi waliopata
mikopo ilikuwa 42,749 ambapo jumla ya bilioni
56.1 zilitolewa.

NINI MAONI YAKO.
 
Tupe Maoni Yako ( Matusi Hapana )

Nilitaka tu kujuzwa maana ya mkopo!
Naona tu ktk taarifa hii bodi imejisifia kupata pesa za kutosha kutoka serikali ya awamu ya tano kugharamia elimu ya juu.

vipi kuhusu makusanyo ya mikopo waliyokopeshwa wasomi wa nchi hii tangu bodi hiyo ianzishwe? Nasema hivi kwa sababu hadi sasa bodi ya mikopo bila sababu ya msingi imeshindwa kabisa kuwabaini wanufaika wa mkopo.
Wapo baadhi wanakatwa huku wengine wakiwa wanadunda tu makazini! huu ni udhaifu mkubwa. Nina imani kama bodi ingesimamia kwa umakini urejeshwaji wa mikopo kwa wanufaika basi hadi leo isingeendelea kuitegemea serikali iiwezeshe! na pia tusingesikia wala kuona wanachuo wakilalamikia kukosa au kucheleweshewa mikopo yao! Ni wakati sasa bodi ya mikopo kuwabaini wadaiwa wake hasa wale waliopo makazini ili sheria ifuate mkondo wake.
Bodi iache kusubiri na kuwategemea waajiri wawapelekee majina na badala yake wao ndio watembelee maofisi ili wanufaika waanze kurudisha mikopo yao.
Nafurahia kuwa mmoja wa wanufaika na pia nikiwa nakaribia kumaliza deni la bodi ndani ya miaka michache ijayo!

Serikali yatumia bilioni 459 kwenye mikopo
ya wanafunzi kwa mwaka wa masomo
2015/2016.
Serikali imetumia bilioni 459 kuwakopesha
wanafunzi wa elimu ya juu katika kipindi cha
mwaka 2015/2016 ambapo jumla ya wanafunzi
122,486 wamenufaika.
Hayo yamesemwa na Meneja wa Habari Elimu na
Mawasiliano wa Bodi ya Mikopo kwa wanafunzi
wa Elimu ya Juu Bw. Omega Ngole wakati wa
mkutano na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es
salaam.
“Walionufaika na mikopo katika kipindi cha
2015/2016 ni wengi na haijwahi kutokea katika
Historia tangu kuanzishwa kwa Bodi na haya ni
matokeo ya utendaji mzuri wa Serikali ya awamu
ya tano “alisisitiza Ngole
Akizungumzia utolewaji wa mikopo Katika kipindi
cha mwaka 2014/2015 Ngole alibainisha kuwa
jumla ya wanafunzi 99,069 walipata mikopo na
jumla bilioni 341 zilitolewa .
Pia Ngole alibainisha kuwa Serikali imeongeza
idadi ya wanaufaika wa mikopo kwa kuzingatia
vipaumbele vinavyotokana na mahitaji ya Taifa.
Ngole amebainisha kuwa mafanikio hayo ni
matokeo ya utekelezaji wa Falsafa ya Serikali ya
awamu ya tano inayosema Hapa Kazi tu.
Aliongeza kuwa Bodi hiyo inaendelea kufanya kazi
kwa kuzingatia kasi ya Serikali ya awamu ya tano
itakayowezesha kutoa mikopo kwa wakati kwa
kuzingatia sheria Kanuni. na Taratibu za utoaji
mikopo.
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya juu ni
Taasisi ya Serikali iliyoanzishwa kwa mujibu wa
sheria Na.9 ya mwaka 2004 na kuanza rasmi
mwezi julai, 2005 ambapo Katika mwaka wa
Masomo 2005/2006 idadi ya wanafunzi waliopata
mikopo ilikuwa 42,749 ambapo jumla ya bilioni
56.1 zilitolewa.

NINI MAONI YAKO.
 
Natamani na mimi niwe miongoni mwa wale wanakubaliana na tambo za Bw NGOLE msemaji wa bodi!
 
Back
Top Bottom