MWAISEMBA CR
Member
- Apr 21, 2014
- 90
- 83
BARUA YA WAZI KWA VIONGOZI WA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)
Yah: Tathmini ya Kampeni ya “No Reform No Election” na Mapendekezo ya Hatua za Haraka
Viongozi wangu wapendwa,
Kwa heshima na taadhima, ninawandikia barua hii kama mwanachama mtiifu wa CHADEMA, mwenye mapenzi makubwa kwa chama chetu na dhamira ya kuona Tanzania yenye demokrasia ya kweli, uchaguzi huru na wa haki.
Hakuna shaka yoyote kuwa hoja ya “No Reform No Election” ilikuwa na nguvu kubwa kisiasa na ilileta hamasa, mijadala na uelewa mkubwa kuhusu udhaifu wa mfumo wetu wa uchaguzi. Tulituma ujumbe wa kishujaa kwa watawala uliyobeba matumaini ya Watanzania waliochoshwa na chaguzi zisizo na haki, vitisho, na tume isiyojitegemea: hatuwezi kushiriki mchezo ambao mshindi anajulikana kabla ya kura kupigwa.
Lakini baada ya muda kupita, nimefanya tathmini ya kina na nimeona udhaifu mkubwa uliotokea siyo kwenye hoja yenyewe, bali kwenye utekelezaji wake. Tulikosa Plan B,mkakati mbadala endapo serikali isingekubali mabadiliko tuliyoyataka. Matokeo yake, tumejikuta tumekosa nafasi ya kushiriki uchaguzi, tumepoteza baadhi ya wanachama, na chama kimeingia kwenye ukimya wa hofu na mkanganyiko wa kimkakati.
1. KUKOSA PLAN B: Kosa Kubwa la Kimkakati
Katika siasa, hoja nzuri bila mkakati wa kuisimamia ni sawa na bunduki isiyo na risasi. Tulipotangaza kutoshiriki uchaguzi, tulipaswa pia kuwa na njia mbadala ya kuendelea kushirikisha wananchi katika mapambano ya kisiasa endapo serikali ingetupuuza.. Lakini badala yake, tukaishia kutegemea presha ya kimataifa na matumaini ya miitikio ya wananchi bila maandalizi ya hatua za ndani.
Matokeo yake, serikali iliendelea na ratiba zake, chama kimebanwa na kesi, na wanachama wameachwa njia panda bila mwelekeo mpya wala mkakati mpya wa kisiasa unaoeleweka.Na sasa, kampeni ya No Reform, No Election imezimika bila muendelezo wala nguvu ya kutufikisha kwenye lengo kuu
Swali muhimu: Baada ya kusema hatushiriki uchaguzi, je tuliwaandaa wananchi kwa njia mbadala ya ushawishi wa kisiasa? Tulipanga nini iwapo chama kitapigwa marufuku kujihusisha na shughuli zake kama ilivyo sasa ?
2. KUSUSIA UCHAGUZI HAKUKUWA SULUHISHO PEKEE YA MAPAMBANO
Historia ya CHADEMA inaonyesha Mwaka 2010 na 2015 tulipenya kwenye ubabe, tukapata wabunge na madiwani wengi, na tukapanua mtandao wa kisiasa, kumbe tumeshawahi kushinda nafasi na kuimarisha ushawishi hata kwenye mazingira yenye mizengwe mikubwa. Kama tulifanikiwa kupambana wakati ule, kwanini leo tumeamua kukaa pembeni bila kupigana hata kidogo?
Siasa ni kama vita, huwezi kulia kwa sababu adui ana silaha, bali unapaswa kutafuta namna ya kumpiga licha ya silaha zake.Hatukupaswa kukataa kabisa uchaguzi tulipaswa kuingia na mbinu za kushinda licha ya upendeleo. Tungeingia kwa masharti yetu, tukasaini kwa tahadhari, tukajipanga, tukapambana. Siyo kwa kuamini utakatifu wa refa, bali kwa kushinikiza nguvu ya wananchi mpaka refa akose ujasiri wa kupindisha..
3. Athari za Kukaa Pembeni
Baada ya kujiondoa tumeacha pengo ambalo CCM imeendelea kupanua uwanja wa ushindani kwa kujisafisha kimkakati kupitia kura za maoni, na kuwasafisha wapinzani wa ndani yao ili kujionyesha kama mashujaa wa mabadiliko na kutupumbaza wafuasi wetu kwa kutufanya kushabikia migogoro ya ndani ya CCM badala ya kujenga ajenda zetu.
Wakati huu , Chadema tumepoteza nafasi ya kuwa kinara wa ajenda za taifa, na kwa sasa tumebanwa na kesi, ukimya kuhusu sera mbadala, na mkanganyiko wa kimkakati, kukosa dira ya wazi kuhusu nini kinafuata baada ya kampeni ya No Reform No Election.Matokeo yake, CCM imepata nafasi ya kufanya siasa bila upinzani wa kweli na tumeshuhudia wanachama wetu wakihama au kukata tamaa..
CCM hawajatushinda kwa hoja, bali wametushinda kwa kudhoofisha utendaji wetu kwa kutumia mkakati tulioujenga sisi wenyewe wa kususia uchaguzi bila mpango.
4. Mapendekezo (Way Forward)
Kwa nia ya kuimarisha chama chetu na kurejesha matumaini, napendekeza:
1. Kukaa mezani kufanya tathmini – kuunda jopo huru la wanataaluma wa ndani kufanya uchambuzi wa kina wa kampeni ya NRNE ili tujifunze tulipokosea na namna ya kurekebisha.
2. Uwazi wa uongozi – viongozi wakiri hadharani kuwa kimkakati tulishindwa, lakini tusibadili msingi wa kudai reform; badala yake tubadili gia.
3. Kuanzisha ajenda mpya nje ya uchaguzi – kwa kuwasiliana na wananchi kupitia mikutano ya kitaaluma, makongamano ya vijana na wanawake, majukwaa ya mitandaoni, na midahalo ya kitaifa kudai katiba mpya na mabadiliko ya msingi.Hii itasaidia kuendelea kuwepo kwenye mijadala ya kitaifa bila kujiondoa kabisa kwenye siasa ya nchi.
4. Kurejesha wanachama waliokata tamaa –uongozi kushuka kwa wanachama kwa mazungumzo ya ana kwa ana, kusikiliza hisia zao, na kuonyesha kwamba siasa ni mbio ndefu.
5. Kujenga ushirikiano mpya – kushirikiana na vyama vingine, asasi za kiraia, na viongozi wa kijamii wenye msimamo wa mabadiliko.
Sasa si wakati wa kulaumiana. Siasa ni mabadiliko na ni kujifunza. CHADEMA bado ni chama kikubwa na chenye mizizi ya matumaini kwa mamilioni ya Watanzania. Lakini mizizi hiyo inaweza kunyauka kama hatutaiwekea maji ya fikra mpya, mbinu mpya, na uongozi unaobadilika kulingana na hali halisi.
Kama tulikosa Plan B, basi tuandike ukurasa mpya wa siasa zetu. Ni heri tuwe na sauti bungeni na kwenye mijadala ya taifa, hata kama changamoto ni nyingi, kuliko kukaa kimya na kupoteza kabisa nafasi ya kushawishi mwelekeo wa nchi yetu.
Kwa heshima na mapenzi mema,
Mwanachama Mtiifu wa CHADEMA
ShujaaCRM