Taswira ya kuwasili nchini mwili wa baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Taswira ya kuwasili nchini mwili wa baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Just Pray

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,142
Reaction score
4,779
Leo imepita miaka 26, sawa na miezi 312, wiki 1,357, siku 9,497, saa 227,912, dakika 13,674,730 au takribani sekunde 820,483,818 tangu tarehe 14 Oktoba 1999 — siku ambayo Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, alifariki dunia katika Hospitali ya Mtakatifu Thomas, London.

Kipindi hicho, vyombo vya habari vilifanya mikutano ya dharura kupanga namna bora ya kuripoti msiba huo mkubwa wa kitaifa, kuanzia safari ya mwili kutoka Uingereza hadi mazishi Butiama.

Siku mbili kabla ya siku ya kuwasili mwili yaani Oktoba 18, 1999, ratiba rasmi ilitangazwa — Baada ya jeneza kuwasili kutoka Uingereza lingepitishwa kupitia barabara za Pugu (sasa Nyerere), Nelson Mandela, Ubungo, Morogoro, Magomeni Mapipa, Kawawa, Ali Hassan Mwinyi, Maji Machafu, TPDC Mikocheni hadi Msasani.​


Mpiga picha, Issa Michuzi

Kwa upande wangu, mimi siku mmoja kabla nikafanya “raking” ya njia yote nikitafuta eneo sahihi la kusimama. Nilichagua daraja la Manzese, kwani niliona ndilo eneo pekee la kuniwezesha kunasa taswira ya ya mambo makuu matatu kwa mpigo- msafara mzima, jeneza lenye mwili wa marehemu na maelfu ya waombolezaji pande zote za barabara.

Kumbuka kipindi hicho drone hazikuwepo. Ila nashukuru Mungu taswira ambayo niliibuni siku moja kabla ya siku la tukio nikafanikiwa kuinasa.

Baada ya msafara kupita, mimi na dereva wa ofisini tukakatisha njia ya mkato ya Tandale hadi Kijitonyama. Tukawahi kufika Msasani takriban nusu saa kabla mwili haujafika.

Hadi leo nahisi fahari na unyenyekevu na kumshukuru Mungu kwa kuniwezesha kuchangia kidogo nilichojssliwa nacho katika kuhifadhi kumbukumbu ya mwisho ya kiongozi aliyebeba matumaini ya taifa letu.​
565522686_1189790636358536_279179646558432142_n.jpg
 
Back
Top Bottom