Tathmini inaonyesha UKAWA itashinda Urais

Tathmini inaonyesha UKAWA itashinda Urais

ibange

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2010
Posts
1,543
Reaction score
553
Kwa tathmini yakinifu, mwaka 1995 upinzani uligawanyika sana na hukuwa na mipango yeyote ya maana. Hata hivyo upinzani ulipata kura za urais asilimia 40%. Mwaka 2010 upinzani pia ulikuwa dhaifu na hawakuwa wamejipanga vema. Hii kasi ya CHADEMA mnayoiona imeanza baada ya uchaguzi wa 2010.

Hata hivyo upinzani ulipata 40%. Je, kwa kazi yote iliyofanywa kujenga upinzani mashinani, muungano wa vyama na Lowassa factor, hawataweza kuzima pengo la kama 15%?

Mimi naona wataziba na hapo ndipo tathmini ya mtu kukaa mezani tu bila hata kwenda field itaonyesha wazi kuwa upinzani utashinda kwa kishindo.

Ila kwa Ubunge nina mashaka kama upinzani unaweza kupata 50%+ ya viti vya Ubunge.
 
Kumbuka safari hii huyo Zombie anaenda kusimama mbele ya Tingatinga!! AKA Earth Moving Equipment...Pichu lazima ziwabane
Kibaka ataishia kuwa rais wa Chadema
 
ibange

wewe ni redet mpya nini? Maana vitakwimu uchwara vimeeza tena vilikuwa vimeisha,
 
Last edited by a moderator:
Endeleeni kujifariji kwa ndoto na mawazo ya kufikirika. Wenzenu wanatafuta ruzuku ili waendelee kuzipiga, nyingi mnashabikia tu.
 
ibange

Kama ubunge hawawezi kupata 50% + hata urais hawawezi!Kama CCM hushinda zanzibar sioni ukawa inawezaje kushinda bara
 
Last edited by a moderator:
Kilichoifanya Chadema ipate 40% mwaka 2010 unakijua???
 
Kilichoifanya Chadema ipate 40% mwaka 2010 unakijua???

Hapa ndipo kwenye hekima juu ya swali hili wengi hawajui suala hili ndio maana wanaropoka hovyi waelevu tunawahurumia tu na siasa zao hawataamini matokeo ya mwaka huu jinsi kura zitakavyo pungua upinzani na kwa kulijua hilo ndio maana chadema wamejishikilia ukawa sababu wanajua ushindi wao wa 2010 ulitokana na nini.
 
Mimi naunga mkono tathmini hiyo mwaka huu ila indication ni kwamba ukawa itashinda kwa kishindo. Ufisadi si hoja na Lowassa atapangua hoja zote
 
Ukawa peke yao walikuwa wanauwezo wa kushinda kwa kishindo bila Lowassa , baada ya kushitukia goli la mkono zilifanyika jitihada kubwa kuzuia goli la mkono kwa kumkaribisha Lowassa ndani ya ukawa.
 
hapo kwenye ubunge ccm ndo wanahofu kama watapata 50% na sio upinzani
 
Naliona anguko la ccm naiona Tanzania mpya ukawa ni ushindi
 
Back
Top Bottom