Tathmini: CCM imesimama kwenye hoja, wengine wanatoa vioja

rose mzalendo

Member
Mar 5, 2019
71
114
Na Mwamba wa Kaskazini

Tunaweza kukubaliana kuwa kuna viashiria vya awamu ya kwanza ya ampeni za uchaguzi kwa ajili ya Urais wa Jamhuri ya Muungano imekamilika na vyama na wagombea vinajipanga kuendelea tena na awamu nyingine.

Hii ni baada ya kuoneakana wazi kuwa wagombea wa Urais karibu wote wamepita Mikoa kadhaa, kubadili baadhi ya mbinu ikiwemo wengine kutokomea nje ya Nchi. Kwa upande wa Zanzibar Kampeni zinatarajiwa kuanza wikiendi hii.

Tathmnini fupi niliyoiona ni kama ifuatavyo:

1. CCM: Mgombea wake amejikita kuelezea mambo aliyoyatekeleza kulingana na Ilani ya chama na atakayoyatekeleza katika kipindi cha miaka mitano ijayo. Amefanikiwa kufanya kampeni ya kiwango cha juu, na ya kistaarabu. Amepita mijini na vijijini kwa gari, ameelezea mafaniko yake na Changamoto alizokutana nazo pamoja na kujenga hoja ya kwa nini apewe miaka mitano tena ili amalizie utekelezaji wa mambo ambayo bado.

Ninachoweza kusema ni kuwa Dkt. John Pombe Magufuli anakipawa cha kuongea, kushawishi na kujenga hoja. Amesadifu kile wachambuzi wa ubora wa wagombea wanachokisema katika "*Say It Like Obama; The Power of Speaking With A Purpose and Vision*."

Katika fasihi hiyo mwandishi Shel Leanne, anasema ubora au udhaifu wa kiongozi unaweza kuonekana vyema katika hotuba zake anapoweka na kuainisha mtazamo wake, anapojenga hoja zake na anapoainisha mikakati yake.

Katika siku takribani 10 alizozofanya kampeni Mgombea wa CCM Mhe.Rais Dkt.John Pombe Magufuli amethibitisha si tu ana kipawa cha kuongea with a "purpose and vision" bali ameonesha anajambo lake la kukamilisha mageuzi aliyoyaanzisha ili kuwaletea wananchi maendeleo.

Ndiyo maana, hata Msemaji wa CCM, ndugu Polepole alipozungumza na Waandishi Habari Wilayani Chato alikuwa akijiamini kuwa kama uchaguzi ungefanyika Siku hiyo Mgombea wa CCM Dkt Magufuli angeshinda kwa zaidi ya asilimia 85.

2. ACT- Wazalendo: Kuna mwanafalsafa mmoja wa kale aliwahi kusema vitendo huongea zaidi ya maneno "*actions speak louder than words*".

Ukiangalia kauli alizokuwa akizitoa kiongozi wa Chama hicho Zitto Kabwe kuwa wao ndiyo mbadala wa kupambana na CCM na kwamba wanasubiri kampeni waoneshe uwezo wa Chama hicho katika siasa, unaweza leo ukakitathmini chama hicho kwani hakionekani kama kipo katika kampeni au la.
Kimedorora, kimeshindwa kufanya siasa, kujitangaza wala kunadi sera zake na zaidi mgombea wake kaweka rekodi ya dunia kwa mgombea Urais wa kwanza kutumia zaidi ya wiki moja kufanya kampeni mkoani kwao kama mgombea ubunge hivi na kisha kuacha kampeni na kukimbilia nchi za nje!

Kiongozi Mkuu wa Chama Zitto amebakiki kutoa maneno tu mitandaoni huku akiweka rekodi ya kupanda ndege ya Bombardier Q400 tarehe 11/09/2020 kutoka Dar kwenda kwao Kigoma, huku akisahau kuwa aliyowahi kubeza ndege hizo kuwa ni maendeleo ya vitu na si watu na kuhoji usalama wake akidai zilikuwa si mpya bali za zamani zilizotolewa huko Vietnam!!.

Kwa kifupi ACT-Wazalendo ni chama Chenye maneno mengi lakini katika siasa kimeshindwa na ni dhahiri kimekwama na zipo tetesi kuwa mgombea wao wa Urais Ndugu Membe, kama atarudi kutoka Dubai alikoelekea tarehe 10/09/2020, basi huenda akajiunga na Chadema. Kwa kifupi wanaonekana wako hoi kisiasa na hata kifedha.

3. CHADEMA: Kama kuna mgombea ambaye anatangazika kifalsafa, kisiasa na kiuchaguzi ni Tundu Lissu. Ni mwanasiasa ambaye ana hulka mbili.
Mosi, kuona kwamba kila kilichofanyika katika Nchi yake ni kibaya lakini hicho hicho kikifanyika kwa wazungu ni kizuri. Amekuwa akibeza ununuzi wa ndege, ujenzi wa barabara, viwanda, madaraja, anawaponda viongozi, watumishi wa umma na majaji kuwa hawajui Kiingereza,

Pili, ni mwanasiasa ambaye unamuona kabisa kuwa amebadilika kutoka yule mpinga ubeberu na sasa amekuwa "compromised" hadi kuwa wakala wa mabeberu.

Na anasema wazi katika kampeni zake kuwa wazungu wanafuatilia, akionewa kuna wazungu watamsaidia!!! Ni kiongozi, huenda wa kwanza Afrika, anayesema wazi na anayetamka wazi kuwa kuwa atawaita wazungu kuingilia kati masuala ya Nchi yake.

Ni mwanaharakati mropokaji asiyetoa matumaini yoyote katika maisha ya Watanzania.

Anatanzika asimamie hoja gani? Hawezi kuahidi barabara kwa sababu alikosoa ujenzi wake kuwa si maendeleo ya watu, hawezi kuahidi viwanda, hawezi kuahidi kuendeleza miradi mikubwa na yenye faida kwa wananchi kama SGR, Mradi wa Umeme Rufiji kwa sababu vyote amevikosoa.

Lakini alikosoa ndege ambayo saizi anatumia kufanya kampeni tena akiruka na kupishana na wananchi wengi na kutua kwenye vituo mahsusi vya mijini ambako kazi kubwa ya kuzoa watu kwa malori inakuwa imefanyika ili walau kumuondolea aibu ya kukosa watu.

Ukitaka kujua jamaa ametanzika angalia hata Msemaji wa Chama chake mara ambazo ametoa taarifa za Chama hicho mpaka sasa, tofauti na kule CCM yameelezwa masuala na hoja na udhubutu walionao, huku ni CHADEMA wakiendelea na malalamiko ya "tumenyimwa kibali cha kurusha ndege (wakati wamekiuka masharti ya usafiri wa anga), tunaonewa, tutavunja baadhi ya taasisi za umma n.k. " Yani ni Chama cha malalamiko na hakitangazi Ilani ya chama kwa sababu Inamapungufu mengi kwani kuna kifungu cha kuweka rehani Madini ili kuchukua mikopo kwa Mataifa ya nje.

Vyama vingine vya kisiasa kama CHAUMA na NCCR_Mageuzi kimsingi vipo na vinafanya kampeni lakini bado havijajipambanua kwa hoja za masingi, hata hivyo vinasaidia kuhubiri amani na upendo kwa Watanzania.

Niite Mwamba (mara 3) wa Kaskazini.
 
Lissu anatoa umbeya kwenye jukwaa la kuomba kura za Rais, nadhani hajajua ukubwa wa dhamana aliyopewa na chama chake
Halafu Sera zake ,ni kumuongelea Magufuli tuuuuuu!Tatizo ni kuwa ,si kila MTU anatakiwa ,awe Rais.Rais anaandaliwa.Pia vyama vya upinzani ni vya watu binafsi.Chadema mwenyekiti wa kudumu Mbowe,ACT -Kiongozi wa kudumu-Zitto.Pia wanadai katiba mpya ,lakini hawadai,tuwe na vyama vya umma.Chama cha umma ni kimoja ,ccm tu.
 
Shauri yao Chadema, sisi Watanzania wote October tupo na Rais Magufuli tu, wala hatutegemei Wazungu watupigie kura
Halafu Sera zake ,ni kumuongelea Magufuli tuuuuuu!Tatizo ni kuwa ,si kila MTU anatakiwa ,awe Rais.Rais anaandaliwa.Pia vyama vya upinzani ni vya watu binafsi.Chadema mwenyekiti wa kudumu Mbowe,ACT -Kiongozi wa kudumu-Zitto.Pia wanadai katiba mpya ,lakini hawadai,tuwe na vyama vya umma.Chama cha umma ni kimoja ,ccm tu.
 
Ccm hawana hoja yoyote mpya zaidi ya ndege, SGR na madaraja huku watu wakikosa huduma za msingi kama dawa na maji.
 
Kwa kifupi tu Lisu anaturejesha kule tulipotoka ,

Kuwa koloni la wazi kabisa la mabeberu.
 
Wanatapatapa
8b8772af65a848b2211cc750a1e7211b.jpg
 
Back
Top Bottom