Mnyakarama
Member
- Jul 11, 2015
- 11
- 3
Umesema kweli ndugu yangu! Dr.Slaa alipata 26% akipambana na Rais aliye mamlakani tena aliekuwa ana kibindoni na 80%, Chadema ilikuwa na Mgogoro wa ndani na Zitto, haikuwa na Backup wala fedha za kampeni leo baada ya kazi kubwa ya uhamasishaji 2010-2015, sapoti ya umoja wa Ukawa, ukwasi wa fedha zilizotumika, mpasuko uliotokea ccm watu kuhama, ccm kuleta mgombea mpya n.k Wamepunguza kura za urais ccm kutoka 61% ya Rais Kikwete mpaka 58% za Rais Mteule Dr.Magufuli i.e only 3% tena baada ya wazee na kina mama wengi kuogopa fujo kupiga kura, Dr.Slaa alisema Siasa ni Science Mbatia akapinga akasema ni Sanaa saaa kaona matokeo ya sanaa za mgombea wake!
Slaa ni bora mara 200 kuliko Lowassa.Lowassa ni nguvu ya FEDHA na kumbuka kaanza kitambo 2008.Halafu Lowassa amekuwa "backed up" na UKAWA ambayo ni vyama vinne.Kwa vyama 4 plus Lowassa mwenye nguvu ya fedha 39% ni ndogo sana.SILAA WA 2010 WATU WALIMPENDA KUTOKA MOYONI KABISA NIKIWEMO MIMI SEMA CCM WALITUMIA UZOEZI WA MIAKA 50 NA NILIUMIA ALIVYOSHINDWA INGAWA ALINITOKA AKILINI ALIVYOANZA KUTUMIWA NA MBOWE-SAKATA LA ZZK.Lowassa kaua vyama 4 kwa mpigo.SUBIRI MTAFUTANO UANZE MAANA KUNA (TeamLowassa,4U Movement,CDM Asilia,NCCR Mageuzi,NLD na CUF).
Mzee naomba ufafanuzi kuhusu utaratibu wa kupata viti maalum.Kigezo ni kipi, ni idadi ya wabunge wa kuchaguliwa ama kura za urais?
Hujaelezea hapo katikati ya 2010 na 2015 effort aliyoweka Dr Slaa kuimarisha na kupanua chama..
Ukweli ni huu, siku Lowassa amepitishwa na UKAWA kugombea, CCM ilifanya sherehe maana walijua hiyo move ingekuwa mwanzo wa mwisho wa agenda ya ufisadi (agenda pekee iliyoipandisha chadema chati)...In short, watu wenye akili (wanajiita Chadema Halisia) walishtukia sanaa za Mbowe na wakakaa pembeni...
Sasa tumeshuhudia Lowassa akisimama majukwaani pamoja na rejects- Kingunge, Lau Masha, Sumaye and the likes...
Imagine hayo majukwaa yangekuwa replaced na Dr Slaa na Lipumba!
#MboweMustGo
Mzee Tupatupa wa Lumumba,
Kwanza nikupe big up kwa kuliona hili ambalo ni ukweli mtupu. Kuna watu wamembeza sana EL baada ya kujiunga na CDM/UKAWA wakisema kuwa hawezi kumfikia Dr. Slaa. Mimi niliikuwa nawashangaa sana. Nidhahiri kuwa wamegundua kosa lao kwamba hawakuwa sahihi.
Kwa taarifa tu ni kwamba kama Serikali ya Madikteta wa CCM wasingefanya Uchakachuaji ikiwa ni pamoja na kuwadhibiti watu wa IT wa CDM/UKAWA ili kuvuruga majumuisho ya kura za UKAWA nina hakika CM wasingelipenya safari hii.
Tuna hakika Magufuli anajua, Kiwete anajua na CCM wanajua kuwa KURA zilizomwingiza JPM Ikulu ni kura za wizi na hivyo basi Urais wake ni haramu.
Unapotosha kasome katiba ! ni idadi ya kura wanazopata wabunge kiuwiano ndio zinazoamua ugawanaji wa viti maalum
Lowassa amesaidia kupoka ngome mbalimbali za CCM na kuzikabidhi CHADEMA na CUF. Mwaka huu, kwa uwiano wa kura za wagombea wa Urais wa Tanzania, CHADEMA itapata nafasi za viti maalum kwa wingi zaidi na kutoachwa mbali na CCM kama ilivyokuwa mwaka 2010. Haya pia ni mafanikio yaliyoletwa na Lowassa huko CHADEMA na kumzidi kwa mbali Dr. Slaa wa mwaka 2010. CHADEMA ilicheza karata zake vyema.
Kila la kheri watanzania!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
sawa mkuu ila hatukushindwa katika box la kura tumeshindwa na ubabe wa jk &co.
Angalia uwiano wa kura, siyo idadi ya kura...maana yake linganisha 26.34% za Slaa dhidi ya 39.97% za Lowassa.Wakati ule haukuwa muungano kama sasa, na wakati ule wapiga kura hawakuwa wengi kama mara hii, mara hii wamekuwa mara 2 ya 2010, kama unatazama hivyo Hata magufuli kapata kura nyingi zaid ya kikwete 2010
<br>Wakati ule haukuwa muungano kama sasa, na wakati ule wapiga kura hawakuwa wengi kama mara hii, mara hii wamekuwa mara 2 ya 2010, kama unatazama hivyo Hata magufuli kapata kura nyingi zaid ya kikwete 2010
<br>
Angalia uwiano wa kura, siyo idadi ya kura...maana yake linganisha 26.34% za Slaa dhidi ya 39.97% za Lowassa.
Slaa ni bora mara 200 kuliko Lowassa.Lowassa ni nguvu ya FEDHA na kumbuka kaanza kitambo 2008.Halafu Lowassa amekuwa "backed up" na UKAWA ambayo ni vyama vinne.Kwa vyama 4 plus Lowassa mwenye nguvu ya fedha 39% ni ndogo sana.SILAA WA 2010 WATU WALIMPENDA KUTOKA MOYONI KABISA NIKIWEMO MIMI SEMA CCM WALITUMIA UZOEZI WA MIAKA 50 NA NILIUMIA ALIVYOSHINDWA INGAWA ALINITOKA AKILINI ALIVYOANZA KUTUMIWA NA MBOWE-SAKATA LA ZZK.Lowassa kaua vyama 4 kwa mpigo.SUBIRI MTAFUTANO UANZE MAANA KUNA (TeamLowassa,4U Movement,CDM Asilia,NCCR Mageuzi,NLD na CUF).
Nakubaliana na wewe asilimia 200, Lowassa amepata backup ya Ukawa na mabilioni ya kwake binafsi wakati Dr.Slaa alipeperusha bendera ya CDM na kutangaza sera ya chama.
Please! Chadema haijaanza kujulikana baada ya Lowassa kulipa ile application/entrance fee ya 12bn! Dr Slaa amefanya chama kijulikane toka 2010 na zile Operesheni Sangara etc..watu wakakielewa ipasavyo...leo unakuja hapa kusema Lowassa ndo ametangaza chama..plsPamoja na hayo ufahamu vile vile dr slaa hangeweza kupatia ukawa ushindi huu. Kampeni za mwaka huu fedha zilitumika sana na nafasi ya lowasa kifedha imeisaidia sana ukawa.
Kwa hiyo unataka kutuambia kwamba effect ya kura hizo ni additive? kama ndio lengo lako, tuambie wale WAPENZI na MASHABIKI wa LIPUMBA walimpigia kura nani wakati inasadikiwa kuwa Lpumba ameondoka UKAWA kwa sababu ya kutoridhishwa na mwenendo wa mambo...Hauoni kwamba kura nyingi za Lipumba zilielekezwa CCM na si Chadema, kwa mtazamo huo ulionao? Huoni kwamba wapo wengine walimpigia kura Magufuli kwa sababuu tu wameumizwa na kitendo cha Dr. Slaa na Lipumba "kufukuzwa" na vyama vyao? na bado Lowassa amepata almost 40%, kwa sababu watu wanampenda na wapo pia watu ambao wanapenda sera mbadala za UKAWA. Usihamishe kura za mwaka 2010 ukaleta 2015, maana theoretically, baadhi ya kura za Lipumba na Dr. Slaa zimeenda CCM na ACT mwaka huuNadhani wewe ndio unaropoka, hebu chukua kura za lipumba 2010 add za Slaa 2010 , Halafu chukua za wale washirika pia,add kwa Slaa,Halafu chukua wapiga kura wa 2010 na wa sasa utapata jibu, sijaona ongezeko lolote la kura za lowassa, hata kama ukawa wangekuwa lema hizi hizi kura zingefika