Tasaf kuonyesha umahiri wa kunusuru umaskini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tasaf kuonyesha umahiri wa kunusuru umaskini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Jun 14, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 14, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf) utapata nafasi ya kuonyesha uzoefu wa kunusuru makundi yaliyoathirika zaidi na umaskini katika kongamano litakalowashirikisha wajumbe 200 kutoka nchi 42.
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tasaf, Ladislaus Mwamanga, alisema uzoefu huo ni pamoja na utekelezaji wa miradi ya ujenzi na namna ya kuwahusisha wanawake katika miradi hiyo.
  Mwamanga alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana.
  Alisema kongamano hilo la mafunzo ambalo limeandaliwa kwa ushirikiano na Benki ya Dunia, litafunguliwa na kiongozi wa ngazi ya juu serikalini na litafanyika mjini hapa kuanzia Jumatatu ijayo hadi Ijumaa.
  “Tanzania itatoa mada ya kuonyesha jinsi ilivyotekeleza miradi ya ujenzi na namna ya kuwahusisha akina mama katika ujenzi…akina mama kushiriki wao katika miradi hiyo ni zaidi ya asilimia 40 na wapatapo hizo fedha zinatumika zaidi kwa matumizi ya nyumbani,” alisema.
  Alisema Tasaf ambayo ina uzoefu wa kazi za miradi kwa muda wa miaka 10 sasa, tayari imekwishatekeleza miradi ya kijamii zaidi ya 11,375 kati ya maombi ya miradi laki moja.
  Mwamanga alisema miradi hiyo yote ina thamani ya zaidi ya Sh. Bilioni 197.
  Akizungumza katika mkutano huo, Mtaalamu wa Maslahi ya Jamii kutoka Benki ya Dunia, Azedine Ouerghi, alisema azma ya kufanya kongamano hilo nchini ni kutaka washiriki wapate uzoefu mkubwa ambao Tasaf inao katika kuwashirikisha wananchi kwenye maendeleo.
  “Dhana ya kongamano hilo ni kutumia utaratibu wa shirikishi badala ya ule wa kutoa maagizo kutoka juu kwenda kwa wananchi.  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
   
Loading...