Taslima: Ninatosha uenyekiti CUF

Taslima: Ninatosha uenyekiti CUF

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
14,242
Reaction score
34,917
IMG_1346-620x308.jpeg

Taslima ambaye kwa taaluma ni Mwanasheria ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akijibu swali la mwandishi wa habari lililohoji kuwa kama anavigezo na sifa za kumshinda aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha CUF Pro. Ibrahim Lipumba katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Agosti mwaka huu.

Aidha, Taslima amesema kuwa wanachama wa CUF na wananchi kiujumla wanatakiwa kujua kwamba kauli aliyoitoa Lipumba hivi karibuni ya kutengua barua yake ya kujiuzulu aliyomwandikia Katibu mkuu wa chama hicho Maalim Seif Shariff Hamad, haitazuia uchaguzi wa chama hicho kufanyika.

“Tulitaka tuweke mambo sawa kwa wananchi kwamba kauli ya Lipumba ya kutengua barua ya kujiuzulu kwake haimaanishi kwamba bado anashikilia wadhifa wa uenyekiti, bali kamati ya uongozi iko pale pale hadi mkutano mkuu wa kuchagua viongozi utakapofanyika,” amesema Taslima.

Amesema kauli inayotolewa na baadhi ya wananchama wa CUF ya kwamba hakuna mwanachama wa chama hicho mwenye uwezo wa kurithi na kuvaa viatu vya Lipumba si ya kweli na kwamba wako wanachama wenye uwezo huo na zaidi.

“Hao wanachama wanaosema kuwa Lipumba kwanza chama baadae na kwamba hakuna mwanachama atakayeweza vaa viatu vyake si wa kweli, chama hiki ni cha kila mtu na nafasi za uongozi zinastahili kugombaniwa na kila mtu,” amesisitiza
 
Tushasahau mambo ya Jecha na ZEC sasa tunajadili Uenyikiti wa chama
 
Twaha Taslima mwepesi sana kwa Lipumba,labda Lipumba akatwe kutoka mtendeni
 
Ukawa wameshindwa kabisa kuwasaidia cuf zanzibar wanachoona kuwa wameporwa.Ni ukawa ndio waliowashawishi cuf zanzibar wasuse,ili wasaidiane kuipiga pressure serikali ya muungano

Matokeo yake ukawa wanalilia tv live,wanagombana na naibu spika makusudi ili wafukuzwe bungeni

Sasa cuf wanahitaji mtu mwenye uchu wa madaraka kama Lipumba aje kutoa changamoto kwa magufuli kuhusu zanzibar

Ukawa wameshindwa,kuitetea cuf,na cuf imekufa bara,Twaha Taslima si aina ya kiongozi anaetakiwa na cuf kwa sasa,hana mvuto hana tofauti na Mashinji
 
Toka lini ccm ikaishauri Ukawa?
 
Huyo taslima kaifanyia nin cuf? hamwezi lipumba ki hoja, kielumu na hata kimapambano sasa hapo ndio mtatambua jinsi chama kinavyoenda mrama endapo lipumba hato pitishwa
 
Back
Top Bottom