Tathimini fupi tu ya "elimu bure"

Tathimini fupi tu ya "elimu bure"

hhhhj

Member
Joined
Oct 5, 2016
Posts
41
Reaction score
68
Mwanzoni mwa mwaka huu baada tu ya raisi JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI kuapishwa kuwa raisi alitangaza rasmi azma yake ya elimu bure kama alivyoahidi kupitia ilani ya chama cha mapinduzi katika kampeni zake za uchaguzi....

Ifahamike kuwa kwa kipindi hiki alikuwa hana waziri hata mmoja bali makatibu tena wauongozi uliopita.Tena hakuwa nabajeti yake bali ilikuwa ya 2015/2016 kwa hili tulimpongeza sana tukiamini alithubutu na akaweza.....

Elimu bure hii ilikuja na nyongeza kubwa ya changamoto na nyengine soon madhara yake tutayaona(matokeo ya kidato cha nne mwakani)Baadhi ya changamoto hizo ni:-

ONGEZEKO LA WANAFUNZI DRS LA KWANZA
Kwanini waliongezeka!!!???
Ikumbukwe kuwa kwa kipindi kirefu sasa shule za msingi hazilipi ada bali baadhi ya shule walikuwa wanamicho midogomidogo(hasa mijini) naambayo haikuwa kikwazo sana bali baadhi ya wazazi walitumia ile kama kisingizio cha kutokupeleka watoto wao shulel...

Baadhi ya michango hiyo ilikuwa ni t-shirt,lebo,tai,pesa ya mlinzi n.k ambapo kimsingi ukiondo mchango wa mlinzi vengine vipo kama kawaida....
Kutokana na tangazo la ELIMU BURE ili walazimu wazazi wakosekisingizio na kupeleka watoto wao hata wale walio waficha na walio pitiliza umri......

MATOKEO YAKE NINI????
Kuna matokeo ya namna mbili yalitokea ambayo nayoyalitatuliwa kisiasa(political technique) matokeo hayo ni:-
1-Uelewa wa tamko(ELIMU BURE)
2-Upungufu wa miundombinu(majengo,madawati,walim)

UELEWA WA TAMKO
Wazazi wengi waliifahamu elemu bure ya nyerere ndiyo walihisi wataikuta kwa magufuli na ndiyo maana wagombea wote wa uraisi walipo itaja ELIMU BURE walishangiliwa sana kwani walijua ileee ya nyerere inarudi.....

Elimu bure ya Nyerere ilikuwaje?
Wakati ule ilikuwa daftari, peni, uniform na vyengine vyote utavipata bure shuleni na hii ndiyo tafsiri sahihi ya ELIMU BURE......

Serikali ikafanya nini?
Baada ya wazazi kutokukiona walichokitarajia ikaanza misuguano baina ya walimu na wazazi na ndipo serikali ikaleta waraka namba tano wa ELIMU BURE.Nakatika waraka huu ndipo ukatoa majukumu ya kila mmoja yaani MZAZI, MWALIMU, SERIKALI.

Nakwakutokana na waraka huu jina likabadilika kutoka ELIMU BURE hadi ELIMU BILA MALIPO. Yaani bado mzazi kunagharama zitaendelea kumuhusu. Na hapo ndipo ukavuruga watu....

.itaendelea
 
Hiyo elimu bure omesababisha watu hasa shule za government wasifanye mtihani wa kujipima kanda (zonal mock examination)... Ngoja tuone movie inavyoendelea
 
Back
Top Bottom